baada ya miezi 6 tu bajaj hio haifai ni ya kutupa.....biashara ya bajaj,taxi,daladala ni sawa sawa na kuweka hela yako 5M,12M,30M RESPECTIVELY na kutumia kidogokidogo hadi inaisha....
Ningeomba tuwe wakweli na tusiwe wanafiki
Wanaofanya bishara hiyo ni watu na wao wanamitizamo yao,na kama ingekuwa hailipi basi wangeacha.na sio kila unachokipenda wewe ndio mtu afanye.Na ndio maana mtu akinunua moja baada ya muda anaongeza nyingine.
We unasema Daladala,wakati ndugu zako wenyewe wanapanda.
tataizo mtu anataka akitoa pesa basi kesho imlipe,we umeona wapi.Na wengie matumizi ni makubwa,unepewa 15,000 kesho huna kitu ikifka siku ya Service mweupee,na ikipata tatizo kubwa ndio kabisaa.Mwisho unamuona Dereva mbaya.
Wapo wanaowekeza mpaka milioni 100 kwa malengo marefu ya kumlipa baada ya miaka mitano hadi sita.Mwisho wa siku
ikijilipa anakula bata.Kisha sie tunaona kama wamebahatisha kumbe ni malengo ya muda mrefu.
We angalia DCM au Gobole zile za Dar unafikira wao wameneunua lini kwa jinsi baadhi yake zilivyo,unakuta miaka hadi kumi imo njiani,imezalisha kama nane kamahizo.
Ninavyofaham, mie Bajaji kwa Dar ni Tsh:15,000 kwa siku kwa sasa.Usimbane sana Dereva biashara imekuwa ngum sana.
Ndani ya mwaka inakulipa kisha unaendelea kula bata.
Muhim kwenye vyombo vya moto ni Services tu,nakutokupuuzia tatizo hata kama ni dogo.
Na ndio maana unaweza kukuta Gari bovu sana kwenye bodi ila Engine yake bado nzima sana.Hii ni kwamba inapata Services ya maana na inahudumiwa.