Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,592
- 11,831
Ni hivi wandugu
Kuna jamaa wetu hapa amejikiuta kwenye matatizo makubwa kifamilia.
Chanzo ni kwamba amempenda mdogo wa mke wa kakayake (kitamaduni zetu ni shemeji yake) huyu binti wamezaliwa tumbo moja na mke wa kakayake ambaye ni brother wake wa damu.
Jamaa anaeleza kuwa walianza mahusiano kitambo na huyo dem tangu wakiwa wanasoma waliahidiana mengi ya kimaisha hasa kuoana, jamaa anakili kuwa huyu dem amemsaidia sana kimaisha hadi kufika hapo alipo.
Jamaa anasema umefika wakati sasa anataka kutimiza ahadi yake ya kumuoa lakini tatizo likaje upande wa wazazi wa binti wamekataa kabisa suala hilo wakidai ni kinyume na mila zao ndugu wawili wa damu kuoa familia moja,
Kwa kweli umekuwa mtafaruku mkubwa huku baadhi wakiunga mkono na wengine wakipinga vikali suala hilo.
Kibaya zaidi imegundulika tayari binti ana mimba ya jamaa.
Binti ametishia kujiua ikiwa ndugu zake wataendelea kushikilia msimamo wao wa kukataa kuolewa na jamaa lakini bado wazazi na ndugu wengine wameendelea kupinga hilo.
Mpaka sasa hali imezidi kuwa mbaya baada ya binti kutoroka kwako na kuhamia kwa jamaa, siku ya pili hii Sasa, wazazi wa binti wametoa onyo kuwa kama hata rudi nyumbani na kuachana na jamaa wao hawata mtambua kama mtoto wao.
Matatizo yamekuwa makubwa hadi sasa familia hazielewani.
Je wandugu hili linakuwaje ni halali kwa watu hawa kuoana na kama sivyo ubaya hasa uko wapi hapa?
Nini kifanyike katika hili na ni kweli kuwa kitamaduni za kwetu hapa TZ kuwa hili haliruhusiwi? Au ni kudhurumu tu nafsi za hawa wapendanao?