Heri ya kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo

Heri ya kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo

Tony Laurent

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
6,383
Reaction score
8,272
Amani ya YESU KRISTO iwe nanyi ndugu Watanzania wenzangu

Naomba kutumia fursa hii kumtambulisha kwenu Yesu Kristo MFALME WA AMANI

ISAYA 9:6 "Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani."

• Yesu Kristo anayo majina mengi ambayo yote yamebeba maana na nguvu katika ujumla wa wokovu kwa mwanadamu. Moja ya jina la Yesu ni Mfalme wa Amani. Neno mfalme linabeba utawala, ukuu, uongozi ikiwa na maana katika masuala yote ya amani kiongozi wake Mkuu ni YESU KRISTO. Utawala wake wa amani unapatikana katika ulimwengu wa Roho wa Nuru.

• Kwa upande wa pili yaani katika ulimwengu wa roho wa giza yupo Shetani ambaye pia ni mfalme wa amani katika katika utawala wake. Huwa anatoa amani kwa wale wanaohitaji huduma hiyo kutoka katika utawala wake. Miongoni mwa kazi za Shetani ni kughushi mambo halisi yanayopatikana katika ulimwengu wa Roho wa Nuru. Lengo lake ni kuwachanganya watu ili washindwe kutambua AMANI halisi inapatikana wapi!!!

• Sijui hadi kufikia Christmas hii na mwisho wa mwaka huu, una jambo gani ambalo limekuwa likikukosesha amani. Je, ni magonjwa, uchumi duni, kukosa ajira, kufeli masomo, kusalitiwa, kufiwa, kuonewa, kurogwa n.k? Nakutia moyo kwamba, amani ya kweli, na ya kudumu na yenye uhakika hupatikana kwa KRISTO YESU pekee. Shetani naye anayo amani lakini ni ya kitambo na ina hila ndani yake, anakupa amani ya kughushi na lengo lake kuu ni kukutesa na kukufanya mateka katika ulimwengu wake uliojaa dhambi.

Usikubali Christmass hii na mwisho wa mwaka huu wa 2025 upite bila kuipokea amani ya YESU KRISTO moyoni mwako. Miongoni mwetu huenda Amani ya Kristo tayari tulishaipokea, lakini kuna sehemu tumejikwaa na kuamua kuifuata amani ya upande wa pili- ambayo ni ya kughushi na ni mtego. Maombi yangu kwa Mungu leo ni kwamba, atujalie sote tuliojikwaa Kwa namna moja au nyingine tuanze upya na YESU KRISTO.

• Mungu atusaidie pia kwamba, kuanzia leo kupitia MFALME WA AMANI- YESU KRISTO tusikae na dhambi yoyote mioyoni mwetu.

Tujifunze kujisamehe wenyewe na kuwasamehe wote waliotukosea. Tusikubali kukaa na kinyongo chochote mioyoni mwetu. Mungu anatuagiza tuishi maisha matakatifu yenye haki na kuitafuta amani kwa bidii.

Waebrania 12:14 "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;"

Mathayo 5:10
"Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni
wao"

Mithali 14:34
Haki huinua taifa;
Bali dhambi ni aibu ya watu wowote

Mithali 28:13
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;
Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

HERI YA KRISMASI KWAKO NA WOTE UWAPENDAO NA MWAKA MPYA WENYE BARAKA MAFANIKIO WA 2026.
 
Yesu alizaliwa tarehe sawa na ya leo na anayepinga atuambie alizaliwa lini.
 
Kwenye Bible sijaona walipoandika alizaliwa tarehe 25 December.
 
Mitubwi waliyokuja nayo wazungu imetuingiza katika utumwa wa akili na maarifa kwa karne nyingi mpaka sasa.kataa utumwa
 
Back
Top Bottom