High Court directs CCM, govt to argue on petition | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

High Court directs CCM, govt to argue on petition

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngolinda, Aug 29, 2010.

 1. Ngolinda

  Ngolinda Senior Member

  #1
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  High Court directs CCM, govt to argue on petition

  Friday, 27 August 2010

  The High Court yesterday directed the government and the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) to argue by way of written submission the reasons why they want the court to dismiss a petition seeking to bar President Jakaya Kikwete from contesting October General Election.

  The order was given by Justice Augustine Shangwa after a dramatic exchange between the petitioner and the judge who spent most of time to inquiry the exact motive behind the petition.

  Mr Mhozy, 59, a former tutor at the Dar es Salaam Teacher's College filed a petition last month, asking the High Court to order the National Electoral Commission (NEC) to remove President Kikwete's name from the list of contesters for Presidency for, among other reasons, violating constitutional rights of Tanzanians and abuse of office.


  Mr Mhozya is accusing President Kikwete, who is widely tipped to win the October General Election, of being "intolerably extravagant with Treasury coffers during his tenure of office".


  "He use them (Treasury coffers) for show of power, flamboyance, unlimited personal voyaging and personal enjoyment," he alleged.


  But the Attorney General and Trustees of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) who are respondents in the petition have asked the court to dismiss the petition for not worth serious consideration and for provoking unnecessary anxiety.


  "The president of the united Republic of Tanzania, Honorable Jakaya Mrisho Kikwete has prudently and properly been executing duties conferred on him by the constitution of the United Republic of Tanzania," argues the AG in a reply to the petition.


  The AG has also asked the court to throw out the petition for not being justiciable but only seeking to want to disrupt the election process.


  Yesterday Justice Shangwa ordered the respondents to file their written submissions by September 6 and a reply by Mr Mhozya on 13th September before the case come for mention on 21 September.


  Source: The citizen
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  .... Mambo ndiyo hayo!!!
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Drama!
  By the time the petition is entertained, general elections are over and the Prez is in office..then guess what?.........the case will be redundant!
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ukidharau mwiba, mguu huota tende
   
 5. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Perhaps the case will be redundant, lakini kumbuka ndio mwanzo wa hali ngumu ya kisiasa ya CCM kwa mgombea wa 2015!
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tatizo pingamizi kama hili na lile la Chadema likiwekwa na kama hukumu haijatolewa mpaka October 31 jina la Kikwete linatolewa katika list ya wagombea kwasababu lina pingamizi. Hivyo CCM ni bora wakajibu mapema ili jibu lipatikane au wavunje sheria walazimishe jina la kiongozi wao liwemo katika list ya wapigiwa kura mwaka huu kweli Watanzania wamechoka!!!!
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Aug 29, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Katiba siku hizi inaruhusu Rais kushtakiwa au anashtakiwa kwa jina lake?
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hili ni pingamizi which means kama mgombea ana pingamizi haruhusiwi kushiriki uchaguzi unless sheria zimebadilika sasa CCM inabidi ijibu kwa maandishi ili mgombea wake aruhusiwe (ambaye ni Jakaya Kikwete). Hili halihusiani na urais kwani urais ni serikali inayoongozwa na mtu yeyote aliyechaguliwa na wananchi.
   
 9. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Mhozya apeleka pingamizi kortini dhidi ya Kikwete

  08/04/2010
  Imeandikwa na Makumba Mwemezi na kuchapichwa katika gazeti Majira kuwa; Raisi Jakaya Kikwete amewekewa pingamizi kortini kugombea urais mwaka huu kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa fedha za umma katika safari zake za nje.

  Hayo yameelezwa na Mwalimu Mstaafu na Mkazi wa Dar es Salaam, Bw. Paul Mhozya ambaye amefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kupinga mgombea huyo katika uchaguzi wa Oktoba 31, mwaka huu.

  Akizungumza na Majira jana, Bw. Mhozya alisema amefungua pingamizi hilo chini ya hati ya dharura akiitaka mahakama kulisikiliza mapema kabla kampeni kuanza, hivyo akaishauri CCM kuteua mgombea mbadala mapema, badala ya kusubiri uamuzi wa mahakama.

  Katika hati ya mashtaka yenye sababu kumi za kuiomba mahakama imuengue Rais Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha urais Bw. Mhozya anasema, rais ametumia nafasi aliyopewa kwa mambo binafsi, amekiuka katiba na kuvunja haki za binaadamu pamoja na matumizi holele ya fedha za watanzania kwa mambo yake mwenyewe.

  Gazeti la The Citizen toleo la jana lilimkariri Bw. Mhozya kuwa aliwahi kufungua kesi ya kikatiba kama hiyo mwaka 1993 dhidi ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuwa alivunja katiba kwa kuruhusu Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC), lakini ikatupwa na Jaji Barnabas Samatta kuwa mamlaka ya kumwondoa rais madarakani yalikuwa mikononi mwa bunge peke yake, chini ya kifungu cha 46A cha katiba.

  Bw. Mhozya alisema amefikia uamuzi wa kufungua kesi hiyo kutokana na ujeuri uliooneshwa na Rais Kikwete katika miaka mitano ya uongozi wake, hivyo ni vema akazuiwa kuurudia kwa kumzuia asirudi madarakani.

  Alisema anayo orodha ndefu ya mambo mabaya aliyofanya Rais Kikwete wakati wa uongozi wake, ambayo anatarajia kuyatumia kama ushahidi na uthibitisho wa malalamiko aliyopeleka mahakamani, ambayo anaamini yatakubaliwa na kumwondoa kwenye kinyang'anyiro.

  "Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame alikwishasema kuwa tume iko tayari kupokea pingamizi dhidi ya mgombea yoyote kwa maslahi ya umma na kuwa itachukua hatua stahili, ninasubiri kauli ya mahakama na ninaamini itasikiliza hoja zangu na kuzifanyia kazi," alisema.

  Alisema kuwa yeye kama Mtanzania anayo mamlaka chini ya ibara ya 30 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufungua kesi dhidi ya uvunjaji wa ibara yoyote ndani ya katiba hasa zinazohusu haki za binaadamu.

  Ibara ya 30 (3) inasema "Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu"

  Bw. Mhozya anasema pamoja na kuwa Rais ana kinga kisheria lakini Kikwete hana kinga ya kuwekewa pingamizi kama mgombea kwa sasa, ndio maana akaamua kufungua kesi hii wakati huu badala ya kusubiri atakaposhinda na kuwa rais, kwani atakuwa na uwezo wa kutumia kinga yake.

  Alisema katika kipindi cha uongozi wake rais amefanya safari za ughaibuni zisizo za lazima nyingi kwa fedha za umma, jambo ambalo limesababisha wananch wengi kuishi maisha ya taabu na umaskini mkubwa, huku akidai kuwa urais ni suala binafsi, akisema kuwa ndio maana alimteua mwanawe kumtafutia wadhamini.

  Alisema sheria inaitaka NEC kutoa muda wa ziada kwa chama ambacho mgombea wake amekufa au ameshindwa kuendelea kukiwakilisha, ili chama hicho kiweze kuteua mgombea mwingine, hivyo anaamini kuwa baada ya pingamizi hilo kukubaliwa mahakamani, NEC itawaamuru CCM kufanya hivyo kwa kuwaongezea muda.

  "Sasa kwa vile sheria inasema NEC itawaongezea muda wa kuteua mgombea mwingine, mimi nashauri wakateua kabisa mgombea mwingine na kumshauri niliyemwekea pingamizi kujitoa, hii itaepusha kupoteza muda pindi pingamizi likikubaliwa, hakuna jinsi," alisema Bw. Mhozya.

  Alisema yeye anahofia zaidi mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo kuliko anavyohofia maisha yake, hivyo pamoja na vitisho anavyopata bado hataogopa kusimamia ukweli na kuwafichua waovu kama anavyofanya.

  "Nimetoka mahakamani leo (jana), nilikwenda kuwaona makarani wa wanipatie 'samansi'(hati ya kuhudhuria mahakamani iliyo na tarehe ya kusikilizwa kesi) lakini walisema bado haijatoka naamini itatoka hivi karibuni ili tukasikilizwe. Matatizo yapo na nilikwisha yazoea," alisema Bw. Mhozya.

   
 10. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kumbe bado naweza kuwania kiti hiki, looooo ungu nisaidie
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :glasses-nerdy:
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  They are wasting their time.
   
Loading...