May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,818
Mimi kila alfajiri huwa nasikiliza RTD, ili kusikiza Usia wa baba, utabiri wa hali ya hewa pamoja na mambo mengine, na baadae nahamia RFA kusikiliza BBC.
Kwa wiki kadhaa sasa nimegundua ya kuwa Vituo hivi, yaani RTD na RFA wanapishana muda...kwani baada tu ya RTD kusema imetimia saa kumi na mbili kamili mimi ndipo nahamisha kituo kwenda RFA, cha ajabu sasa huwa nakutana na Muziki na mara Muziki utashuka na atasikika Mtangazaji akisema imebaki dakika moja itimie saa kumi na mbili kamili.
Sina uhakika kama ilikuwa hivi tangu muda mrefu lakini kwangu nimegundua hii tofauti kama wiki moja na siku hivi sasa..na nipo na ratiba hii kwa miaka.
Na nimelazimika kusikiliza kwa siku kadhaa ili kujiridhisha nisikurupuke na hali imekuwa ni hivyo hivyo, hata leo asubuhi.
Sasa je hii iko sawa au kuna kosa mahali?.