Herufi ya mwanzo ya jina lako inabeba tabia yako

Siku zote na mara nyingi nimekuwa nikijiuliza bila kupata majibu sahihi,kati ya jina na tabia ni kipi kinaanza especialy kwa binadamu,Mfano mtu anaitwa Mateso,Chawote,Matata,Matatizo,Hurruma,chakupewa, nk na mengine mengi ya kienyeji ambayo ukipewa tafsiri yake utacheka Mfano Komba,Sendhia,nk Ukichunguza kwa undani maisha ya hawa watu utakuta tabia walizonazo zinaendana na majina yao,Je ni kutokana na Tabia ndio jina linatungwa kutokana na Jina ndio tabia inafuata?

Kwa Upande wangu nimefananisha mahusiano ya Tabia na Jina kama "KUKU NA YAI"Ni nani kaanza au nani mkubwa,Mfano wa Mahali,Machinjioni(makutano ya Mandela eoad na Chang'ombe rd),Tuamoyo,Bagamoyo,Sinza kwa wajanja/Kijiweni,nk Ukichunguza kwa undani tabia na maisha ya wakazi wa Eneo hilo yanaendana na jina la mahali husika.

NIJUZENI ZAIDI Wanajamii,Ili kuwe na Umakini ktk kuwapa Watoto wetu majina au mahali pa biashara, JINA KWANZA.
 
Sisi tunaotumia simu za mchina kuna kitu tunakimis hapa! naomba mnisaidie, mimi majina yangu yanaanza na herufi hizi R M, inakuwaje hapo kuhusu tabia?
 
HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.
HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.
HERUFI G mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi
 
Mimi kiukweli jina langu linaanza na herufi A
My ''To Be'' naye kaanzia na herufi A, hayo uliyoandika hapo juu ni kweli kabisa kwake kwa 100%! Nami jina langu limeanzia na S, yote uliyoandika yananihusu sana. NIMEIPENDA SANA HII....
 
sasa Y na V ziko wapi?
Mimi jina langu linaanzia na V ebu niangalizie huko
 
Uliposema herufi M ni mropokaji yaani ni kweli kabisa.
Mfano hai tukianzia hapa hapa Jf akina Msalani na wengineo.
 
Si kweli,nimesoma maelezo ya herufi nyingi hapo si kweli labda umetafiti ktk ukoo wenu but IT IS WRONG,VERY WRONG hata erufi ya jina langu umechemka vibaya sijui umetoa wapi idea hizi
 
ungekua ata na riference ungenishawishi au mfano wa mtu kama E lowasa apo kwenye herufi E mkuu haendan kabisa na hayo maelezo ni wazi kwamba umekurupuka usingizin ukakosa kitu cha kukuweka bize ukatunga hii kitu ukaona ni vyema kupotosha watu
 
Back
Top Bottom