Heshima kwa Faragha: Usishiriki Bila Ruhusa

Heshima kwa Faragha: Usishiriki Bila Ruhusa

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
895
Reaction score
777
Dhana ya kuheshimu faragha za watu ni ngumu kuielewa kwa wengi wetu. Mtu anaweza ‘kuposti’ jambo WhatsApp na likawa kwa wote anaowajua yeye ukiwemo wewe lakini si kwa wote unaowajua wewe. Kwamba umeona ‘ameposti’ WhatsApp haimaanishi amekuruhusu kuwaonesha na wengine bila ruhusa yake.

Mtu akikupigia simu wewe, akijua mnazungumza wewe na yeye, haimaanishi unaweza kumuweka ‘loudspeaker’ na mtu mwingine asikie bila ruhusa yake. Unaandikiwa ujumbe wewe na sio kwa wote unaowaamini wewe. Kuna maneno anayesema kwa sababu anajua unayeyasikia ni wewe na huenda asingeyasema angejua kuna mtu mwingine anasikiliza. Kuna maneno anayaandika kwa sababu anajua unayeyasoma ni wewe na huenda asingeyaandika angejua kuna mtu mwingine anayasoma.

Ukiambiwa jambo binafsi na mtu, maana yake umeaminiwa wewe na sio wote unaowaamini wewe. Huwezi kumshirikisha na mwingine unayemwamini wewe bila ridhaa yake. Unapowaamini wengine kwa mambo uliyoaminiwa wewe bila ridhaa yake maana yake wewe huaminiki na ulichokifanya ni usaliti.

Kuna watu wanaishi maisha ya faragha kiasi kwamba kuna taarifa akiisikia mahali anaweza kujua ni nani ameitoa. Unaona kwenye ‘status’ ya WhatsApp kumbe amekuwekea wewe peke yako. Unapigiwa simu kumbe mazungumzo hayo hayajafanywa na mwingine yeyote. Unasimuliwa jambo wewe peke yako bila kujua na likisikika kwingine mtu anaweza kufuatilia kujua nani hasa aliyesambaza habari hizo. Utadharaulika.
 
Back
Top Bottom