Heri upweke mara 100 kuliko mpenzi asiyejua maana.

^^
MziziMkavu
Kuna jambo umenifumbua nitalifanyia kazi.
Lakini vipi hapo pa mapenzi asili yake moyoni,,huoni uasili huo unatiwa giza sasa na pesa?
^^
Hapana Himidini mapenzi ya kweli hayatiwi giza na pesa. Na kama mtoa mada alivyosema anaekupenda kwa dhati/ kwa pesa utamjua tu kwani kuna kitu ambacho Mungu ameweka ndani ya mioyo yetu sema mara nyingi tunapokua tumezama huko huwa hatupendi kuisikiliza sauti ya ndani. Unaweza kabisa kuziona dalili mbaya na ukazipotezea.
 
Last edited by a moderator:
Hapana Himidini mapenzi ya kweli hayatiwi giza na pesa. Na kama mtoa mada alivyosema anaekupenda kwa dhati/ kwa pesa utamjua tu kwani kuna kitu ambacho Mungu ameweka ndani ya mioyo yetu sema mara nyingi tunapokua tumezama huko huwa hatupendi kuisikiliza sauti ya ndani. Unaweza kabisa kuziona dalili mbaya na ukazipotezea.

^^
Ni kweli Ablessed lakini kama tutachukua muda kujadili hili,basi ninachokiona pesa imekuwa njia kuu ya kumpata mwenza au pengine kupata penzi la dhati.MF.kuna rafiki yangu ambaye alimpenda sana binti fulani.Japo hata yule binti alimpenda,lakini kundi lililomzunguka yule binti na binti mwenyewe walimkataa kwa ajili ya ufukara wa huyu rafiki yangu.
NINI KILITOKEA
Rafiki yangu aliamua kuazima (toka mbali) sofa,subwoofer,Tv,na mavazi kwa rafiki yake.Na akakopa pesa ya kutosha kutoka kwa kazi yake,ni hapo binti alipopagawa na familia yake ikakubali kuwa kwa uzuri wa yule binti sasa yule rafiki yangu alikuwa na hadhi ya kumuoa.Ndoa ikabarikiwa.
Binti alipopata ujauzito tu,,yule rafiki yangu akarudisha kila kitu kwa mdhamini wake,na binti akachanganyikiwa lakini akamsifu kwa akili hiyo..
Wameishi vema sasa wana watoto 3 gari 1 nyumba yao na miradi ya kukidhi mahitaji.Wapo Arusha.
HUONI KUWA PESA NDIO KIVUTIO CHA PENZI LA DHATI hususani kizazi cha sasa?
Cc: MziziMkavu
^^
 
Last edited by a moderator:


..... Watu wanaingia kwenye uhusiano kwa kujaribu.
.... Kuna waliofunga ndoa si kwa kuchaguana, isipokuwa walidanganyana kwa hisia za "mapozeo" mwisho wa siku wakazoeana, ikawa ngumu kuachana.
... Wapo wanaoingia kwenye ndoa si kwa kuvutwa na nyoyo zao, ila wanakabiliwa na fikra za "waoaji wenyewe hawapo, acha nimkubali huyu huyu!"

Ogopa sana mtu anayekuwa na wewe kwa sababu haoni chaguo lake. Adhabu yako ni kubwa mbele ya safari ingawa unaweza kujiona upo kwenye bwawa la asali mwanzoni.


MziziMkavu, hii ni mojawapo ya thread zenye mafundisho ya kina juu ya mahusiano. Natamani kila mwana JF angepitia kwa umakini, na kisha kuelewa na kuyafanyia kazi yaliyomo. Wengi wetu huingia kwenye mahusiano kwa sababu nyepesi nyepesi kama alivyoorodhesha baadhi yake hapo juu. Na motokeo yake ni kujikuta unageuka kuwa MHANGA wa ndoa!!! Ni hatari kwa afya ya moyo, mwili na akili yako!
Thanks MziziMkavu!
 
MziziMkavu, uliyosema uliyosema ni kweli, mapenzi ni hisia ya ndani ya mtu wa jinsia moja kwa mtu wa jinsia nyingine. Mara nyingi watu wanarahisisha sana wanakuwa marafiki na hatimaye kufunga ndoa, wakishafunga ndoa ndio sasa mtu anagundua vitu fulani fulani kwamba havipendi kwa mwenzie na kama angevigundua kabla ya kufunga ndoa pengine asingethubutu kufunga ndoa na mtu huyo, lakini inakuwa too late.

Mtazamo wangu ktk hili;
Kwanza pamoja na hisia zako, muombe Mungu akusaidie kufanya uamuzi wa kumchagua mtu maana Mungu ndiye anajua mke/mume wako ni nani na hata kama kutakuwa na kasoro baadae mtachukuliana na kusameheana kwa wepesi maana upendo hapo ni wa dhati.

Kinachonishangaza;
Wazee wetu wa zamani walikuwa wanawachulia mke/mume watoto wao na maisha yao yalikuwa yanaenda vizuri sana, nadhani na Mungu alikuwa anahusika ktk hilo, hayo ni maoni yangu
 
mapenzi yanauma jamani,
unaempenda hajui thamani ya penzi lako
thats when I come to realise

love is no longer blind.........
love is future

well said MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Heri upweke kuliko mpenzi asiyejua maana III


KATIKA somo lililopita kama nilivyogusia ushauri wa Brandon King na makala yake ya “Be aware with ones heart” nilieleza kuwa ni kosa kubwa kumuona mwenzi wako ana thamani ndogo na wakati huo huo ukawa unatoa kipaumbele kwa watu wa pembeni.

Tafsiri inayotawala katika uhusiano ni kuwa kundi linalosumbua mno na kuonekana ni sugu kwa tabia ya namna hii ni lile ambalo linawahusisha memba wanaoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi pasipo imani kamili.
Wanajaribu na hawana ufahamu kwamba moyo haufanyiwi majaribio.
Hii ndiyo sababu ya kusisitiza kuwa ikiwa hujaamua kupenda basi kaa mbali.

Kuna mengi unayoweza kumsababishia mwenzako, ukampotezea muda huku ukimjengea imani upo naye lakini mwisho anakuja kujikuta anauguza dondo la moyo.
Sikitiko la mahaba linashinda msiba!
Hujaumia subiri usimuliwe.

Moyo unapouma kwa sababu ya mapenzi hakuna kitu cha kupoza. Unaweza kunywa pombe na usilewe, ukabugia dawa za usingizi na usilale.
Kifua kinajaa na kwa sababu inaathiri mfumo wa upumuaji na mapafu nayo huingia katika maumivu.
Sikitiko la mahaba ni hatari, likikufika utapungua uzito kwa kasi bila maelezo ya ziada.

Chakula hakiwezi kupita na macho yanaweza kujaa machozi ilhali unatamani kujizuia. Binadamu tumetofautiana, wapo wanaotamani kupendwa lakini wengine wanawacheza shere wanaowapenda.
Dawa kuu ni kujihadhari na watu wasio na mapenzi ya dhati.

Kuwaepuka kadiri inavyowezekana.

Ni mzuri na anakuvutia lakini heri umuone kwa mbali kwa sababu ukimjaza moyoni atakusumbua.
Atakutoa machozi katika eneo ambalo ulihitaji kufurahi.
Maumivu yako hata yajali kwa sababu hana hisia na wewe.

Atakusaliti bila woga kwa maana hana hofu yoyote juu yako.
Itakuwa ngumu kumuacha, vilevile utaona uamuzi wowote wa kutengana naye ni mateso makubwa kwamba heri uumie ukiwa naye kuliko kuachana.

Usijidanganye ndugu yangu, wewe ni binadamu uliyekamilika, kwa hiyo usitarajie mtu wa pili au wa tatu anaweza kusikia kile kinachokuuma moyoni.

Mateso yaliyopo ndani yako unayajua mwenyewe, kwa hiyo unatakiwa kuwa wa kwanza kujihurumia na kuchukua uamuzi wa kujiokoa na mateso.

Kuna kitu kimoja ambacho unatakiwa kukifahamu; Binadamu ni wa ajabu sana, watayajua yako ya siri na kile ambacho mwenzi wako anakifanya pembeni, lakini hawakwambii badala yake wataketi pembeni kuzungumza. “Aah yule wa ajabu, anadhani kapata mpenzi kumbe kapatikana!”

Wengine utakaa nao meza moja kushauriana mambo mbalimbali, lakini anayekwambia umvumilie mwenzi wako licha ya vitimbi anavyokufanyia, ndiyo huyo huyo akikaa pembeni na watu anawaambia kwa mtindo wa kukucheka kwamba unamng’ang’ania mpenzi bomu.

Lingine ni kuwa unapokuwa na mpenzi ambaye hakuheshimu, thamani yako katika jamii inashuka.
Kukuheshimu si mpaka akutukane, bali vitendo vyake. Kutoka na wapenzi wengine, kujenga mazoea na watu wa jinsia nyingine kiasi kwamba mpaka anahusishwa kwamba ni wapenzi wake.

Mathalan, mpenzi wako anakuwa na urafiki na watu mpaka anafikiriwa anatembea nao.
Hii ni tabia mbaya na haikubaliki, ingawa wapo wazuri wa kutetea. Watasema, sisi ni washkaji ila fahamu mapenzi yenu yanazikutanisha familia mbili. Una ndugu, marafiki, wazazi.

Inakuaje mpenzi wako anahisiwa anatoka na mwanamke mwingine na taarifa zinafika mpaka kwa wazazi wako? Watajua mkwe wao ni kicheche na hilo litakugharimu kwa kiasi kikubwa.

Unatakiwa kulinda thamani, heshima na utu wako, kwa hiyo achana na mtu asiyejua maana!
Unaweza kuona leo inakuuma kwa sababu unaepukana na mtu ambaye unampenda lakini hiyo ni nafuu kwako kesho.
Amini kwamba mwisho wa mateso hayo ya moyo ni furaha kubwa, mwisho utajiuliza:

Ni kipi kilichokuwa kinakufanya uumie kwa muda wote? Upo huru sasa!
Mapenzi maana yake utulivu wa moyo, yaani wewe na mtu wako spesho muogelee katika dimbwi maalum, ninyi wote mkiwa na amani.

Mkishirikiana katika hali zote. Inakuwa hakuna anayewaza la kwake peke yake isipokuwa kwa ajili yenu.
Ukilia anakuwa wa kwanza kukubembeleza, anapogundua amekuudhi ni mwepesi kukuomba msamaha.
Anasoma mabadiliko yako na kukuuliza kile kinachokusumbua.
Anaficha siri zako, anazungumza lugha tamu na hisia zake zote zipo kwako. Kwa wengine haoni hatamani.

USITHUBUTU KULAZIMISHA PENZI

Yamewafika wengi na wameumia, kwa hiyo ni vizuri kuwa makini.
Utauguza donda la moyo lisiloweza kutibika, utakonda wenzako watakucheka, atakugeuza punda afanye anachokitaka.
Ni kazi bure kumpenda mtu asiyekupenda.
Pamoja na maumivu unayoweza kuyapata lakini kuna vitu hivi lazima vikukute kwa huyo mwenzi wako wa kulazimisha.

ATAKUTESA KWA UBINAFSI WAKE

Hana mapenzi ya kweli na wewe, kwa hiyo si kila wakati atakufikiria.
Kama hamjawa kwenye ndoa itakusumbua kwa sababu ni ngumu kufikiria kwa ajili yenu, isipokuwa atawaza kwa matilaba yake. Kama kuoana, utalazimisha wewe lakini yeye hatokuwa na habari.

Mkiwa kwenye ndoa, hatojisikia fahari kutoka na wewe atalazimisha maisha ya kila mmoja kuwa huru kufanya mambo yake.
Nguo atanunua za kwake na hata siku moja hutoona amekununulia. Wewe utafanya mengi kwa ajili yake lakini yeye atabaki na ubinafsi wake.
Atakutesa, pasha moto ubongo!

AKIONA WENGINE ATAHISI NI WAZURI ZAIDI YAKO!

Mtu huishi kwa fikra zake, kwa hiyo kwa sababu hakupendi kwa moyo wake wote inakuwa ngumu kukukubali, hivyo anapokutana na watu wengine barabarani atadhani ni wazuri kuliko wewe. Atababaika hata mbele yako.

Unahitaji heshima ya kiwango bora na kwa kawaida mpenzi wako anapaswa kukuona wewe ni mtu namba moja.
Kama hakupi nafasi hiyo maana yake anapenda nusunusu au hapendi kabisa.
Usikaribishe mateso, fikiria kesho, chukua uamuzi leo.

HASIFU MUONEKANO WAKO, ANA LAKE KICHWANI!
Hujiulizi, kila siku anakuona na hakusifii! Ni wazi kuwa hata kama wewe ni mzuri kiasi gani, unavaa na kupendeza kwa namna bora kabisa lakini mwenzi wako hawezi kukupa pongezi kwa sababu ana lake kichwani.

Ukiona hilo ujue kwamba yupo mtu ambaye anamsifu kwa sababu ndiye anayemkubali, na wewe utasifiwa na wengine.
Inauma mwenzi wako kukuacha nyumbani na kwenda kumwaga sifa pembeni, wakati na wewe unazihitaji.
Una thamani kubwa, pigania utulivu wa moyo wako!

 
somo hili lina maana kubwa sana hasa kwa vijana wanaokurupukia mapenzi na kujifanya kuwa pesa ndio kila kitu katika mapenzi...
 
Dah MziziMkavu asante sana kwa makala hii nzuri ambayo ina mambo mengi na mafundisho mengi sana kuhusu suala zima la kupenda ambalo kwa wengi hawalielewi na suala zima hata la ndoa ambalo kwa wengine imekuwa ni ndoano
Swala la watu kujaribu mapenzi au kujaribu kama fulani ananipenda au kujaribu kama kweli ndoa ipo na itadumu yapo sana na kuna watu wanaingia tuu kwenye ndoa kwa kuwa imebidi bila kujali kama wako tayari kwa hilo au wana upendo wa dhati
Asante sana mkuu kwa makala nzuri
 
Last edited by a moderator:
HATOKUSIKILIZA IPASAVYO

Mapenzi ni hisia. Ni rahisi kwako kujua kwamba uliyenaye anakupenda kwa dhati mnapokuwa mnazungumza. Je, anakusikiliza kiasi gani?

Mtu ambaye hana mapenzi na wewe, hata umwambie kwa lugha gani hawezi kukuelewa. Tena inawezekana ulizungumza naye jana kwa herufi kubwa, lakini leo jua limechomoza anarudia yale yale.

Inawezekana ulimuonya kuhusu tabia ambazo zinakufanya heshima yake ipotee. Hakatazwi kuwa na marafiki wa jinsia nyingine, lakini mazoea yake siyo mazuri kiasi kwamba wanaweza kutembea barabarani wameshikana viuno. Ikiwa unamueleza habadiliki, huyo hakupendi.

Hakusikilizi kwa sababu hana hisia na wewe.

wengi huwa wanahisia na wewe ila tatizo ni tamaa ya mzee fisi wanataka kula hata visivyoliwa...................
 
Mzizi Mkavu,labda niongezee tu hapo kidogo, kuwa na watu huwa wako serious na wanamaanisha mwanzoni, ila baadaye, wanachange, so wakati mwingine ni ngumu kidogo hata kujua kama mtu hayuko serious, mpaka pale unapoumizwa. Na wengine, wanaweza wakajua moyoni kuwa hakupendi sana, ila, anapretend anakupenda sana, so, kuja kugundua umeshaumia. Mimi ninachosisitza ni kuwa mtu yeyote anayeingia kwenye mahusiano ya mapenzi, ajue kuwa Mungu kwanza, yeye mwenyewe pili, huyo mpenzi ni wa tatu. Na watu wajue wana thamani sana, hata kama mapenzi hayako unavyotamani kuwa.
 
Back
Top Bottom