Baada ya Freeman Mbowe kuachiwa Huru kutoka kwenye kesi ya uongo ya Ugaidi , aliyobambikiziwa kwa sababu ya harakati zake za kudai KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI , Na sasa tena baada ya kinachoitwa KIKOSI KAZI CHA SERIKALI kinachodaiwa kutumwa kukusanya maoni ya wananchi KUTOA MAPENDEKEZO YAKE HADHARANI ( Huku Tume ya Warioba ikiwa imekusanya maoni ya wananchi huko nyuma , tena kwa uwazi ) , wadau wa duru za kisiasa wanaona kama CHADEMA NDIO CHAMA MAKINI NA CHENYE KUSTAHILI KUHESHIMIWA NA KUAMINIWA .
Hii ni kwa sababu hakuna Mtanzania yeyote anayepingana na hoja zao , hakuna mtanzania asiyekubaliana na Matakwa ya Chadema kuhusu KATIBA MPYA wala TUME HURU YA UCHAGUZI , Hata Rais Samia Suluhu kwa sasa anakubali kwamba upo umuhimu wa kuwapo kwa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi , kinachosumbua ni kile Kigugumizi kinachoitwa NITOKE VIPI , na hii inasababishwa na WAHAFIDHINA walio Serikalini , walio ccm na kwenye idara nyingine za serikali wanaohofia UGALI WAO .
Dunia yote sasa imethibitisha UMAKINI WA HOJA YA CHADEMA ya kuwapatia wananchi wa Tanzania KATIBA MPYA pamoja na TUME HURU YA UCHAGUZI , tena si kuwapatia bure hivihivi tu , CHADEMA imetoka DAMU , JASHO LA MWILI NA MENO , na Maumivu mengine yasiyoandikika humu JF , Dunia imejua kwamba Chadema tangu awali ndio Tegemeo na nguzo ya Haki , ndio chama cha Kizalendo kinachostahili kuheshimiwa na Kuaminiwa .
Shukrani ziende kwa wote waliounga mkono jambo hili , Wakiwemo akina Askofu Mwamakula , Sheikh Issa Ponda , Askofu Bagonza na wengine wote ambao wametukanwa kila aina ya matusi yakiwemo na yale ya Nguoni , huku wengine wakikamatwa na kudhalilishwa kwa msimamo wao huu wa Kizalendo .
Hatimaye Haki Imeshinda .