Hii Imekaaje?

Da Womanizer

JF-Expert Member
May 24, 2010
1,577
148
Leo wakati nasikiliza BBC asubuhi kuna watu walikuwa wanahojiwa kuhusu ajali iliyowahi kutokea huko nyuma kule Kongo mashariki. Ajali hii ni ile iliyohusisha lori la mafuta lililopata ajali ambapo kama kawaida ya waafrika wakakimbilia kwenda kuiba mafuta, kilichotokea ni lori hilo kulipuka na kuua idadi kubwa sana ya watu.
Sasa katika mahojiano hayo kuna watu wanajenga hoja kwamba ajali ile imetokea kwa sababu Mungu ndiye aliyepanga itokee. Hoja yao in kwamba iweje gari lile litoke kote huko lilikotokea lije kupata ajali mahali pale na kisha kulipuka.
Wanaosema hivyo wanaamini Mungu aliamua kuwaletea maafa kwa sababu wamemkasirisha sana Mungu.

Hivi hii style ya kumlaumu Mungu hata kwa mambo ambayo ni wazi yametokana na uzembe wa watu wenyewe imekaaje wadau??

Nawakilisha na naomba maoni yenu.

Kiranga nakusubiri kwa hamu hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom