Heshimu sana jinsia ya kike.

Bra-joe

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,562
986
Tangu tuzaliwe mpaka tumekuwa watu wazima ni 95% nguvu za malezi ya jinsia za kike. Tukianzi nyumbani mtoto siku zote hulelewa na jinsia hii, mama, dada au house girl, tukianza chekechea au day care walimu wengi jinsia ya kike, shule za msingi walimu wengi ni wanawake, hata wakati tunazaliwa wanawake ndio hutoa msaada kwa mama zetu kule ktk chumba cha kujifungulia, hata sasa ni watu wazima wanawake ndio tunawategemea kutusaidia kupata watoto na kulea familia. Hata leo hii bahati mbaya ukilazwa hospitalini nesi wa kike lazima atakuwepo pembeni yako kukusaidia. Hivyo tusipende kuiita jinsia ya kike kwa majina ya kihuni, hawa ni mama zetu, dada zetu, mashangazi, mama wa dogo n.k. Je, utajisikiaje ukimsikia mtu anamwita mama yako au dada yako jina la kihuni?
 
Weka mfano mkuu...

Majina ya kihuni kama yapi sasa..!

Gambachovu hatukujui, lkn swali lako linaonyesha umetoka ktk familia yenye maadili duni. Yani unataka nitaje majina ya kishenzi kwa mama zetu? Labda mwenzetu umezaliwa na nyoka. Mimi siwezi hata kuyataja majina hayo ya kihuni wanayoitwa mama na dada zetu.
 
Inaonekana una heshima na huruma saaaaana kwa jinsia ya kike... Je,wewe ni mwanamke?
Swali dogo la nyongeza Bra Joe..... Je, huoni kama umeitukana familia yangu kwa kuiita yenye maadili duni,na tena ya majoka ambayo ndiyo wazazi wangu? Akiwemo mwanamke aliyenizaa..
 
mimi ni mwanaume. Niliuliza "labda umezaliwa na nyoka" kwasababu ulitaka niwaite mama na dada zetu majina ya kihuni, kana kwamba wewe hujazaliwa na mwanamke. Kuhusu maadili ni kweli inaonyesha huna, inawezekana vipi mtoto kaja kushtaki kwako kama ametukanwa halafu unamwambia aseme waziwazi tusi alilotukanwa? Kama hatukuelewana (nimekukwaza) naomba unisamehe.
 
Ndo maana mnakosa maadili na kuwatukana baba zenu! Wanaume wengine bana, ndo maana mnazidiwa akili na wadada mpaka wanawadunda! Mkome kujipendekeza. Weka heshima kwa wazazi wako wote ili upate miaka mingi na kheri duniani.
 
mimi ni mwanaume. Niliuliza "labda umezaliwa na nyoka" kwasababu ulitaka niwaite mama na dada zetu majina ya kihuni, kana kwamba wewe hujazaliwa na mwanamke. Kuhusu maadili ni kweli inaonyesha huna, inawezekana vipi mtoto kaja kushtaki kwako kama ametukanwa halafu unamwambia aseme waziwazi tusi alilotukanwa? Kama hatukuelewana (nimekukwaza) naomba unisamehe.

Mi sikuelewi hata kidogo... Ila naamini lengo la uzi wako ni jema kabisa.. Ila una udhaifu katika namna ya kujieleza, na kuwasilisha kwa hadhira yako yale uliyonayo moyoni..

Siku njema.
 
Back
Top Bottom