Heri upweke mara 100 kuliko mpenzi asiyejua maana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heri upweke mara 100 kuliko mpenzi asiyejua maana.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by chriss brown, Dec 18, 2011.

 1. chriss brown

  chriss brown JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAPENZI yana siri kubwa. Kila mmoja ana ugonjwa wake wa kupenda. Wengine wanawapenda wapenzi warefu, lakini kuna kundi ambalo huchanganyikiwa zaidi kwa wafupi. Pamoja na mchanganuo huo, kuachwa inauma hata kama anayekutosa hukuwa na mapenzi naye.

  Ile dhana tu ya kuachwa ndiyo hutesa watu. Kuna dhana kwamba anayeacha mara nyingi hujiona mshindi dhidi ya aliyemuacha. Na hiyo ndiyo sababu ya wengi kuumia wanapofungiwa milango ya kukatisha uhusiano ambao pengine hata hawakuwa na masilahi nao.
  Mathalan, mwanamke anaweza kuwa havutiwi na mtu aliyenaye kwa maana moja au nyingine. Ilitokea kuwa naye kama ajali tu! Kutokana na kutokuwa na hisia naye, hakuona tatizo kumsaliti kwa mwanaume mwingine, lakini huwezi kuamini siku akiambiwa basi, atalia machozi na kuomba msamaha.

  Si kwamba atalia kwa sababu ya mapenzi ya dhati aliyonayo kwa mwenzi wake, kwamba inamuuma kuachana naye, ila kinachomtesa ni zile hisia za kuachwa. Na ingetokea kuwa yeye ndiye anayeamua kuacha, tafsiri ingekuwa kinyume chake.
  Macho yangekuwa makavu na ikiwezekana angekwenda kusimulia kwa marafiki: "Aah, James nimempiga chini kanililia huyo!" Anafurahi dada yetu na wenzake watampongeza kwa kugongesheana viganja!

  Tatizo kubwa ambalo linawagharimu wengi ni kuwa mapenzi yanabebwa kama aina ya mchezo wa kuigiza. Watu wanaingia kwenye uhusiano kwa kujaribu. Kuna waliofunga ndoa si kwa kuchaguana, isipokuwa walidanganyana kwa hisia za "mapozeo" mwisho wa siku wakazoeana, ikawa ngumu kuachana.

  Wapo wanaoingia kwenye ndoa si kwa kuvutwa na nyoyo zao, ila wanakabiliwa na fikra za "waoaji wenyewe hawapo, acha nimkubali huyu huyu!" Mapenzi ni nguzo maalum mno kwa maisha ya binadamu, kwa hiyo ni vema yabebe heshima inayostahili.

  Ogopa sana mtu anayekuwa na wewe kwa sababu haoni chaguo lake. Adhabu yako ni kubwa mbele ya safari ingawa unaweza kujiona upo kwenye bwawa la asali mwanzoni. Kiama chako ni pale atakapomuona anayedhani ndiye sahihi kwake. Utasilitiwa upende usipende!
  Nimekuwa nikisisitiza hili kuwa ni bora kuacha kumsogelea kabisa kuliko kumdanganya unampenda wakati unamcheza shere. Ukatili wako ni mkubwa kwa maana yeye anaweza kudhani amefika na akatuliza ‘mizuka' yote, hivyo akapandikiza matarajio juu yako.

  Siku atakapojua haupo naye atajisikiaje? Unaweza kuua bila kukusudia kwa sababu binadamu tumeumbwa na roho tofauti. Utamuona aliyekunywa sumu kwa mapenzi ni mjinga kwa sababu hayajakufika. Kuna waliosema wao ni ngangari lakini ukurasa ulipofunguka kwao, waliona dunia chungu.

  USIJARIBU MAPENZI

  Dhana ya mapenzi duniani kote inaelekeza kwamba asili yake ni moyoni. Hii ina mantiki kuwa ndani ya kila mtu kuna vitu ambavyo anahisi kuhitaji mwenzi wake awe navyo. Sura, umbo na tabia.

  Hata hivyo, kuna nakshi nyingi ambazo si za lazima lakini hutokea kuwavutia watu na kufunika hata yale ya msingi.
  USHAURI: Zingatia sifa muhimu na kuachana na vionjo vya ziada (accessories).

  Kuna mwanamke yeye huvutiwa na mwanaume mwenye kucha ndefu.

  Ukimuuliza, anakwamba basi tu napenda. Mwingine anaweza kusema: "Nikiwa naye napenda kuichezea, naskia raha!" Yupo atakayekueleza: "Ile kucha yake akinipitishia mgoni au shingoni kwangu taabani!"

  Ni vionjo tu vya ziada! Kuna wasiotaka mambo mengi ila wakikutana na watu ambao wananukia ni balaa! Wapo watakaosema wanataka wachangamfu, ingawa mapepe yakizidi nayo ni tatizo kubwa, ila mwingine atadai anahitaji mpenzi anayejua Kiingereza.

  Ipo sifa nyeti kwenye dimbwi la mahaba. Kama karata zako unazicheza vizuri kwa mwandani wako na kuhakikisha kila mnapoachiana anakuwa ameridhika kwa 100% ni turufu ya kulinda penzi lako.

  JAMBO MUHIMU KWAKO

  Penda kujiona mtu nambari moja kwa ubora kwa sababu Mungu aliona una umuhimu ndiyo maana akakuumba. Linda thamani na heshima yako, usikubali mapenzi yakuondolee nguvu ambayo Mfalme wa Mbingu na Ardhi amekupa.

  Ni rahisi kudharauliwa ikiwa utakuwa na mtu ambaye hana mapenzi ya dhati na wewe. Atakusaliti, watu watazungumza pembeni. Atakusema vibaya, ukipita mitaani utaonekana kituko. Mpenzi mwenye uelewa na anayekupenda kwa dhati, atakulinda mahali popote.

  Hatakusaliti, ataishi ndani yako. Linalokuuma, litamtesa. Wasiokupenda atawachukia. Marafiki zako atawageuza ndugu. Kinyume chake ni kwamba mwenzi asiyekupenda kwa dhati, si ajabu akashiriki kukumaliza.

  Kuna watu hawaoni hili umuhimu, mpenzi maana yake ni msiri wa maisha yako. Unapokuwa umelala fofofo hujitambui, ubavuni kwako yupo yeye. Anaweza kukufanya lolote wakati wewe unaogelea ndotoni. Mpende akupendaye, vinginevyo utakumbana na maumivu yafuatayo;

  HATOKUSIKILIZA IPASAVYO

  Mapenzi ni hisia. Ni rahisi kwako kujua kwamba uliyenaye anakupenda kwa dhati mnapokuwa mnazungumza. Je, anakusikiliza kiasi gani?
  Mtu ambaye hana mapenzi na wewe, hata umwambie kwa lugha gani hawezi kukuelewa. Tena inawezekana ulizungumza naye jana kwa herufi kubwa, lakini leo jua limechomoza anarudia yale yale.

  Inawezekana ulimuonya kuhusu tabia ambazo zinakufanya heshima yake ipotee. Hakatazwi kuwa na marafiki wa jinsia nyingine, lakini mazoea yake siyo mazuri kiasi kwamba wanaweza kutembea barabarani wameshikana viuno. Ikiwa unamueleza habadiliki, huyo hakupendi. :lol::lol::lol:
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu ngoja nitaimalizia baadae ila nahisi CB umepigwa chambavu maana hii ni post ya pili unaongelea mashosti job true true..
   
 3. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Dah........ngoja kwanza ninywe uji!
   
 4. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Eeeeh! kweli hizo "makala" zinazohusu kupendwa na kutokupendwa umeziamkia leo...maana si mchezo..! Keep it up bwana chriss brown..
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  yanarani duniaaaaaaa, yanarani duniaaaaa
  ila strory ndefu iyo.
   
 6. Candy kisses

  Candy kisses JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkubwa hakika umefunguka.!
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kina nafasi yake na wakati wake so utasema hivyo ukiwa huko na ukitoka huko utaona ni bora hakuna kilichokamilika
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kina nafasi yake na wakati wake so utasema hivyo ukiwa huko na ukitoka huko utaona ni bora hakuna kilichokamilika bali uvumilifu na busara
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Mh!Ndefu hiyo,nitarudi kumalizia!
   
 10. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Brown! Imetulia 100% !
  Ndiyo hizi tunazosema zimeandaliwa "Out of the pitch! " umeifikiri nje ya box ! Ukiingia uwanjani pasi moko ---> Nyavu!
   
 11. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sante Chriss, makala nzuri mungu akubariki
   
 12. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sredi nzuri cb
  Ntamalizia kusoma baadae ,
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  leo! Kila nikifungua thread nakuta ni wewe umepost. Hongera sana. Asante kwa madarasa
   
 14. DULLAH B.

  DULLAH B. JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 674
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hayo yalinikuta. Mke anickii kila nikimrekebisha yy anaona nakosea. Nikaachana nae!
   
 15. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Perfect mkubwa
   
 16. C

  CHEMBUNA New Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama binadamu hatuoni umuhimu\value ya kitu au mtu mpaka hakipo.eg huoni umuhimu wa kitu kama remote contol till imeisha battery n u realize ooops kumbe nayo ilikuwa na nafasi yake...we take pipo valuable to us for granted till they move on and its too late then reality hits hard. ...definately an eye opener
   
 17. M

  Myn17 Senior Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu bonge la darasa,ubarikiwe.
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [h=3]
  [/h]
  MAPENZI yana siri kubwa. Kila mmoja ana ugonjwa wake wa kupenda. Wengine wanawapenda wapenzi warefu, lakini kuna kundi ambalo huchanganyikiwa zaidi kwa wafupi. Pamoja na mchanganuo huo, kuachwa inauma hata kama anayekutosa hukuwa na mapenzi naye.

  Ile dhana tu ya kuachwa ndiyo hutesa watu. Kuna dhana kwamba anayeacha mara nyingi hujiona mshindi dhidi ya aliyemuacha. Na hiyo ndiyo sababu ya wengi kuumia wanapofungiwa milango ya kukatisha uhusiano ambao pengine hata hawakuwa na masilahi nao.

  Mathalan, mwanamke anaweza kuwa havutiwi na mtu aliyenaye kwa maana moja au nyingine. Ilitokea kuwa naye kama ajali tu! Kutokana na kutokuwa na hisia naye, hakuona tatizo kumsaliti kwa mwanaume mwingine, lakini huwezi kuamini siku akiambiwa basi, atalia machozi na kuomba msamaha.

  Si kwamba atalia kwa sababu ya mapenzi ya dhati aliyonayo kwa mwenzi wake, kwamba inamuuma kuachana naye, ila kinachomtesa ni zile hisia za kuachwa. Na ingetokea kuwa yeye ndiye anayeamua kuacha, tafsiri ingekuwa kinyume chake.

  Macho yangekuwa makavu na ikiwezekana angekwenda kusimulia kwa marafiki: “Aah, James nimempiga chini kanililia huyo!” Anafurahi dada yetu na wenzake watampongeza kwa kugongesheana viganja!

  Tatizo kubwa ambalo linawagharimu wengi ni kuwa mapenzi yanabebwa kama aina ya mchezo wa kuigiza. Watu wanaingia kwenye uhusiano kwa kujaribu. Kuna waliofunga ndoa si kwa kuchaguana, isipokuwa walidanganyana kwa hisia za “mapozeo” mwisho wa siku wakazoeana, ikawa ngumu kuachana.

  Wapo wanaoingia kwenye ndoa si kwa kuvutwa na nyoyo zao, ila wanakabiliwa na fikra za “waoaji wenyewe hawapo, acha nimkubali huyu huyu!” Mapenzi ni nguzo maalum mno kwa maisha ya binadamu, kwa hiyo ni vema yabebe heshima inayostahili.

  Ogopa sana mtu anayekuwa na wewe kwa sababu haoni chaguo lake. Adhabu yako ni kubwa mbele ya safari ingawa unaweza kujiona upo kwenye bwawa la asali mwanzoni. Kiama chako ni pale atakapomuona anayedhani ndiye sahihi kwake. Utasilitiwa upende usipende!

  Nimekuwa nikisisitiza hili kuwa ni bora kuacha kumsogelea kabisa kuliko kumdanganya unampenda wakati unamcheza shere. Ukatili wako ni mkubwa kwa maana yeye anaweza kudhani amefika na akatuliza ‘mizuka’ yote, hivyo akapandikiza matarajio juu yako.

  Siku atakapojua haupo naye atajisikiaje? Unaweza kuua bila kukusudia kwa sababu binadamu tumeumbwa na roho tofauti. Utamuona aliyekunywa sumu kwa mapenzi ni mjinga kwa sababu hayajakufika. Kuna waliosema wao ni ngangari lakini ukurasa ulipofunguka kwao, waliona dunia chungu.

  USIJARIBU MAPENZI

  Dhana ya mapenzi duniani kote inaelekeza kwamba asili yake ni moyoni. Hii ina mantiki kuwa ndani ya kila mtu kuna vitu ambavyo anahisi kuhitaji mwenzi wake awe navyo. Sura, umbo na tabia.

  Hata hivyo, kuna nakshi nyingi ambazo si za lazima lakini hutokea kuwavutia watu na kufunika hata yale ya msingi.

  USHAURI: Zingatia sifa muhimu na kuachana na vionjo vya ziada (accessories).
  Kuna mwanamke yeye huvutiwa na mwanaume mwenye kucha ndefu.

  Ukimuuliza, anakwamba basi tu napenda. Mwingine anaweza kusema: “Nikiwa naye napenda kuichezea, naskia raha!” Yupo atakayekueleza: “Ile kucha yake akinipitishia mgoni au shingoni kwangu taabani!”

  Ni vionjo tu vya ziada! Kuna wasiotaka mambo mengi ila wakikutana na watu ambao wananukia ni balaa! Wapo watakaosema wanataka wachangamfu, ingawa mapepe yakizidi nayo ni tatizo kubwa, ila mwingine atadai anahitaji mpenzi anayejua Kiingereza.

  Ipo sifa nyeti kwenye dimbwi la mahaba. Kama karata zako unazicheza vizuri kwa mwandani wako na kuhakikisha kila mnapoachiana anakuwa ameridhika kwa 100% ni turufu ya kulinda penzi lako.

  JAMBO MUHIMU KWAKO

  Penda kujiona mtu nambari moja kwa ubora kwa sababu Mungu aliona una umuhimu ndiyo maana akakuumba. Linda thamani na heshima yako, usikubali mapenzi yakuondolee nguvu ambayo Mfalme wa Mbingu na Ardhi amekupa.

  Ni rahisi kudharauliwa ikiwa utakuwa na mtu ambaye hana mapenzi ya dhati na wewe. Atakusaliti, watu watazungumza pembeni. Atakusema vibaya, ukipita mitaani utaonekana kituko. Mpenzi mwenye uelewa na anayekupenda kwa dhati, atakulinda mahali popote.

  Hatakusaliti, ataishi ndani yako. Linalokuuma, litamtesa. Wasiokupenda atawachukia. Marafiki zako atawageuza ndugu. Kinyume chake ni kwamba mwenzi asiyekupenda kwa dhati, si ajabu akashiriki kukumaliza.

  Kuna watu hawaoni hili umuhimu, mpenzi maana yake ni msiri wa maisha yako. Unapokuwa umelala fofofo hujitambui, ubavuni kwako yupo yeye. Anaweza kukufanya lolote wakati wewe unaogelea ndotoni. Mpende akupendaye, vinginevyo utakumbana na maumivu yafuatayo;

  HATOKUSIKILIZA IPASAVYO

  Mapenzi ni hisia. Ni rahisi kwako kujua kwamba uliyenaye anakupenda kwa dhati mnapokuwa mnazungumza. Je, anakusikiliza kiasi gani?

  Mtu ambaye hana mapenzi na wewe, hata umwambie kwa lugha gani hawezi kukuelewa. Tena inawezekana ulizungumza naye jana kwa herufi kubwa, lakini leo jua limechomoza anarudia yale yale.

  Inawezekana ulimuonya kuhusu tabia ambazo zinakufanya heshima yake ipotee. Hakatazwi kuwa na marafiki wa jinsia nyingine, lakini mazoea yake siyo mazuri kiasi kwamba wanaweza kutembea barabarani wameshikana viuno. Ikiwa unamueleza habadiliki, huyo hakupendi.

  Hakusikilizi kwa sababu hana hisia na wewe.

 19. Himidini

  Himidini JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2013
  Joined: May 8, 2013
  Messages: 5,570
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 145
  ^^
  MziziMkavu
  Kuna jambo umenifumbua nitalifanyia kazi.
  Lakini vipi hapo pa mapenzi asili yake moyoni,,huoni uasili huo ******* giza sasa na pesa?
  ^^
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Heri upweke kuliko mpenzi asiyejua maana 2

  KILA mtu angeyaheshimu mapenzi, angejua jinsi ya kulinda hisia za mwenzi wake. Angeelewa maana ya kupenda, asigekuwa na shaka pale anapopendwa. Angeishi ndani ya mwenzake, hivyo kuumizana kusingekuwepo, migogoro mikubwa na kuachana isingetokea.

  Migogoro mingi inatokea kwa sababu wengi wameyageuza mapenzi kama mchezo (game), hawajui kuwa saikolojia inaonya vitendo vya kuucheza shere moyo wa mtu. Kumfanyia hivyo mtu mwenye hisia za ndani na za kweli katika kupenda unaweza kuua bila kukusudia.

  Katika sehemu ya kwanza ya makala haya nilieleza kuwa kama hujawa tayari kupenda, kunyenyekea na kuheshimu ni vizuri ukakaa pembeni kwa sababu unaruhusiwa kucheza game na mtu lakini ni kosa kubwa kucheza game na moyo wa mtu.

  Hata hivyo, nilitaka kila mtu awe makini anapokuwa anaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu. Anapaswa kujihakikishia upendo kutoka moyoni badala ya kujaribu. Wengi walioingia kwa mtindo wa kupima kina cha maji, walilia kwa kusaga meno.

  Lipo tabaka ambalo linakuwa limejitosheleza kuwa mapenzi hamna lakini wanang'ang'ania, matokeo yake wanauguza jeraha la moyo kwa muda mrefu. Wengine wakajipa ugonjwa wa moyo. Ni vizuri kuwa makini mno ikiwa unahitaji kupata thamani halisi ya penzi.

  Pigania kuhifadhi moyo wako. Uweke katika himaya salama. Usijidanganye kwa penzi lisilo na uelekeo. Lenye sura ya upande mmoja. Wewe unapenda, yeye anakuchora, presha inakupanda na kushuka mwenzako hana habari hata kidogo, tena ikiwezekana atakucheka kama katuni.

  Kuna watu hawaoni hili umuhimu, mpenzi maana yake ni msiri wa maisha yako. Unapokuwa umelala fofofo hujitambui, ubavuni kwako yupo yeye. Anaweza kukufanya lolote wakati wewe unaogelea ndotoni. Mpende akupendaye, vinginevyo utakumbana na maumivu yafuatayo;

  HATAKUSIKILIZA IPASAVYO

  Mapenzi ni hisia. Ni rahisi kwako kujua kwamba uliyenaye anakupenda kwa dhati mnapokuwa mnazungumza. Je, anakusikiliza kiasi gani?

  Mtu ambaye hana mapenzi na wewe, hata umwambie kwa lugha gani hawezi kukuelewa. Tena inawezekana ulizungumza naye jana kwa herufi kubwa, lakini leo jua limechomoza anarudia yale yale.

  Inawezekana ulimuonya kuhusu tabia ambazo zinakufanya heshima yake ipotee. Hakatazwi kuwa na marafiki wa jinsia nyingine, lakini mazoea yake siyo mazuri kiasi kwamba wanaweza kutembea barabarani wameshikana viuno. Ikiwa unamueleza habadiliki, huyo hakupendi.
  Hakusikilizi kwa sababu hana hisia na wewe.

  ATAPENDA KUKUFANANISHA

  Haamini kama wewe ni mwanamke au mwanaume mwenye mvuto kamili. Akiona wengine barabarani ni rahisi kushawishika. Atajiuliza hivi huyu na wangu vipi? Huyu anaonekana ni mzuri zaidi. Anajiuliza maswali hayo kwa sababu hajakukubali. Shtuka mapema.

  Mwanasaikolojia Brandon King katika makala yake: "Be aware with ones heart!" anasema kuwa ni rahisi mtu kujidanganya kwamba aliyenaye siyo chaguo sahihi kwa sababu yupo naye lakini hiyo hutokea kwa mtu ambaye mapenzi yake si asimilia 100.

  Anasema: "Vitu vya thamani yeye huvichukulia ni rahisi. Hajui kama mpenzi wake ni wa gharama kubwa. Mtu wa barabarani labda kwa sababu tu amevaa kapendeza, yeye ataanza kumfananisha na mwenzi wake nyumbani na ikiwezekana kumuona bora.

  "Wengine hawana uvumilivu, kwa hiyo wanaweza kujikuta wakimwaga sifa kwa watu wa pembeni. Wakiendelea huharibu kabisa kwa sababu hujikuta wakiwaeleza hata wapenzi wao, kitu ambacho taaluma ya saikolojia katika eneo la mapenzi inakataza."

  Brandon anaonya: "Ni kosa kubwa kumsifia mtu wa jinsia inayofanana na mwenzi wako mbele yake. Mfano unamwambia mwenzi wako wa kiume kwamba ‘yule kaka mzuri jamani'! Hata kama huna hisia za ndani ya moyo wako lakini haiwezi kumpa picha nzuri, atajiona hayupo salama kwamba unavutiwa na mwingine.

  "Fikiria na wewe upande wako. Mwenzi wako anamuona mwanamke na yeye anamwagia sifa, ‘dah yule manzi mrembo, wewe ungekuwa mrembo kama yeye ningejidai sana'! Bila shaka utaumia sana, kwa hiyo na yeye ndivyo anavyoweza kupata maumivu."

  Anashauri: "Kila mmoja aridhike kwa jinsi mwenzi wake alivyo. Haikusaidii kitu kumuona bora wa jirani kwani kuna wenzako wanajiuliza huyo wako watampataje? Mheshimu na mtukuze mbele za watu. Ukijenga imani kwamba mpenzi wako ni bora kuliko wote duniani, itakuwa na moyo wako utakubali."

Loading...