Heshima kwa Brothers mliooa na mnaishi kwa upendo, amani na furaha katika ndoa zenu

Guevara Jr

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
300
811
Wasalaam Wakuu,

Basi tu nimeamka nawafikiria bros mliooa na mpo kwenye ndoa muda mrefu na ndoa zenu bado zina furaha na amani, heshima kwenu.

Bros mlio kwenye ndoa hata kama zina wiki tatu ila bado mpo na furaha, amani, kuheshimiana, kusikilizana na kupendana, heshima kwenu.

Bros ambao mpo kwenye ndoa zaidi ya miaka 10 na bado mnapendwa sana na wake zenu, wanawaheshimu, na kujua vyema nafasi zao kwenu, sio tu mna wake bora, nyie mna zawadi ya maisha. Heshima kwenu wazee.

Bros mliopitia changamoto nyingi za ndoa na bado mkazishinda na leo hii mkirudi home vitoto vyenu vinafurahia uwepo wenu huku mkipokelewa na tabasamu la wake zenu na mna kula kwanza kabla ya kula...Kongole sana wazee wangu.

Bros mlio kwenye ndoa zaidi ya miaka mitano na leo hii mkipiga simu kwa wake zenu, wawe peke yao au kwenye kundi la watu, wanapokea na kusema hello Mume wangu au Baba flani. Na sio kusema halooo habari ya saa hizi, hata kama hamjaongea toka asubuhi....Heshima kubwa kwenu wazee.

Bros ambao mpo kwenye ndoa na siri zenu za ndani zimebaki vifuani mwa wake zenu kwa zaidi ya miaka 5 bila kwenda kwa mashost, mashemeji, ukweni au hata kuharibu watoto....Pongezi kwenu wazee

Bros ambao mpo kwenye ndoa muda mrefu na bado mipango na mikakati yenu ya kimaendeleo ipo vizuri kwa ushirikiano mzuri na wake zenu....Heshima kwenu Bros.

Nisiwasahau bros ambao mpo kwenye ndoa na wake komodo dragons na bado mnasimama kulinda ndoa zenu na huku mitaani ni watu wenye heshima na kukubalika kwa jamii....You guys are heroes, heshima kubwa kwenu.

NB; nawazungumzia bros waliooa kwa maana ya NDOA. Ndoa ni tunu aheshimiwe ailindae, kuitetea na kuipigania.
 
Tunashukulu mkuu, ila kumbuka dhahabu haiwez kung'ara paspo kuptishwa kweny moto, changamoto zpo kwenye maisha na ili kuwa mkamilifu na imara lazma hayo uyapitie then ndio baraka zikufuate, Chamsingi nikuwa na moyo wa uvumilivu, mwisho wa siku hayo yote hubak kuwa story, na furaha hutawara
 
Back
Top Bottom