Naomba msaada kwa wataalaamu wa Kiswahili,
Ni kwamba hawa jamaa wa ndege zenye kutoza nauli ya mabasi (sina uhakika sijathibitisha hilo) yaani Fast jet wana mabango yao yanayosomeka "Hembu tupae....." Kama nilimuelewa vizuri mwalimu wangu wa Kiswahili, katika lugha sanifu haya maneno yalipaswa kusoma "Embu tupae....." Nawaombeni msaada kipi ni sahihi ili kama hawa jamaa wamechemka warekebishe kwani inakera sana kuwa na bango kubwa kama ghorofa halafu lugha imekosewa hasa kama unalazimika kuliona hilo bango angalau mara mbili kwa siku kama mimi.
Ahsanteni sana wadau!

Nimerudi wakuu. EBU na hebu haya yoe yapo kwenye kamusi na yana maana mmoja.
EBU na HEBU ni maneno sahihi.:target:
Kinaathiri nini kwenye suala zima la usafiri,binafsi mimi nawapa, Bg Up,mbona matangazo ya TANESCO yote ni mazuri na yanapendeza.
TAFAKARI :confused2:
Sio Hembu wala Embu. Ni Ebu.
Kwa kuongezea HEBU ndio sahihi ila kimatamshi HEBU hua ni rahic kutamkika kama EBU
Pmwasyoke kama umechemka vile!!? Hicho labda umesema Kinyakyusa, maana hata kwenye Kisukuma hatuna EBU!!!. Jibu sahihi ni "HEBU"
Wakati mwingine kukosea spelling hufanywa kwa makusudi kwenye matangazo ili msomaje aweze kulikumbuka tangazo na kuliweka kichwani. Kikubwa zaidi huwa inasaidia hata mtu mmoja akisoma tagazo aweze kulibeba ili akawatangazie wengine kama ambavyo mtoa mada.
Kwa mfano, mimi niko mbali na sijaliona tangazo la fastjet, lakini wewe umeshanitangazai. So, they know the language na wala hawajakosea kama unavyofikiria. Wamefanya hivyo kwa makusudi!
Lakini pamoja na kutojua kwao lugha ya kiswahili au kujua kwao lugha kulikopitiliza bado usafiri wao wa ndege wanatoza nauli za mabasi,hilo ndio swali la kujiuliza je;wanapata faida?.Hilo ndio swali la msingi.