The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 19,254
- 42,873
Mkuu Chige asante kwa ufafanuzi wako! Mie sio mtaalamu wa mambo ya banking hivyo bado nina duku duku la kujuzwa zaidi - kwa mazingira yetu ya Tanzania hivi transfer ya kiwango kikubwa hivyo cha fedha kwa mara moja haipaswi ku-arouse interest ya kila mhusika kuanzia kwenye Branch mpaka HQ kutaka kumjua huyo "Mteja"?
Hiyo ni lazima mkuu, tena kuna benki zingine wana daftari la kurekodi mialama yote mikubwa kulingana na mwenendo wa mteja, kama Samaritan amezoea kuja kutoa vilaki 1 mara elfu 80, siku zingine 150,000/=, siku akija kutoa hata 3,000,000/= tu italeta utofauti na huenda akauluzwa hela imetoka wapi. huo ni mfano tu kuhusu swali lako. Nimewahi shuhudia mabenki wakipeleka daftari la miamala wanaiita high value pamoja na withdrawal receipts kusainiwa kwa meneja ili kujiridhisha na huo muamala. Ila kwenye hili ulishaambiwa serikali ilipigwa ganzi/ili paralyze mkuu. Watu walikua wanafuata oder tu!
Last edited by a moderator: