Hii inakera aisee!

Hii inakera aisee!

Killeville

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2015
Posts
410
Reaction score
1,218
Hapa tutakuwa tunatupia mambo yanayokera katika jamii,kama vile tabia zikerazo,vijimambo na issues nyingine zikerazo,lengo ni kuwazindua wahusika "Acheni hizo"

Zinikerazo mie
1. Mama ntilie kumfuta mwanae kamasi kwa mkono-kavu halaf kuendelea kuwahudumia wateja bila kunawa.INAKERA
2. Jamaa katoka 'kuchimba viazi' na ulimwona hakunawa,halafu anakupa mkono kukusalimia.INAKERA
3. Unakuta kidume hakijishughulishi na kazi yoyote,halafu mishe zake ni "Oya ntoe buku nkapone".INAKERA

Endelea kutupia zingine.
 
Mama mwenye nyumba kumchunguza mpangaji wake amepika nn inakera
 
Mwanaume kupendwa na Wake za watu,wanafunzi na wanawake wa humu JF wenye avatar fake inakera sana aiseee
 
Kwenye daladala mtu kalowa jasho halafu anakuegemea😀
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom