Hii Digitali kweli ni balaa!

Mliga

Senior Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
101
Reaction score
16
Huku kuzima hii mitambo ya analogia kumeshatumbukiza nzi Startimes, Clouds ni punje tupu na kukoroma tu hadi kwenye king'amuzi chao!
 
kwani hamjui hizi ni siasa!! na hii ni tz!! na hiyo bado,ngoja iende nchi nzima ndo tutakoma!!!!
 
Jameni digital bado 'inasychronize" ipeni muda itakuwa powaa.
 
nimefurahi sana clouds walivyotoweka,
kesho wapige hii story kinafiki kwenye kile kipindi hao cha asubuhi.
 
Mi ndo kabsa napata mpunga tupu!
Heli enu nyie wenye mchele kabsa
 
nimefurahi sana clouds walivyotoweka,
kesho wapige hii story kinafiki kwenye kile kipindi hao cha asubuhi.

Unaonyesha ni jinsi gani wabongo tunavyoombeana matatizo ili tuchekana!!! Dah!! Kazi kweli kweli!!! Sasa kimekufurahisha nini???!!
 
Tulieni mpate digitalii

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
mimi sio m'bongo,
nitake radhi tafathali.

Nisamehe bure saba mara sabini. Labda sentensi ingesomeka hivi: "Unaonyesha ni jinsi gani binaadamu tunavyoombeana matatizo ili tuchekana!!! Dah!! Kazi kweli kweli!!! Sasa kimekufurahisha nini???!!"
 
Clouds TV si wapenda vya bure! Nasikia walikubaliana na startimes wawekwe for free na wao watarusha matangazo yao for free, sasa Startimes si ishajulikana so wamekataa kuwarusha bure na wenyewe wameijtoa, sasa hivi wako zuku wanarushiwa matangazo yao for free tena!

Hii nchi ukiwa mjanja safi sana!
 

Kama ni kweli hayo usemayo, hakuna ubaya wowote. Kibiashara inakubalika. Rejea kanuni ya SET-OFF katika accounting techniques au waulize wahasibu na wakaguzi wa hesabu za fedha watakupa shule.
 
Alaa kumbe Clouds TV ni maarufu na inapendwa kihivyo,nafikiri Kusaga atakuwa naye yumo humu JF atakuwa amesikia kilio chenu
 
Hayo ndio mambo ya digitali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…