Napenda kutoa salamu za kheri ya mwaka mpya kwa wale wote tuliokuwa nao ktkkubadilisha mawazo na uzoefu wa masaula ya mapenzi.
Lakini mambo haya yamenikwaza sana, hasa suala zima la ubaguzi na ulimbukeni.
Nikianza na ubaguzi, ni kwamba,kuna baadhi ya wanajf huamua kuweka uzi harafu wanaweka tags, kwamba inawahusu fulani na fulani, hii ina maana kwamba ikiwa id yako haipo kwenye tags basi ujue kuwa uzi huo haukuhusu, hii sio nzuri hata kidogo ma ni dalili ya kuwadharau wengine.
2.Uchanganyaji wa lugha- kuna watu hutumia kiswahili nj kiingereza kwenye mada zao, hii inawafanya wale wasio na uwezo wa kuelewa hyo lugha kushindwa kuelewa nini kinajadiliwa, hii ni kero.
Unakuta mtu anaanzisha uzi harafu watu wanachangia kwa kiingereza! kama mtu anataka kuonesha kuwa yeye hajasoma santa kayumba, afungue uzi wa kiingereza na wachangiaji watumie hyo lugha, maana kama mimi naweza kutumia lugha nne tofauti za kimataifa na kiingereza ni mojawapo, ila natumia kiswahili kwa sabab wengi tunakifaham.
Acheni hyo tabia.