Liverpool VPN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 7,589
- 17,736
Dah IMENIUMA japo HAYANIHUSU ila nimemuonea huruma sanaa mwamba.
Ni mwezi wa 12, Kama kawaida ikifika december au ikiwa inakaribia huwa nazama mikoa ya baridi kupanda miti. Safari hii nimekuja mkoa fulani hivi nyanda za juu kusini na lengo ni kupanda miti ya matunda.
Sasa katika hiyo guest house niliyoshukia huwa nawaona madada fulani wawili, mmoja ni mke wa mshkaji mmoja hivi ambae ni mtafutaji tu kama mimi ila yeye anakusanya mazao na kupeleka Dar. Huyu Mwamba huwa anakuja sanaa huku then imekua kama kwao na mzoefu sanaa wa huku.
Na huyu mkewe kampata huku huku kijijini. Kwahiyo akiwa huku anakuwa yupo kwenye mishe za kutafuta pesa na ni kwa wakwe.
Huyu dada mwengine hajaolewa. Sasa bana kilichonifanya niandike huu uzi ni jana bana.
Nimerudi mapema mchana kutoka shamba, kufika guest nikaagiza chakula (guest ina mgahawa). Mule kwenye mgahawa kulikuwa na madada wawili walikua wanaongea.
Kilichoniuma yule dada alimkandia sanaa mumewe halafu mwisho kabisa nikasikia Yule mwengine anasema.
"hapendwi mtu hapa inapendwa pesa"
"Toa pesa upewe mapenzi motomoto"
"nikulee bure wewe baba angu, hata huyo baba namlea bure kwasababu alitumia hela zake kunilea"
Dah ghafla mwamba (muuza mazao) akaingia. Wale madada wakabadilisha maongezi, nikasikia "mume wangu mzuri umerudi, vipi shamba jamani?"
Yaani aliongea mengi lakini nikiwaza vile alivyokuwa akimnanga huyu bwana dah niliuona unafiki kabisaa. Mara jamaa akaoga wakaingia ndani na mkewe wakajifungia.
Nilitamani kuwachana wale madada ila dah ndio hivyo hayanihusu. Mke na mume walivyoingia ndani nikamdadisi yule dada aliyebaki "Hawa wameoana?" akanijibu "Ndio na ubwabwa wao tulikula June mwaka huu..."
Dah nikajiuliza kimoyomoyo "ina maana hata kwa mumewe HAPENDWI MTU ZINAPENDWA PESA?""
1. Itakuaje siku mumewe mtaji ukikata?
2. Itakuaje siku mumewe kapata ugonjwa wa kumlaza kitandani muda mrefu?
3. Siku mumewe akipata mchongo mwengine akamuachia huu wa mazao mkewe, hivi mkewe si atahamisha hela zote kwake?
Dah nimejiuliza mengi ila ndio HIVYO HAYANIHUSU. Nikiwaona njiani vile wanapetiana naona kabisa mke anazipeti hela ila mumewe anamuona mbuzi tuu. Mlioa Mungu awape uwezo kuona unafiki wa wake zenu. Mnaotafuta wake dah kwa Hawa wanawake wa millennial wenye material love, MUNGU AWAONGOZE.
UZI TAYARI.
Nitaoa baadaye sanaaa, na la huyu Mwamba limezidi kupiga pin lengo langu la kuoa miaka mingi ijayo.
#YNWA