Hii hali tunaweza kuielezea vipi?

Hii hali tunaweza kuielezea vipi?

ERTUGRUL BEY

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
11,597
Reaction score
21,642
Habari zenu members.

Kuna hali Fulani ambayo ipo,kwamba waeza kutana na mtu lkn bila sababu yoyote ukajikuta unamkubali,mnaenda Sawa na mnajikuta kana kwamba mmefahamiana siku nyingi,mkikutana mnasalimiana vizuri na mnaweza tengeneza connection kirahisi Tu.

Lakini kinyume chake kuna mtu unakutana nae,Bila sababu yoyote ya msingi unajikuta Tu yaani haumkubali hata kidogo,hata kuzoeana tabu,unajiuliza hata hajakufanyia kitu chochote kibaya lakini yani inatokea Tu.

Niliwahi sikia kuwa Kwa nadharia ya kidini kuwa,zile roho ambazo baada ya kuumbwa zliikiwa pamoja au majirani huwa huku duniani zikikutana huwa zinaenda Sawa Kwa maana zilikuwa na back ground moja na zile ambazo haziivi hazikuwahi kuwa pamoja Kwa maani zilikuwa mbali mbali.

Bila Shaka hata wewe msomaji ushawahi msikia mtu anasema,mi Fulani simpendi hata kidogo,ingawa hajawahi kumfanyia chochote kibaya,ebu tupanuane mawazo hapa.

Ni hayo tu.
 
Unaonekana una uchawa. Sasa kuna watu ukijipendekeza mnaelewana ila kuna watu wakigundua wewe ni chawa wanakupotezea. NI HAYO TU.
 
Back
Top Bottom