Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2010
Posts
1,007
Reaction score
601
1.jpg

2.jpg


Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.

Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.
 
Haya bhana vizuri,ila kimtindo kama kusafishana.

Mtumishi wa mungu achafuriki wala kuchafuliwa.. unajua LUSEKELO MZEE WA UPAKO anaaishi wapi na anaendesha gari gani?

Hapa naona mimi ni kuwekana sawa tu.
 
Unamkingia mabomu kwa sababu unalipwa au unajenga kashfa fulani ambayo watu watafunguka?
 
Mara nyingi hawa watumishi feki wanaweka pesa zao ndani,wanachimba chini kisha wanatunza madola tu.Nadhani Kakobe atakuwa na dola bilioni 1.Msanii Gwajima atakuwa na dola bilioni 2 kwa maana yeye sadaka zote anatia kwapani,hataki hata kununua eneo ajenge.mama rwakatare atakuwa na bilioni 3,Yule mwenye bank atakuwa na bilioni 5,lusekelo nae yuko nyuma yao na anawakimbiza kwa hasira atakuwa na milioni 7.Waacheni wajinga waliwe,hawajazimishwa.
 
Ni kweli kabisa, hizo tu ndiyo mali zake binafsi Askofu Kakobe. Mimi nimekuwa muumini wa Kanisa la FGBF, kwa miaka 25 sasa, yaani tangu lilipoanzishwa 1989. Muda huu mrefu, umenipa kumfahamu kwa karibu sana, Mchungaji wangu huyu. Ninathibitisha kwamba haya ndiyo maisha halisi ya Askofu Kakobe, tofauti na uzushi mwingi wa mashetani. Mtumishi huyu wa Mungu, analiishi hasa Neno la Mungu analolihubiri; ndiyo maana waumini tunampenda, kumwamini na kumheshimu; na makelele yote ya mashetani, hayawezi kututenganisha naye. Ninapafahamu mpaka kijijini kwake Askofu Mkuu Kakobe, huko Kakonko, Kigoma. Kijijini kwake, nako, hana hata banda. Miaka yote hii, akienda kijijini, amekuwa akifikia kwenye nyumba ndogo ya wazazi wake, Frank Kakobe, na Debora Kakobe, waliofariki muda si mrefu uliopita.
 
Mara nyingi hawa watumishi feki wanaweka pesa zao ndani,wanachimba chini kisha wanatunza madola tu.Nadhani Kakobe atakuwa na dola bilioni 1.Msanii Gwajima atakuwa na dola bilioni 2 kwa maana yeye sadaka zote anatia kwapani,hataki hata kununua eneo ajenge.mama rwakatare atakuwa na bilioni 3,Yule mwenye bank atakuwa na bilioni 5,lusekelo nae yuko nyuma yao na anawakimbiza kwa hasira atakuwa na milioni 7.Waacheni wajinga waliwe,hawajazimishwa.

kwa hiyo watazitumia wakifa?
 
Mtumishi wa mungu achafuriki wala kuchafuliwa.. unajua LUSEKELO MZEE WA UPAKO anaaishi wapi na anaendesha gari gani? Hapa naona mimi ni kuwekana sawa tu.

Vipi kuhusu Mwingira, Gwajima, Lusekelo na Rwakatare, nao wanaishi nyumba za design gani?
 
Mtumishi wa mungu achafuriki wala kuchafuliwa.. unajua LUSEKELO MZEE WA UPAKO anaaishi wapi na anaendesha gari gani?

Hapa naona mimi ni kuwekana sawa tu.

Lusekelo ana nyumba 23 za maana za wapangaji,ana hoteli 2 mbeya na 2 arusha,ana yard ya magari na ameagiza Chopa 1 toka ujerumani.
 
Back
Top Bottom