Heri tungekuwa na Akili tuikose Elimu

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,991
1,364
1 :Enyi kizazi cha UVIKO mbona mnaufurahia ujinga WA mwenye hekima na kuzishangaa hekima za mjinga? 2:Tangu Leo jueni kwamba kuendelea kumuamini mwenye hekima hata katika maneno ya kupotosha, ni kuhatarisha Maisha yenu wenyewe?
3: Enyi marafiki zangu WA Facebook, ni Nani anayeweza kukaa siku nzima bila kuifikiria SIM yake?
4 :Amin Amin nawaambia haiwezekani Ila Kwa Yule ambaye ni mgonjwa mahututi!
5: Kipato hukuunganisha na watu. Basi uwe mwenye bidii ili ujipatie marafiki wengi na katika hao uwazingatie marafiki wema!
6 :MTU mmoja akauliza Ee Mtumishi mwaminifu nitawezaje kumjua rafiki mwema!
7 :Rafiki mwema ni vigumu kumjua, lakini waweza kuangalia katika SIM yako yule anayehangaika kujua Habari zako yawezekana ndiye!
8: Kuishi vizuri na majirani zako ni kutambua kuwa hakuna aliye na uwezo WA kuchagua jirani!
9 :Mjueni Sana MUNGU, ña kamwe msiwadharau walio karibu na nanyi, kwani hao ndio uwekezaji wenu
10 :Apendaye mshahara apende na KAZI pia, Kwa kuwa mshahara ni matokeo ya kufanya KAZI!
11: Enyi waajiri walipeni wanaowafanyia KAZI Kwa haki, mkijua mshahara usiotosha ni chukizo Kwa Mwajiri Mkuu ambaye haonekani machoni penu!
12:Mkichagua kulalamika mjiandae kulalamikiwa, maana katika kulalamika mnaweza kusahau wajibu wenu!
13:Waacheni watu wawahukumu wapendavyo, Kwa kuwa hukumu Yao haiwezi kubadilisha uhalisi WA jinsi mlivyo!
14: Usichome kitabu Kwa sababu umeshindwa kukielewa!
15: Usivunje daraja bàada ya kuvuka mto!
16 :Maumivu yanayotokana na kumwamini MTU ni makali kuliko kuumizwa na MTU usiyemfahamu
17 :Utachagua kumwamini Nani Kati ya Yule anayeona kisichokuwepo au Yule asiyeona kilichopo?
18: Enyi mnaoishi ndani ya nyumba msiifumbie macho haki inayotendwa na Yule msiyempenda, huku mkiisifia dhuluma inayotendwa na Yule mmpendaye!
19 :Amin Amin nawaambia haki ni haki na dhuluma ni dhuluma. Hakuna haki mbaya wala dhuluma nzuri!
20 :Usikilaumu kioo Kwa uchafu ulionao usoni! Kwa kuwa Kioo hakina uwezo WA kuondoa uchafu usoni mwa MTU!
21 :Nimesikia mmesema aliye Kando haangukiwi na mti,
22 :nami nawaambia Leo mti unaoanguka huenda mbali zaidi ya kimo chake hivyo jihadharini Kwa kuwa kwenu hapo Kando mlipo muda wote
23 :Kwa maana mtego WA panya waliingia waliomo na wasiokuwemo!
24 :Nimesikia pia mkisema Maisha ni kitendawili, nami nawaambia Leo Maisha ya MTU huyapanga mwenyewe
25 :Na atafutaye mambo ya kipuuzi atavuna huo upuuzi na kwake huyo Maisha yatakuwa kitendawili!
26: Hakuna MTU mzuri asiyekuwa na mbaya wake, kama ambavyo hakuna MTU mbaya asipendwa!
27: Mmesikia imesemwa kuwa mjumbe hauawi, lakini Mimi nawaambia mara nyingi Sana wajumbe wameuwa!
28: Basi iweni na busara mnapochagua kuwa wajumbe ili msije kufa kabla hamjakamilisha Ujumbe wenu!
29 :Upatapo fursa ya kuonesha kipaji chako tumia uwezo wako wote 30 :wala usifanye chochote unachoagizwa kufanya Kwa uzembe maana matokeo yake yanaweza kuwa mabaya zaidi kwako kuliko Kwa Yule aliyekuagiza!
31: Ndipo wengi watauliza Kwa nini umesema hivyo? 32 Nami nawajibu Kwa mfano Huu:
33 :MTU mmoja Tajiri aliyekuwa na wafanyakazi wengi WA fani mbalimbali alikuwa pia anamiliki maeneo mengi!
34 :Tajiri alikuwa na kampuni ya ujenzi iliyopata kusifika Sana Kwa sababu ya mhandisi Mtaalamu WA usanifu uliofanya KAZI zake zipendwe Sana katika maeneo mengi ya nchi! 35: Ndipo siku moja injinia huyu akamuarifu Tajiri wake juu ya matarajio yake ya kupata mwenzi WA Maisha!
36:Tajiri alifurahi lakini akataka kumpima injinia wake!
37 :"Nahitaji utembelee viwanja vyangu vilivyopo mjini kisha uchague kimojawapo!
38 :Hapo Ndipo utakapomjengea mteja wangu nyumba ya kifahari Kwa ramani ambayo itakuvutia!
39: Naamini KAZI hii utaifanya Kwa uaminifu na bàada ya KAZI nitaweza kujadili na wewe mipango ya arusi yako". 40: Injinia hakuwa na furaha hata kidogo Kwa sababu alikuwa na usongo aliazimu moyoni mwake kufanya KAZI ya Tajiri wake Kwa haraka ili mipango ya arusi iendelee!
41 :Alifanya uchaguzi WA kiwanja Kwa haraka, kisha akachagua ramani ya nyumba ndogo na nyepesi ili aweze kuijenga Kwa haraka!
42 :Kisha akaanza kupeleka vifaa vya ujenzi vyepesi na vingi vikiwa vya chini ya kiwango!
43 :Hatimaye bàada ya siku chache akarudi Kwa Tajiri ili amkabidhi KAZI yake!
44 :Tajiri alifurahi akapokea ufunguo WA nyumba na Ndipo walipoanza kumpanga mipango ya arusi!
45: Hatimaye siku ya arusi ikafika, na muda WA zawadi ukafika!
46: Tajiri alipopita mbele ya maarusi alikuwa ameshika funguo mkononi!
47 :"Kijana wangu injinia nilikupa KAZI ya kujenga nyumba na nikakuagiza uchague kiwanja kizuri, na ujenge nyumba Kwa ramani nzuri na ya kupendeza Kwa ukubwa uutakao wewe na Kwa gharama zozote!
48 :Nafurahi KAZI hiyo uliikamilisha, nami Niko hapa kukukabidhi funguo za nyumba hiyo kama zawadi yako!
49 :Ghafla USO WA kijana ukaanza kutiririkwa na machozi!
50: Kila MTU katika wageni aliowaalika aliiamini yalikuwa ni machozi ya furaha,
51 :lakini amini nakuambieni yalikuwa machozi ya aibu na huzuni!
52: Nami nawauliza Leo hivi mara ngapi Sisi tumefanya kama huyu kijana mpumbavu?
 
Haya ni maandiahi na yatabakia kuwa maandiahi tu. Uhalisia na maandiahi haya ni mbingu na ardhi.
 
Copy and paste from Facebook..hujaandika wewe usitudanganye
Ndo ma'ana nimeandika heri tungekuwa na Akili Tukakosa elimu!
Umetumia kigezo kipi ukajua mimi ndo nimekopi?Nikukumbushe tu hoja yako ingeonekana ina mashiko ikiwa ungesema huu uzi ni wako( wewe ndo umeuandika)! Jamiiforum facebook nyoteni mitandao ya kijamii
 
Copy and paste from Facebook..hujaandika wewe usitudanganye
Heri kukosa elimu ukapata akili! Sasa wewe umetumia kigezo kipi ukajua aliyeandika fb na aliyeandika jf ni watu tofauti?
2: umetumia kipimo gani kujua mimi ndo nimekopi na kupesti?
3: ingependeza ikiwa ungeonesha chanzo sahihi cha huu uzi! Ili kuthibitisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom