Nchi imeshakuwa addicted na uongo. Tanzania kila kiongozi ni mwongo. Maisha ya kila siku yanaendeshwa kwa kudanganyadanganya tu imefikia pahala ukweli unageuka uongo and vice versa. Siku hizi utaonekana mwongo ukisema kulikuwa na ahadi kama vile maisha bora kwa kila mbongo, reli ya kasi Dar to Mwanza and Kigoma, ajira zaidi ya milioni moja (eti watasema imetimizwa kwa kuongezeka bar kumeleta ajira za mabaa maid na wachoma chips)
Ni uongo pia ukisema kuna series ya kauli nbiu kama nguvu mpya, ari mpya na okasi mpya wakati majirani zetu wanatupima na kuona tupo nyoronyoro hadi wanaamua kututenga, utakuwa mwongo pia ukisema kina kauli kama kilimo kwanza, tena ikaja matokeo makubwa sasa.
Na hizi nazo? Watanzania wanaweza kuwekeza kwenye juice na soda, asiyeweza kulipa feri apige mbizi, wapinzani wanafuata juice ikulu, nk..