Hii imekaaje Vituo vya Redio kupishana muda?

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,584
2,000
Mimi kila alfajiri huwa nasikiliza RTD, ili kusikiza Usia wa baba, utabiri wa hali ya hewa pamoja na mambo mengine, na baadae nahamia RFA kusikiliza BBC.

Kwa wiki kadhaa sasa nimegundua ya kuwa Vituo hivi, yaani RTD na RFA wanapishana muda...kwani baada tu ya RTD kusema imetimia saa kumi na mbili kamili mimi ndipo nahamisha kituo kwenda RFA, cha ajabu sasa huwa nakutana na Muziki na mara Muziki utashuka na atasikika Mtangazaji akisema imebaki dakika moja itimie saa kumi na mbili kamili.

Sina uhakika kama ilikuwa hivi tangu muda mrefu lakini kwangu nimegundua hii tofauti kama wiki moja na siku hivi sasa..na nipo na ratiba hii kwa miaka.

Na nimelazimika kusikiliza kwa siku kadhaa ili kujiridhisha nisikurupuke na hali imekuwa ni hivyo hivyo, hata leo asubuhi.

Sasa je hii iko sawa au kuna kosa mahali?.
 

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,584
2,000
Nunua saa yako uwe unaitumia kuangalia muda... Simple
Sina tatizo na muda maana mimi ninazo sehemu kama nne ninazoweza kufuatilia muda...ninachotaka kujua mimi kama ni sawa wao kupishana na tupo kwenye nchi moja?

Kuna Watu wanaziamini sana Redio kwa suala la muda, na hata saa zao wanarekebisha kupitia redio.
 

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,584
2,000
Majira ya Mwanza na Dar tofauti kwa hiyo ndio maana umekutana na changamoto kama hiyo na ni kweli ulichokisema na mi pia nilishafatilia Mara kadhaa huwa Radio Free inachelewa kiasi
Ingawa mimi huwa naamini ndani ya mipaka ya nchi muda unapaswa kuwa sawa.
 

Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,451
2,000
Nje ya MADA

Edhi zetu waenga SAAza KIMWEKUMWEKU
Ilikuwa ufahari sana Majira ya saa yako kuendana sawa na radio
Yaan unasubiri ile saa 2 usiku
Pu pu pu pu pu puuuuuuu hivi sasa ni saa 2 kamili usiku
Radio ONE stereo inakuletea taarifa ya habari kutoka JIJINI DAR ES SALAAM
Msomaji wenu ni mimi JULIUS NYAISANGA Kwanza ni MUHTASARI wake

watu wawili wamefariki dunia na wengine 45 kujeruhiwa baada ya basi waliokuwa wakisafilia kuacha njia na kupinduk
Raisi wa MAREKANI bwana BILL CLINTON akutwa na kashfa ya ngono ya kutembea na sectretari wake

Na katika michezo timu ya YANGA yaibugiza MALINDI SC 3 bira na kutwaa kombe la muungano

HABARU KAMILI

Aisee mkuu ulivyotaja hicho kipindi cha WOSIA wababa umenikumbusha mbali
Hivi ile MAZUNGUNZO baada ya habari bado yapo

Halafu kulikuwa na SONGI tunaimba
Tunafatisha tu beat
"Baba yake juma
Alikuja jana na viraka nyuma
Vinaulizaana
Umekuja lini
Nimekuja jana na leo naoondokaaaa"

Sijasikiliza taarifa ya habari radio zaidi ya miaka 5 na sasa dah hakika teknolojia inatuweka mbali na uharisia
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,646
2,000
Kwa sababu sioni pointi/sababu ya msingi ya kutofatiana muda ndani a mipaka ya nchi hiyohiyo.

Timezone ndani ya mipaka ya Tanzania kuanzia visiwani hadi magharibi kabisa kule Manyovu Kigoma ni sawa. Kama Znz ni saa 6 kamili mchana basi Mwanza na Kigoma kote ni 6 kamili mchana. Tofauti unayoisikia wewe inasababishwa na speed ya mawimbi kama walivyosema wadau wengine basi.
 

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,584
2,000
Timezone ndani ya mipaka ya Tanzania kuanzia visiwani hadi magharibi kabisa kule Manyovu Kigoma ni sawa. Kama Znz ni saa 6 kamili mchana basi Mwanza na Kigoma kote ni 6 kamili mchana. Tofauti unayoisikia wewe inasababishwa na speed ya mawimbi kama walivyosema wadau wengine basi.
Hapo kwenye 'mawimbi' mimi nipo Arusha, RFA ipo Mwanza, RTD ipo Dar, kwa hiyo ninachokisikia mimi Arusha ni tofauti na anavyosikia wa Dar na Mwanza?
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,193
2,000
Timezone ndani ya mipaka ya Tanzania kuanzia visiwani hadi magharibi kabisa kule Manyovu Kigoma ni sawa. Kama Znz ni saa 6 kamili mchana basi Mwanza na Kigoma kote ni 6 kamili mchana. Tofauti unayoisikia wewe inasababishwa na speed ya mawimbi kama walivyosema wadau wengine basi.
... radio waves zenye kasi ya kuweza kuizunguka dunia mara saba kwa sekunde yachukue dakika nzima kutoka Mwanza - Arusha? There must be some other reasons but not the radio waves speed!
 

Kategele

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
663
1,000
Siku moja nenda kwenye mabanda umiza kwenye mechi za bongo ndio utapata picha kamili. Yaani goli linaingia wa radio hii analisikia mapema huku wa radio nyingine anachelewa kulisikia.
Halafu wanaudhi wasikiliza redio kwenye TV faulo haijapigwa unasikia Mwenye redio anakwambia hilo goli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom