BABU KIZEE
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 452
- 72
Kuna jamaa mmoja ni mwanachuo alitokea kumpenda dada mmoja ambaye ni mwanachuo mara ya kwanza wamekutana kwenye discussion, jamaa akamwomba namba yule duu akampa alipohipata tu,jamaa akaanza kumtokea, yule duu akamjibu ana mtu wake lakini jamaa akulizika akaendelea kumfatilia ikafika wakati yule duu kubadilisha laini, jamaa alipoona hapatikani akaanza kupeleleza mpaka akajua room anapoishi akawa anaenda mara kwa mara kumtokea lakini wapi demu hataki ikafika muda yule duu akamwambia sikupendi lakini jamaa amekaza uzi tu,kuna siku jamaa alienda room kwake akamkuta demu yuko na kanga moja ametoka kuoga kama kawaida yule ,mwanamke alipomuona akakasilika na kumwambia atoke avae lakini jamaa hataki , akamwambia kwa upole atoke aje kesho ndo atakuwa na muda wataongea jamaa akakubali akatoka kesho yake akaja tena akamkuta anachemsha maji kwa ajili ya kunywea chai , akamwambia aingie anamchemshia chai yake jamaa akawa anafurahia sana akijua leo hatimaye kaingia laini ,yule akamwangalia na kutabasamu na kumwambia leo nakupikia chai na mkate na mayai jamaa akawa anafurahia mara yule duu akazima jagi la maji ya moto na kuchomoa waya wa jagi na kumwajia usoni maji ya moto, jamaa alipiga kelele na kutoka nje , yule jamaa akaaungua uso wake ukimuona amealibika sana usoni mpaka leo anakovu usoni.