Heri ukutane na Magufuli kuliko Majaliwa...

Heri ukutane na Magufuli kuliko Majaliwa...

Huyu ni vuvuzela kuliko hata waliopita. Heri hata EL ameacha alama ya shule za kata. Huyu kutwa kumsifia boss wake amefanya nini? Hivi kiongozi anaezunguka nchi nzima kuwambia wananchi mkulu hapendi rusha tafasiri yake yeye anapenda rushwa!! Au anazunguka kuwambia wananchi watumie vizuri pesa za miradi alizotoa rais inamaana hajui kama hizi pesa ni za walipa kodi!!!!
 
Majaliwa kweli anatisha anaanza kukuuliza maswali kama upo interrogation room za kuhoji magaidi , swali kwa swali huku akiwa na details zako zote na bila wewe kujua .

Nimeona watendaji wakitatizika sana na wengi wamepoteza kazi ,kwa sasa ukisikia kuna ziara ya majaliwa unakesha ukisali ila ukisikia jpm tuliza roho ndio maana hata makonda aliomba ziara ya jpm na hawezi kamwe kumuomba PM atembelee dar es salaam

Omba usikutane naye

Nchi ya vilaza bana ina raha kwelikweli, nchi kubwa kama hili unasubiri mpaka rais au waziri mkuu ndio waone wezi? Rais kaua mifumo wamebaki kufanya kama watu ili kusaka kiki za kisiasa.
 
Mshana huwa unasoma word by word. Aisee
Daktari alipoambiwa arudi kazini alikataa kutokana na kudhalilishwa na Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara. Waliendelea na jitihada mbalimbali kumshawishi, sina uhakika kama mwishoni walifanikiwa au waliendelea kugonga mwamba. [emoji109][emoji123]
 
Mtu anaekuja na detail zote za ofisini kwako kuhoji ni hatari sana!
 
Kuna mkurugenzi kapewa siku tatu huko singida arejeshe milioni 109,Majaliwa si wa kukaa nae karibu,unaweza kufa kwa kihoro

Kiki za kijinga tu, utakuta katika hayo maagizo ya kiki wala hakuna utekelezaji wowote utaendelea. Mkoa umejaa Takukuru hawawezi kufanya kazi yao wanasubiri waziri mkuu aje ndio aone huo wizi. Kwa hiyo waziri mkuu asipokwenda huko huo wizi utaendelea tu. Karne ya 21 bado mbinu za kupambana na wizi ni za kama kina Sokoine. Halafu wanaume mmekaa mnashangilia kiki za kitoto.
 
Wakati mwingine kama alisomeshwa na kodi za wa Tanzania ni kunyang'anya cheti cha udaktari akafanye kazi anayoitaka
Sasa ukimnyanga'nya cheti ndio hataweza kufanya kazi sehemu nyingine? Think twice!
 
Yeah...naunga mkono hoja! Majaliwa anakuondoa kwenye reli na sababu unazijua live maana atakuulza maswal magumu ambayo huna majibu nayo na ili hali ulikuwa mtendaji wake, pia ushirika huko mikoani karudisha heshima hawana hamu naye!
 
Daktari alipoambiwa arudi kazini alikataa kutokana na kudhalilishwa na Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara. Waliendelea na jitihada mbalimbali kumshawishi, sina uhakika kama mwishoni walifanikiwa au waliendelea kugonga mwamba. [emoji109][emoji123]
Awamu ya 5 eti tuhuma za mkutanoni zinapewa uzito bila kujua hata undani wake wanajali kupigiwa makofi tuu.
Bora wangechukua tuhuma za JF ambazo huwa ushahidi unapatikana beyond reasonable doubt kutokana na mijadala mikali
 
As if hatuna TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Police na vyombo vingine kama hivi. Ni aibu kila kukicha.
 
Ndio raha ya mkaa kijiweni. Kwao ni bora watu warudi kijiweni ili wawe wengi. Hawakumbuki madhara gani yatawakuta wakiwa level moja. Namnukuu Mh Peter Msigwa; Umaskini hauondoki kwa kumchukia tajiri.
Mnasifia watu wanaoshindwa kujenga mifumo mizuri ya kiutawala kwa maendeleo ya nchi, na badala yake wanajijenga wao wenyewe kisiasa kupitia migongo ya watu wengine, wakiwemo hao watumishi wa umma!
 
Magufuli ana huruma alafu anasamehe kuliko Majaliwa huyu ni moto wa kuotea mbali
 
Mnasifia watu wanaoshindwa kujenga mifumo mizuri ya kiutawala kwa maendeleo ya nchi, na badala yake wanajijenga wao wenyewe kisiasa kupitia migongo ya watu wengine, wakiwemo hao watumishi wa umma!
Jambo hilo ni baya sana. Viongozi Madikteta huwa hawajengi mifumo bali hujijenga binafsi. Ikitokea wameondoka au kuondolewa ghafla, Taifa huwa linaparanganyika. Hayo yalitokea Yugoslavia, Ivory Coast, Iraq, Egypt, Libya, DRC, Burundi, Rwanda, Chile, Romania, n.k.
 
Majaliwa anajitahidi but not yet perfect.

Mtwara aliamuru Daktari bingwa asimamishwe (na hospitali nzima ya mkoa ilikuwa na huyo surgeon mmoja tu) kwa kusikiliza tuhuma za uwongo kutoka kwa mama mkutanoni kuwa daktari alimwomba rushwa ya sh laki 1 ili mgonjwa waje afanyiwe upasuaji wakati laki 1 kilikuwa ni kiasi cha fedha alichotakiwa kulipa hospitalini na siyo kwa daktari.

Kama angekuwa makini angeweza kufahamu kuwa wagonjwa wanatakiwa kilipa nini hospitalini kwa huduma gani. Na hilo angeweza kulipata kutoka menejimenti ya hospitali.

Daktari alipoambiwa arudi kazini alikataa kutokana na kudhalilishwa na Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara. Waliendelea na jitihada mbalimbali kumshawishi, sina uhakika kama mwishoni walifanikiwa au waliendelea kugonga mwamba.
Hahahahahahaha Fort ndiye daktari bingwa?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Fort akasusia kazi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nashngaa kwa sababu sionagi katika mataifa ya jirani na hata ya mbali, wanasiasa wa ngazi za juu wakiwadhalilisha watumishi wa umma. Kwanini Tanzania?
Acheni uwizi, abuse of power na corruption hamtaonewa kama unavyosema..
 
ahsante tindo naanzisha uzi....
Nchi ya vilaza bana ina raha kwelikweli, nchi kubwa kama hili unasubiri mpaka rais au waziri mkuu ndio waone wezi? Rais kaua mifumo wamebaki kufanya kama watu ili kusaka kiki za kisiasa.
 
Back
Top Bottom