JADILI KWANZA ILIKUWAJE WAKAHAMA HUKO WALIPOKUWA na urekebishe hayo ili waweze kurudi kwa kuona ubaya wa uislam, tuondolee hizi hadithi zako za abunuwasi humu
Hapa naunga mkono kabisa.
Wakristo wengi wenye ndugu zao ambao wameingia kwenye Uislam, kwa hiari yao, huwa wanakataa kukubali kwamba ndugu zao hao - wa kike au wa kiume - wameingia kwa hiari yao, wanaona kwamba WALILAZIMISHWA.
Tujiulize:
1) Kuna ushahidi wowote kwamba huko ambako Wakristo hao wa zamani wamenyanyashwa au kudhalilishwa, kwa kuwa tu wamekuwa Waislam?
2) Je, kuna ushahidi wowote kwamba hao waliokuwa Wakristo wamelalamika kwamba wamedhalilishwa au kudhulumiwa haki zao?
Hapa duniani maisha ni mafupi kabisa. Kama mtu amechagua kuwa na imani yake, basi, abakie na imani yake, na kama mtu anataka kubadili imani yake, abadili na asitishwe.
Yapo mambo mengi ambayo Uislam umepotoshwa juu yake, kwa mfano:
1) Nchini Marekani, watu wengi - licha ya Obama kuitwa Barack Hussein Obama (na katika kuapishwa kwake aliapa kwa jina hilo...) - wanaamini kwamba WAISLAM WOTE ni magaidi.
2) Hapa nchini, baadhi ya madhehebu (ingawa neno hili si sahihi...) ya Kikristo huwafundisha (nje ya 'katekista') kwamba Waislam ni watu wabaya, wasiomcha Mungu, washirikina, wenye "kufuga majini", na kadhalika...
Nauliza:
1) Wapi kwenye Quran imeandikwa kwamba ukiwa Muislam shurti uwe mshirikina au ufuge majini?
2) Kuna ushahidi gani kwamba ni Waislam pekee wenye kufuga majini?
Pale ambapo sisi wote tutakapotambua kwamba, (1) Mungu habagui, (2) Mungu hajasema kuna dini iliyo bora zaidi ya yule kwenye Kuamini pekee, na (3) kwamba Siku ya Hukumu kila mtu atahukumiwa kwa "matendo yake" peke yake, na hatokuwa na fursa ya kusema, "nilifanya hivi kwa ajili ya kumfuata fulani..." basi siku hiyo itakuwa ya FURAHA KUU!
Wanadam, kumbukeni, kila unachokisema, kibaya, juu ya IMANI ya mwenzako, Mungu anakuhukumu kwa hilo. Malaika wako wanaandika rekodi yako, matendo mema upande wa kulia, mabaya upande wa kushoto. Siku ya Hukumu (Al Qiyama), mizania yako ya kushoto ikiwa nzito kuliko ya kulia, njia yako ni motoni tu... hutauona mlango wa pepo.
Unayejiita "Mwana wa Mungu", rekebisha kauli yako, tubia makosa yako.... Ni Amri ipi ya Mungu inayosema "usimshuhudie jirani yako uongo"?
Nimezaliwa Muislam, sioni haya kuitwa Muislam, na katu sitaacha kuwa Muislam. Ukiona Uislam unapigwa vita mbele, nyumba, kushoto na kulia, basi ujue kwamba HIYO NDIYO NJIA SAHIHI ZAIDI ya KUMCHA MUNGU!
"Mwana wa Mungu", tafuta Quran uisome, ujue Mungu anakuambia nini, kabla ya kubwatuka na kashfa za rejareja, unajichulia dhambi kwa maneno yako ya UONGO!
./Mwana wa Haki
P.S. Hao dada zako "wanawajua" majini kweli, wanayolazimishwa kuyafuga? Au unawashuhudia..... ?