Hii boat iliishia wapi?

Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Posts
4,607
Reaction score
3,187
Wadau,

Miaka michache iliyo pita, kuna boat ilinunuliwa na tajiri mmoja kufanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba. Boat hii ilileta gumzo kubwa kwani Magufuli kama waziri wa ujenzi alikataa hiyo boat isisafirishwe kupitia barabara zetu kutoka Dar kwenda Mwanza kwa madai ya kulinda barabara. Hatimae boat hii ilisafirishwa kupitia Mombasa na mwisho ilifika Mwanza na kuanza safari zake kati ya Mwanza na Bukoba.

Nani anayejua hii boat ilipatwa na nini na kwa sasa iko wapi?

Tiba

Ilisitisha safari maana kwenye injini yake iliunguza kifaa kwa kitaalamu kinaitwa ropgifiboreingene
 
Zilikuwa boti 2, ziliruhusiwa kupita kenya na zikafika mwanza kupitia bandari ya kisumu baada ya kuruhusiwa na raila odinga
 
Hiko kifaa kiliungua baada ya kugonga mwamba unaoitwa frooktotostabolization mofatti

Jamani JF kwa vituko hamna mfano, yaani nimecheka mpaka basi. Kwa hiyo hiyo boat iko wapi kwa sasa na inatumikaje?

Tiba
 
Zilikuwa boti 2, ziliruhusiwa kupita kenya na zikafika mwanza kupitia bandari ya kisumu baada ya kuruhusiwa na raila odinga

Ni kweli zilipita Kenya na hatimae kufika Mwanza, sasa ziko wapi na zinatumikaje?

Tiba
 
Ilisitisha safari maana kwenye injini yake iliunguza kifaa kwa kitaalamu kinaitwa ropgifiboreingene

Kwa hiyo hicho kifaa hakijapatikana spare yake mpaka leo au?

Tiba
 
Ilisitisha safari maana kwenye injini yake iliunguza kifaa kwa kitaalamu kinaitwa ropgifiboreingene

Hiko kifaa kiliungua baada ya kugonga mwamba unaoitwa frooktotostabolization mofatti

Mwanamke mwenye mimba changa anaweza kupata complications kama akiyasoma hayo majina mpaka mwisho Tiba hivi vingine hivi tuviache tu kama vilivyo
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka hii ishu ya boti ilileta uhasama sana hadi mijahidina ikawa inatokwa povu et magufuli akuziruhusu zisipite kwenye barabara zetu kwa sababu mwenye boti Muislamu. Naye Magufuli akajitokeza bila kumung'unya mdomo na kusema ni yeye kasema hapana kama vp mniombee albadili
 
Mwanamke mwenye mimba changa anaweza kupata complications kama akiyasoma hayo majina mpaka mwisho Tiba hivi vingine hivi tuviache tu kama vilivyo

Afadhali na wewe umeona hiyo ndugu yangu. Hayo majina ni hatari. But seriously hii boat iliishia wapi?

Tiba
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli ilikuwa ni issue iliyopamba vichwa vya habari za magazeti na hata hapa JF. Sasa mwisho wa hii boat ulikuwaje maana sijaisikia siku nyingi sana.

Tiba
 
Hiko kifaa kiliungua baada ya kugonga mwamba unaoitwa frooktotostabolization mofatti
hiki kifaa nacho kilikuwepo kwenye titanic nazan kwa kitaalam wakat hule kilijulikana kama MAFIZIKOLO-AMPHIBIAN DECLOFENAC
 
Ni kweli ilikuwa ni issue iliyopamba vichwa vya habari za magazeti na hata hapa JF. Sasa mwisho wa hii boat ulikuwaje maana sijaisikia siku nyingi sana.

Tiba
hii nchi tiba achana nayo tu jins ilivyo uhenda labda hata boti zenyewe hazikuwepo
 
Afadhali na wewe umeona hiyo ndugu yangu. Hayo majina ni hatari. But seriously hii boat iliishia wapi?

Tiba

Honestly speaking Tiba sijui
 
Last edited by a moderator:
Zipo mwanza sielewi fukwe gani lakini nikiwa naenda ukerewe naziona zimepaki,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…