Henry Matata: Dr. Slaa mwongo no. 1 duniani

Ichaguzi ujao hatutakuwa na nafasi ya vichaa kwenye chama, wagombea hata wa udiwani ndani ya Chadema watakuwa wengi na watateuliwa wenye akili timamu tu
 
Mwongo namba 1 duniani? loh

Yaani kwa maneno mepesi ni kuwa ukichukua waongo wote duniani mchumba wa josephine anaongoza kwa uongo.

hili neno kubwa sana! mtake radhi slaa.

usiwe unaandika vitu as if umeshikishwa ukuta ***** wewe..mbona mchumba wa mama yako humtaki radhi
 
Mi naamini kabisa mabadiliko ya nchi hii mungu yupo nyuma yake, sasa je ni nani mwenye uwezo wa kuepusha mabadiliko hayo, lazima huyo aende na maji 2.
 
Huyo matata na Dr.slaa wanamengi yapo nyuma ya pazia..Ukiona pnafuka moshi ujue pana moto.
 
Mnyonge Mnyongeni lakini Haki yake........

Jamani kata ya Kitangiri iliyo chini ya Matata matunda yanaonekana leo Kigari changu kidogo (Carina) ninaweza kupanda nayo Milimani barabara ya kwenda Jiwe kuu sasa hivi inapitika bila shida. Pia barabara ya kwenda Milimani mpaka Ziwani (Mihama) pia yapitika bila tabu na hivi alikuwa na mpango wa kufufua barabara ya Matauro

Ahhh Chungu lakini.......
 
Chadema itaendelea kuwapima na kuwachuja wale wote ambao ni pandikizi la CCM au wenye tamaa na uchu wa madaraka kwa manufaa yao wenyewe. Kauli ya Bw. Matata ni kauli ya mwendawazimu.
 
Anafanya kile kilchotarajiwa na wengi.Tatizo alilonalo ni tabia yake ya kutopanga hoja zake kimtitiriko.Kama akifanikiwa kuzipanga hoja zake mimi naamini atafanikiwa kisaidia CCM.Go on mstahiki.
 
mtoa uzi huu, kwanza ungeweka ushabiki wako pembeni, kisha utuabarishe vzr aliyosema meya. nasi tupate nafasi ya kuukubali / kuukataa usemi huo wa,,,,,,,,,,,,, no 1 duniani . vinginevyo tukishindwa sisi basi mwenyewe mlengwa atusithibitishie vinginevyo.
 
Henry Matata...?! Mla rushwa, Mamluki na ......utoto wa maisha unamsumbua huyu...

 
Huyo mtu ni dhahiri yuko frustrated. Na sijui MEDIA zinapowaita watu walio out of mind zinategemea nini kama si matumizi mabaya ya airtime!

Ninategemea sasa ni wakati wa vyombo vya habari kuonyesa ukomavu na kufnya kazi yake ya kujenga nchi kwa kumaanisha. Tafuta watu ambao ni competitive and constructive ili watoe taarifa za manufaa na ujenzi wa taifa linalopumulia mashine. Acha ushabiki wa kisiasa kwa kushadadia ujinga usio na tija kwa yeyote. Wapo watu sahihi wenye uelewa na uwezo wa kuchambua hoja kwa mitazamo tofauti na wasikilizaji wakapata manufaa.

Sasa watu kama matat unawaweka ili nini?
 
Chadema inabidi ijipange sana kuchuja wagombea katika hatua za awali ndani ya chama ili watu ambao wa akili kama hizi wasifikie hapo walipofika
 

Mkuu mbona maelezo yanaeleweka sana, kweli umeshindwa kufahamu ufinyu wa akili wa huyo diwani katika hata majibizano ya simu na mpiga kura wake aliyekua anataka kumuuliza swali.Ama ni ushabiki wako ambao unashindwa kuelewa maelezo ambayo yanaeleweka hata kwa mtu ambaye hana elimu ya darasani?
 
Apimwe akili mnaweza jikuta mnapoteza muda wenu bure
 
Kwanini asiseme Pinda ndo mwongo namba moja maana ndiye aliyedanganya Bunge mpaka hoja ya Lema ikazimwa
 
Huyu Bw. anaeitwa Henry Matata sio mzima hata kidogo. Mara ya kwanza kumwona ilikuwa kwenye harambee ya kuchangia Kanisa hapa Pasiansi na mgeni rasmi alikuwa Mhe. Waziri Mkuu. Jamaa alibehave kihuni sana. Wanaomfaham wanasema anafujo sana na anarekodi ya kuwai kuwa mhalifu sana (jambazi). Tatizo CDM inakomba kila aina ya mtu ilimladi anataka kugombea uongozi. matokeo yake ndo haya. Ila huu upinzani wa CCM na CDM hapa Mwanza utarudisha maendeleo nyuma. Nashangaa sana waliomchagua kuwa meya, sijui walitumia akili gani kati ya kwenye visigino na makalio?!! Hapa ndo ninapoichukia siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…