Heri ya Kuzaliwa Kamanda wa Anga Freeman Mbowe

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
31,427
2,000
Leo tuna sheherekea siku ya nchi yetu ilipo pata Uhuru kutoka kwa wakoloni (Waingereza)
Siku hii ni muhimu sana kwa watanzania kwani ni siku iliyo tupa uhueu wa kujitawala wenyewe kama nchi tukiwa na mamlaka kamili ya kujiongoza. Niliwahi kusimuliwa na mama yangu ni kwa jinsi gani wananchi walivyo kumbwa na furaha isiyo elezeka pale walipo tangaziwa kwamba sasa wapo huru katika nchi yao, hakika ilikuwa ni furaha ya ushindi.

Lakini pia tarehe kama ya leo ya Uhuru wa nchi, Alibatizwa mtu muhimu sana kwa nchi, kwa wananchi na kwa siasa za upinzani na demokrasia. Mtu huyu alibatizwa na kuitwa Mtu Huru (Freeman) ambaye amekuja kuwa kielelezo bora cha siasa za ushindani, asiye tetereka, asiye yumbishwa na kudanganywa na peremende za vyeo na fedha. Hakika ame simamia jina lake na ame ishi kwa kuwa huru kwa maoni, mtazamo, fikra na matendo. Yeye ndiyo nguzo ya upinzani, yeye ndiye aliye jenga Chadema yenye falsafa na misingi inayo kuwa. Ipo siku Tanzania ita simama na kukuita KAKA WA TAIFA.

HAPPY DAY Tanzania, HAPPY DAY Freeman.
 

Mtwintwi

Member
Dec 20, 2012
46
95
Happy birthday Mwenyekiti wa chama cha mwanachama wanaojitambua na uelewa mpana wa siasa. Mungu akupe maisha marefu ili ushuhudie 2020 tunavyochukua dola CHADEMA.
Hayo ndiyo maneno yanayowakosesha kura nyinyi nyumba! Kwa hiyo ss ACT ss CUF ss NCCR na wengine hatujitambui! Then unategemea jicho chama kushika dola? Hujatinga Ikulu unatoa maneno ya kejeli cku ukiingia Magogoni? Angalia kauli zenu ndiyo zinatuponza UKAWA!
 

Chanyauru

Senior Member
Jul 4, 2016
172
250
huwa ananikosha kwenye uchaguzi wa wabunge viti maalum tu.Utasikia devotha minja kutoka morogoro, jesca kishoa kutoka singida, anna komu kutoka sijui wapi ni full kujaza wachaga tu.Achen kuhadaa wabongo wasiojielewa na mtaendelea kupukutika! hadi 2030 chadema itakufa rasmi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom