Heri dhahabu kuliko uhai wa Wana Tarime | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heri dhahabu kuliko uhai wa Wana Tarime

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Prodigal Son, Feb 22, 2010.

 1. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Inasikitisha na inauma jinsi wenye mamlaka wanavyojali PESA kiliko roho za watu, jAMANI WATU WANAKUFA, MIFUGO INAKUFA MAJI YA KUNJWA YAMECHAFULIWA HAKUNA ANAYEJALI????NDO NGUVU YA PESA?????

  maji yenye kemikali yaliyovuja kutoka kwenye mgodi wa North Mara madhara yake kwa wananchi ni makubwa tena saana, Roho inaniuma jinsi ambavyo hawa wenye mamlaka wanavyolishughulikia hili tatizo, kwa kuwa wenye mgodi wanauhusiano mzri na watawala inaonekana ni halali hao wana tarime waendelee kufa, Reginald Mengi alipokuwa boss wa NEMC walienda Japan wakajionea mdahara ya madini ya zebaki yanayotumika kwenye hiyo migodi aliporudi aliionya serekali hakuna kilichofanyika, sasa hivi roho za wananchi wa tarime zinateketea hakuna anayejali kinachotafutwa ni ushahidi wa kitaalamu wakati hata kwa macho mdhara ya hizo kemikali yanaonekana

  Watanzania Wenzangu
  Watu wameadhirika wengine wamekufa, mifugo imekufa hakuna anayejali, wawekezaji wanasikilizwa kuliko wananchi, nimeshuhudia kwa macho madhara ya hiyo kemikali INASIKITISHA

  TAFAKARI
  Hii serekali ipo kwa ajili ya nani????kama dhahabu ni rasilimali Mungu aliyotujalia ni kwanini itumike kutuuwa? wako wapi wanaojiita wanaharakati??

  Mlio nje ya Tanzania hamuwezi hata kusaidia ili wamiliki wa huu mgodi washakiwe kwenye mahakama za kimataifa?????

  Viongozi wa CCM na serekali yenu mbona mmewasaliti wananchi Hivyo???KUMBUKENI SIKU YA HUKUMU KUANZAI KWA RAISI NA WANAOMZUNGUKA WOTE MTAULIZWA
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,018
  Likes Received: 37,328
  Trophy Points: 280
  Hii ndio Tanzania yetu. Punda afe mzigo ufike.
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Neno zito sana, ndo hali halisi lakini
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Linashughulikiwa nimeonana na mtu personaly ambaye alienda Mara kwa kutatua hilo tatizo yeye anatokea kampuni ya SRK

  All in all maamuzi yote ya project yoyote inatakiwa kufanywa na wananchi husika wa hilo eneo!

  Nimekuwa nikisema Kakobe anatoa somo kali sana kati yake na Tanesco, na watu wamekuwa wagumu kujua ni same story inayotokea kwenye hiyo migodi.

  Nchi ndiyo iko hivyo kila kitu kinafanywa kana kwamba watu wa hayo maeneo ni wanyama, wakati mwingine na sisi humu tumekuwa tukiwapa vichwa hawa watendaji kufanya lolote lile , kwa misemo ile ile ;;;;;;;;zidumu fikra za mwenyekiti;;;;;;
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,629
  Likes Received: 23,793
  Trophy Points: 280
  Pole Prodigal Son, usiumie, ndio Tanzania yetu hii.
  North Mara waliweka makinga maji kuzuia sumu isivuje, wananchi wakayaiba hayo makinga maji, kwenda kuezekea, nani wa kulaumiwa?.

  North Mara wameanzinza mgodi bila EIA, hayo ndio matokeo, nani wa kulaumiwa?.

  Kamati ya bunge nayo imefanya uchunguzi, wakakuta hakuna uhusiano kati ya North Mara na waathirika, jee nani alaumiwe?.

  Hao wanaokufa, wanafia nyumbani na kuzikwa bila kwenda hospitali, hiyo mifugo inakufa na kufukiwa bila uchunguzi wa chanzo cha vifo, wabunge wetu wenyewe wameshindwa kuthibitisha, sasa nani alaumiwe?.

  Siku zote penye uzia, penyeza rupia, kuanzia serikali ya kijiji, ya wilaya, serikali kuu mpaka sasa na wabunge, wametulizwa, North Mara inaendelea kupeta, kwao hao wanaokufa wanathamani kama ile dhahabu?.

  Hata wasipokufa serikali inapata faida gani kwa watu hao, jee wanapokufa serikali kwani serikali inapata hasara yoyote?.

  Hebu fikiria mwenyewe jinsi dhahabu ilivyo muhimu, yaani inaleta mapesa kedekede, hata ikibidi watu wa vijiji vyote vinavyozunguka North Mara wafe, serikali iendelee kujipatia huo mrahaba wa asilimia 0.03!.

  Halafu October ndio hiyo inakuja, na tutaendelea nao, na tutawachagua tena, na tena na tena! .

  Mungu Ibariki Tanzania!.
   
 6. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Pasco,
  Hivi Mwaka 2009 ndo tumejua kuwa hawa jamaa hawana EMP? MEM should be blamed.

  Isitoshe hawa wataalam wetu ndo akina nani? Watalaam wa kuwatafutia wazungu leseni? Wafanye biashara bila kikwazo, ili ulinde mkate wa kesho TU?
   
 7. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Mkuu PASCO

  kuna tofauti kubwa saana kati ya kuona kwa macho na kusoma au kuona kwenye TV na kusikia kwenye redio au kusoma kwenye gazeti,

  Inasikitisha inasikitisha tena saana tunaomwamini Mungu tunajua hii ni laana kwa nji

  Kama hayo makaratasi yaliibwa ni wnanchi wote waliiba? Si kuna polisi kwanini wazi wasingetafutwa wapelekwe kenye vyombo vya sheria???
  uchunguzi uchunguzi wakati watu mameshakufa na wengine wanakufa? Mifugo inakufa, Nini juhudi za maksudi zilichukuliwa kuzuia tatizo? na kama mgodi ulichukua hatua gani kulinda hayo mabwawa yake dhidi ya wezi?? Ni maswali mengi ambayo watoa maamuzi wetu mbele ya haki lazima watatakiwa watoe majibu tea ya kina

  Watoa maamuzi wala msichoke kuwafurahisha WAWEKEZAJI ila ila tambueni hii laana itawatafuna vizazi vyenu milele hata milele.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...