Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,343
- 217,381
Baada ya Freeman Mbowe kuachiwa Huru kutoka kwenye kesi ya uongo ya Ugaidi , aliyobambikiziwa kwa sababu ya harakati zake za kudai KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI , Na sasa tena baada ya kinachoitwa KIKOSI KAZI CHA SERIKALI kinachodaiwa kutumwa kukusanya maoni ya wananchi KUTOA MAPENDEKEZO YAKE HADHARANI ( Huku Tume ya Warioba ikiwa imekusanya maoni ya wananchi huko nyuma , tena kwa uwazi ) , wadau wa duru za kisiasa wanaona kama CHADEMA NDIO CHAMA MAKINI NA CHENYE KUSTAHILI KUHESHIMIWA NA KUAMINIWA.
Hii ni kwa sababu hakuna Mtanzania yeyote anayepingana na hoja zao , hakuna mtanzania asiyekubaliana na Matakwa ya Chadema kuhusu KATIBA MPYA wala TUME HURU YA UCHAGUZI , Hata Rais Samia Suluhu kwa sasa anakubali kwamba upo umuhimu wa kuwapo kwa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi , kinachosumbua ni kile Kigugumizi kinachoitwa NITOKE VIPI , na hii inasababishwa na WAHAFIDHINA walio Serikalini , walio ccm na kwenye idara nyingine za serikali wanaohofia UGALI WAO.
Dunia yote sasa imethibitisha UMAKINI WA HOJA YA CHADEMA ya kuwapatia wananchi wa Tanzania KATIBA MPYA pamoja na TUME HURU YA UCHAGUZI , tena si kuwapatia bure hivihivi tu , CHADEMA imetoka DAMU , JASHO LA MWILI NA MENO , na Maumivu mengine yasiyoandikika humu JF, Dunia imejua kwamba Chadema tangu awali ndio Tegemeo na nguzo ya Haki , ndio chama cha Kizalendo kinachostahili kuheshimiwa na Kuaminiwa .
Shukrani ziende kwa wote waliounga mkono jambo hili , Wakiwemo akina Askofu Mwamakula , Sheikh Issa Ponda , Askofu Bagonza na wengine wote ambao wametukanwa kila aina ya matusi yakiwemo na yale ya Nguoni , huku wengine wakikamatwa na kudhalilishwa kwa msimamo wao huu wa Kizalendo .
Hatimaye Haki Imeshinda .