Heshima kitu cha bure ,wajibu kuwazindua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heshima kitu cha bure ,wajibu kuwazindua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mohammed Shossi, Jan 28, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nianze yangu kalamu Kuandika muhusia
  Tena na iwe muhimu Wasomaji zingatia
  Haya ninawakirimu Pengine yatawafaa
  HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA

  Werevu chunga heshima Matusi katu kutoa
  Usijione wasema Hayo ni majaalia
  Wangapi wanalalama Tabia kuichukia
  HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA

  Nidhamu ndio heshima Kuyasema ya murua
  Majaala ya Karima Huumba na kuumbua
  Fikiri na kujipima Wapi unakotokea
  HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA

  Uungwana ni heshima Mungu analiridhia
  Kisiingie kiyama Bila ya kujikagua
  Ulimi uyaseme mema Sio kujiropokea
  HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA

  Kulinda yako heshima Si jambo la kununua
  Bure silaumu mama Mzazi alokuzaa
  Hafundishi ya zahama Mabaya kukutakia
  HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA

  Heshima inaposimama Mja mwema unakua
  Heshima inapoparama Utu thamani potea
  Heshima nayo tizama Hifadhi kishikilia
  HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA

  Yangu ninayoyasema Mwisho nimefikilia
  Sikieni waadhama Nikoseapo kosoa
  Tusitafute hasama Mchawi tukimjua
  HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA
   
 2. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Duh na wewe pia umo????? Imekaa vizuri sana
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nimo lakini sio kihiiivyo...
   
 4. Blue_Face

  Blue_Face Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  shossi, io shairi safi kabisa, ahsante kwa kutizindua. ni wajibu kukumbushana.
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Heshima hakuna siku hizi hapa JF mwenye kusikia na asikie..............
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huvumi lakini umo
   
 7. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hehehehehhee.... heshma imepigwa ban siku hizi umesahau wewe??? hehehehe lol....
   
 8. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  watu mna maneno jamani hee...
   
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Na vigumu kujua kama nimo labda kwa watu wangu wa karibu ka wewe hahahahaha
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Assalam alaikum bibie
  Hali yako nijulie
  Si vibaya ujue...
  Wanasema salamu haitii mimba na ingekuwa inatia mimba waalimu wangekufa kwa uzazi.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wanadau wanasema heshima hainunuliwi siku hizi heshima inanunuliwa kwa pesa
   
 12. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Alaaa sina khabari..........
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kazi basi ndio maana siku hizi wanasema mtoto uliemzaa wa mwezio......................
   
 14. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mh mohamed abuy hebu taratibu si umesema we huvumii mbona wataka vuma tena?? haya ok waaleyku salam warahmatllah...
   
 15. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hujanijulia hali yako lakini............?
   
 16. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bukheyr wa sihha alhamdulillah na yako yasemaje??
   
 17. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #17
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Yangu bukheir kadhalika Shukran salam zimefika
   
Loading...