Herufi ya kwanza ya jina lako imebeba tabia yako

Herufi ya kwanza ya jina lako imebeba tabia yako

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
10,569
Reaction score
21,075
Kama ulikua hujui kuwa TABIA YAKO inaendana na HERUFI YA KWANZA YA JINA LAKO wacha nikufahamishe;-
Unaweza ukabisha lakini huo ndio ukweli,

Nimefanya utafiti wa kutosha na kugundua haya yafuatayo, Utafiti huu nimeufanya kwa muda mrefu kwahiyo ninacho kisema hapa ninauhakika nacho,

Je unataka kujua tabia yako ikoje au ya rafiki yako ikoje, Naomba usome hapo chini kwa umakini halafu uniambie ukweli hiyo tabia unayo au huna,
Na je rafiki yako hiyo tabia anayo au hana.

HERUFI "A"

Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa,
Anajiamini na mwenye uwezo wa
kutimiza malengo yake,
Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio,
Anapenda kuheshimiwa,
anapenda mamlaka,
Lakini mtu huyo huwa ana kiburi na hasira za karibu.

HERUFI "B"

Mwenye jina linaloanziana na herufi B,
Ni mtu mkarimu,muaminifu na hupenda kazi,
Ni jasiri, shujaa na mkatili katika
vita au pale anapotaka kulinda vilivyo
katika himaya yake.

HERUFI "C"

Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika,
Pia ni mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda,
Ni watu wa wabunifu na
wanaopenda mawasiliano.

HERUFI "D"

Mwenye jina linaloanziana na herufi D,
Ni mtu anayependa usawa na biashara,
Ni watu wanaopenda pia kuamrisha na mwenye kupenda usafi,
Lakini pia ni jeuri na wenye msimamo usioyumba.

HERUFI "E"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi E,
Ni mtu mwenye roho nzuri yenye mapenzi na huruma,
Pia wenye kupenda uhuru
katika mapenzi na mchangamfu,
Lakini mara nyingi ni mtu
asiotegemewa na ni kigeugeu.

HERUFI "F"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi F,
Ni mtu mwenye mapenzi ya kweli, huruma l, roho nzuri,
Pia mtu huyu ana uwezo wa kuwafariji watu,
Yani huyu ni mzuri sana kwenye kuuguza wagonjwa,
Kwasababu anauwezo mkubwa wa kumfariji,
Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni,
Tatizo lake ni moja tu ni mzito wa kufanya maamuzi.

HERUFI "G"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi G,
Ni mtu mwenye imani ya kidini na
nguvu za kiroho,
Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu,
Ni mtu mwenye hisia kali,msomi na hupenda kujitenga,
Tatizo lake ni mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu,
Kiufupi mtu huyu hashauliki unaweza ukamsgauri kitu,
Akitoka tu hapo ushauri wako wote kauacha hapohapo.

HERUFI "H"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi H,
Ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara,
Hupata faida kubwa kutokana
na jitihada na bidii zake,
Tatizo lake ni mtu mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.

HERUFI "I"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi I,
Ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu,
Tatizo lake wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.

HERUFI "J"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi J,
Ni mtu mwenye matamanio, mkweli, mkarimu na muerevu,
Pia ni mtu asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa,
Tatizo lake wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.

HERUFI "K"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi K,
Ni mtu mwenye jeuri, mwenye msimamo thabiti,mashuhuri,
Na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu,
Pia mtu huyu huwa na uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana,
Tatizo lake ni mtu asieridhika na hali fulani ya kimaisha.

HERUFI "L"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi L,
Ni mtu wa vitendo, pia ni mtu mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha,
Lakini huwa wanapata ajali mara kwa mara.

HERUFI "M"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi M,
Ni mtu mwenye kujiamini sana,
mchapakazi na hupata mafanikio,
Tatizo lake mtu huyu kuwa ni mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika,
Yani huyu ukimpa siri yako imeisha hawezi kabisa kukaa na kitu moyoni mwake.

HERUFI "N"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi N,
Ni mtu mwenye ubunifu, pia mtu huyu ana hisia kali na hupenda kuwasiliana,
Tatizo lake huyu mtu huwa ana wivu sana.

HERUFI "O"

Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni
mtu mwenye subra, mvumilivu na
mwenye bidii ya kusoma.
Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia zake.

HERUFI "P"

Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na
hekima kubwa.
Ana nguvu za kiroho
lakini anapenda sana kujitumbukiza
kwenye mambo ya watu yasio muhusu,
Kiufupi huyu jamaa mara nyingi huwa ni kiherehere,
Na mara nyingi kutokana na tabia yake ya kiherehere basi mtu huyu Huwa anasutwa.

HERUFI "Q"

Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni
mtu mwenye kupenda mambo ya asili.
Ni watu wasiyoelezeka na wana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulika,
Lakini pia ni mtu mpole na aliyepooza sana.

HERUFI "R"

Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni
mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma
lakini ana hasira za haraka.
Muda wote anakuwa mpenda amani.

HERUFI "S"

Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni
mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta
utajiri.
Ni watu wenye maamuzi ya
ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

HERUFI "T"

Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa
kiroho,
Anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu.
Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.

HERUFI "U"

Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla.
Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.

HERUFI "V"

Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni
mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie
choka.
Hata hivyo ni watu wasiotabirika.

HERUFI "W"

Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi,
Pia mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya.
Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.

HERUFI "X"

Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika mambo yake,
Pia ni mtu WA kupenda anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.

HERUFI "Y"

Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na
hawapendi kupingwa jambo lao lolote.
Ni watu wanaokosa uamuzi na
husababishia kupoteza bahati katika
maisha.

HERUFI "Z"

Mtu mwenye jina linaloanzia na herufi Z,
Ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani,
Wanashaurika na kufikiria kabla ya kuamua jambo,
Tatizo lao hawa jamaa huchagua watu wa kiwasikiliza,
Kuna wengine hata wamshauri vipi hawasikilizi.
 
1744238603537.png
 
Hadi kwenye jina la mdogo wangu umenidanganya pia naomba mfano wa jina lililo anza na herufi x hapa bongo ukiachana na akina xabi alonso,xavi hernandez
 
Kuna herufi yangu ipo pale mwisho inasema ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo😀😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom