Namshukuru sana Mungu kwa yote aliyonikubalia mwaka huu wa 2013; kubwa zaidi nimemaliza masters salama sio tu nimeongeza cheti bali fikra; kipato na cheo vimeongezeka; wadau wa jamii forum wamekuwa chachandu katika masomo yangu; na graduate mwakani najua wengi hamtakuwepo lakini ndani ya nafsi yangu mtakuwepo; Jamii Forum sio darasa dogo ni pana mithili ya bahari; wakati najiandaa kuanza rasmi majukumu yangu rasmi January 06 2014, itakuwa sio uungwana kama sitawashukuru wanajamii forum; Mamndenyi muhibu wangu hujui ulikuwa unanifariji kiasi gani lakini ni ukweli usiokificho maneno yako yalikuwa yananiliwaza; Bujibuji mtani wangu darasa lako burudani; Bishanga utata wako ni fundisho kwangu; Baba V imenifundisha uzee sio hekima; wakuu Ritz; ZeMarcopolo; CHAMVIGA hekima zenu ni chachandu katika maisha yangu.
Nawatakia wote heri na fanaka ya mwaka mpya wote na wanajamii wote yaliyopita si ndwele tugange yajayo; elimu ni ufunguo wa maisha JAMII FORUM ni darasa litumieni ipasavyo msitumike tu kuandika pumba kwa kuwafurahisha watu litumieni kupanua wigo wa fikra!

Last edited by a moderator: