- Thread starter
- #21
JINSI INAVYOFANYA KAZIHii ina nini cha ziada tofauti na ile ya kawaida inachoipa uwezo wa kuzuia uharibifu wa mazao?
Mifuko hii hairuhusu hewa kuingia Wala kutoka. Ukifungia mazao katika mifuko hii, mazao hutumia hewa yote ya oxygen iliyopo mifuko na kubakisha Carbondioxide.
Wadudu wanahitaji Oxygen ili waishi. Wakikosa Oxygen hugs ndani ya siku Saba.
ONYO: Usihifadhi mbegu humu, inaweza kufa.
JINSI YA KUTUMIA
Hakikisha mazao yamekauka vema. Safisha mazao yako kwa kuhakikisha Vumbi Na uchafu mwingine vimetolewa.
Weka mazao katika mfuko. Funga mfuko wa kwanza kwa kamba, funga wa pili, funga wa tatu.
Weka mifuko sehemu salama ili isitobolewe Na misumari ama vijiti. Tumia njia zingine kudhibiti wadudu kama panya.
ONYO: Usishone mfuko
MUDA WA MATUMIZI
Mfuko huu Bado uko salama mpaka tu pale utakapokua umetoboka.
Waweza kutumia zaidi ya misimu mitatu.
MAELEZO ZAIDI
FARMRICH Agro-Enterprises Limited
farmrichagro@gmail.com
www.farmrich.wordpress.com
0755325442