Hii imekaaje?

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Wanajanvi, ninamtaji mdogo wa sh. 600,000 ninaotarajia kuanza nao katika biashara ya mkaa kutoka mbeya kuuleta hapa DAR.
Bei ya kununulia kule ni sh. 13000 kwa gunia ambalo huku nitauza kwa sh 30000 @. Naomba ushauri wenu njia ipi bora na ya ufanisi zaidi kusafilishia ikizingatia gharama za usafilishaj, au mahala pengine ninapoweza kuupata mkaa kwa bei ya chini zaidi.
Nawasilisha
 

Lady N

JF-Expert Member
Nov 1, 2009
1,916
129
mpaka ufike huku mjini esp dar maliasili sijui washa kukama mara ngapi!!!! kuna sehemu singida ndani2 huko yuko ancleangu wanauza 3000/=
 

Doltyne

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
442
166
Ili kusafirisha mkaa kutoka mkoa mmoja kwenda mungine, unahitaji usajili wa kutoa mkaa mkoa fulani mf mbeya, huu unalipiwa laki mbili na elfu tano, na unakoupeleka mf dar inabidi uwe umesajiliwa kama muingiza mkaa huku nako unalipa laki mbili na elfu 5.

Kila gunia linalipiwa kodi maliasili kiwango kati ya elfu 5 na elfu 6. Kwahiyo kila gunia litakucost elf 6 ya maliasili, elf 13 ya kununua na gharama ya kukodi fuso kutoka mbeya ambayo ni zaidi ya laki8. Kwani kutoka moro ni laki4 na nusu.

Maliasili sio tatizo kabisa kama umelipa kodi zote ipaswavyo. Na kama utakuwa na store yako ya kuuzia unahitaji leseni ya biashara nk.

Mkaa unauzwa elf 30 Dar sio kwakuwa watumiaji ni wengi na ni bidhaa adimu, la hasha, bali kwakuwa gharama za uzalishaji na usafiri ni kubwa mno. Minimum gunia moja linacost kama elf 22 kama kila taratibu ikifatwa. Ndio maana Dar unauzwa elf 30.

Kuutoa mkaa mbeya ni kuongeza gharama zaidi, nenda bagamoyo au morogoro (japo kwa sasa usajili wa maliasili umesitishwa mpaka watakapotangaza) au mikoa mingine ya karibu. Ambayo inachukua masaa chini ya matatu kufika dar utapata faida nzuri.
 

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Ahsante mkuu. Sasa kumbe kiasi nilichotarget chote kinaishia huku! Hebu nitafute plan b.
 

Doltyne

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
442
166
Kama unataka kufanya mkaa, unaweza kuuza rejareja, au ongeza mtaji ili uweze kuleta mzigo mkubwa. Kwa maisha ya sasa, laki sita ni mtaji ambao una matata kidogo kuleta tija.
 

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Wanajanvi, ninamtaji mdogo wa sh. 600,000 ninaotarajia kuanza nao katika biashara ya mkaa kutoka mbeya kuuleta hapa DAR.
Bei ya kununulia kule ni sh. 13000 kwa gunia ambalo huku nitauza kwa sh 30000 @. Naomba ushauri wenu njia ipi bora na ya ufanisi zaidi kusafilishia ikizingatia gharama za usafilishaj, au mahala pengine ninapoweza kuupata mkaa kwa bei ya chini zaidi.
Nawasilisha

Kachome wewe mwenyewe maeneo ya Mvomero. Bei itashuka
 

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Kachome wewe mwenyewe maeneo ya Mvomero. Bei itashuka
<br />
<br />
mkuu vip kuhusu gharama za kibali kama zilivyoelezwa hapo awali nazo zitapungua?
Halafu mvomero sijawahi fika, je miundombinu ya usafirishaji ikoje?
 

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Kama unataka kufanya mkaa, unaweza kuuza rejareja, au ongeza mtaji ili uweze kuleta mzigo mkubwa. Kwa maisha ya sasa, laki sita ni mtaji ambao una matata kidogo kuleta tija.
<br />
<br />
nashukuru mkuu. Ila ukweli ni kuwa changamoto ya kupata zaidi ya hapo ni kubwa sana. Lakini nashukuru na napokea ushauri na ntaufanyia kazi.
 

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
plan b:

maana una mpango wa mkaa tafuta wale wanaoleta kutoka polini nunua kwa jumla then tafuta wafanyabiashara mf mahoteli au migahawa au chips unawapelekea moja kwa moja ..
 

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Nimefika mbeya, bei ya gunia moja kutoka chunya ni sh.2000 na transport ni 6000 kwa gunia. Ila vibali ndo changamoto sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom