Pesa za ESCROW zilikuwa za umma ama watu binafsi???

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
1,758
2,000
“Tusijipe usahaulifu wa lazima tena kwa haraka.., zile pesa zilikuwa za UMMA au za WATU BINAFSI.., zile pesa za TEGETA - ESCROW Account... NANI ANAWALIPA SCB-HK DENI LAO!?”

Martin Maranja Masese [MMM]

.., hivi zile pesa zilizofunguliwa TEGETA - ESCROW Account zilikiwa mali ya UMMA au zilikuwa pesa za watu binafsi!!? Hivi ule mjadala unaukumbuka kweli!? Ok..., tuliambiwa ni pesa za watu binafsi..., ila kuna kodi ya serikali tu.., sawa..., (kumbukumbu zangu bado ziko salama sana)...

Tangu mwanzo, ukifuatilia kwa ukaribu sana sakata hili.., utaona harufu ya wizi, rushwa, ubadhirifu na ufisadi uliokomaa.. Lakini mamlaka zinazohusika zilijitahidi kukanusha kwa juhudi kubwa sana.., ukitazama hata namna PAP walivyonunua hisa zao.., PAP walinunua hisa za PIPAL LINK huku kukiwa na amri ya mahakama ya kutouza hisa,.. Hata uchunguzi wa kimahakama kuhusy uuzwaji (haswa bei za hisa) haujatoka hadi leo..

Hivi unafahamu kwamba pesa zile ambazo watu walikuwa wanagawana kama 'peremende' kwenye sandarusi na magunia ziliishi kwenye akaunti ile kwa miaka takribani 7!!??

Tarehe 5.7.2006 ndiyo rasmi akaunti hii ya Tegeta ESCROW ilifunguliwa na kufungwa rasmi 5.9.2013 na kuamriwa shughuli zote za TANESCO zikabidhiwe kwa IPTL... akaunti hiyo ilifunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka fedha za tozo ya uwekezaji, ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao, pande hizo ni (TANESCO na IPTL)..

Wakati wa UKAGUZI wa awali wa akaunti hiyo chini ya CAG.., alikuta 202. 9bilioni fedha za kitanzania.... Inasemekana kwamba kama TANESCO wangelipa tozo ya uwekezaji akaunti hiyo ya TEGETA ESCROW ingelikuwa na shilingi bilioni 307/-, hivyo kutokana na TANESCO kutolipa tozo hiyo, ilibaki na madeni yenye thamami ya US$33.6billions.. (yaani dola za kimarekani bilioni thelathini na tatu nukta 6)..

Awali ilitamkwa kuwepo kwa kodi ya serikali katika fedha hizo (ambazo zilikuwepo katika akaunti hiyo) kodi hiyo ikiwa ni bilioni 21. 7 (bilioni ishirini na moja na milioni mia saba)..., taarifa iliyokanushwa na Kikwete na kusema UKAGUZI wa CAG haukuonyesha lolote kwamba pesa zile ni mali ya umma..

...., Wizara ya nishati na madini (chini ya Prof Sospeter Muhongo) waliamua kuomba ushauri kwa mwanasheria mkuu juu ya pesa, AG (attorney General) ambaye alielekeza kuwa pesa zilipwe kama mahakama ilivyotaka, benki kuu waliuliza maswali haya, na AG akaelekeza walipe kwa PAP na hakuna kodi, ushauri wa AG uliitoa nafasi ya akaunti kufungwa na kugawanywa rasmi na baadae kuingia barabarani.

Kabla sijaanza kukumbushia kauli za Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu sakata hili.., nipende kuuliza tu.., je, mapendekezo ya CAG kwenye taarifa yake, yalifika kwenye dawati la TAKUKURU!? binafsi ningependa kufahamu hatua zilizochukuliwa na TAKUKURU...

Vipi kuhusu wale waliomegemewa pesa na RUGEMALIRA!!? Tena baadhi wakiwa watumishi wa umma!!? TAKUKURU na tume ya maadili ya watumishi wa umma walisema wanachunguza na kushughulika na watumishi wa umma wote waliopewa pesa, na pia tume ya maadili ya umma iliwahoji wote waliopewa pesa... (matokeo yake yalisomwa wapi, au mwisho ni kuwahoji na kuwaacha waende zao bila kuujulisha umma!?)

Maamuzi yote yaliyofanyika yalifanyika kwa maelekezo ya mwanasheria mkuu (AG), uamuzi huu wa mwanasheria mkuu wa serikali uliibua mjadala mkubwa sana, na hata watu, wananchi wengi kuanza kuhusi kuwa kuna rushwa kubwa, watu wamemegewa mshiko, kila mtu kuongea analofahamu!

OK...., tuendelee sasa..,

..., labda niwakumbushe tu ambayo mheshimiwa Rais wa wakati huo (Jakaya Mrisho Kikwete) aliyosema kuhusu sakata hilo (siku anaongea na wazee wa DSM katika ukumbi wa Diamond Jubilee)...

> Kikwete alisema kwamba., kutoka na hali ya mgogoro ulivyokuwa pesa zilizokuwa ndani ya akaunti ya ESCROW SIYO PESA ZA UMMA BALI NI ZA IPTL kwani ndiye mlipwaji kutokana na madeni ambayo IPTL inaidai TANESCO kutokana na tozo za uwekezaji.

> Kikwete pia alisema, kama TANESCO wangeshinda keai ya mgogoro wao na IPTL basi pesa hizo zingekuwa mali ya UMMA kama ilivyokuwa kwenye kesi yao ya mwaka 2001, lakini kwa sababu TANESCO walishindwa, pesa hizo ni za IPTL na siyo UMMA (PUBLIC)

> Kikwete pia alisema PAP walipelekewa deni la kodi ya serikali, akasema CAG alikagua na kusema pesa zilizokuwemo kwenye akaunti ya ESCROW hazikuwa na SIFA ZA KUITWA PESA ZA UMMA.

> Kikwete alisema, serikali haikupata hasara yoyote Kutokana na sakata hilo la ESCROW..

> Kikwete akatengua uteuzi wa Profesa Tibaijuka, kwa Kukubali kuwekewa pesa kwenye akaunti yake binafsi huku akiwa ni mtumishi wa umma...

> Kikwete akaamua kumweka kiporo Prof Sospeter Muhongo (licha ya kuatajwa na kamati ya PAC) akisema uchunguzi kuhusu Muhongo bado haukakamilika.., akipata majibu atatoa maamuzi..

> Bunge kupitia kamati yake ya PAC chini ya Zitto Kabwe likatoa na kuridhia mapendekezo yake..., Kikwete akayapinga na kupangua baadhi ya mapendekezo!

> Kikwete akasema, wabunge wa CCM na chama hicho kwa ujumla wake, kilikuwa imara kwenye sakata hilo.., na hakijayumbishwa kamwe!

> Kikwete akawataka wabunge, wanachama, wapenzi na viongozi wa CCM wakawaambie wananchi mitaani kuhusu ESCROW (kama ambavyo wapinzani wamekuwa wakifanya wakati huo)..

> Kikwete pia alikanusha kuwa kufungwa kwa akaunti ya Tegeta - ESCROW hakukuwa na msukumo kutoka kwa maafisa wa serikali, alisema serikali ilifanya juhudi kubwa kwenye sakata hilo..

> pia akasema, mwanasheria mkuu (Francis Werema) alimwambia hakukuwa na makosa yeyote kwenye maamuzi ya mahakama, na pia hakuna hasara ambayo serikali imepata kutokana na sakata hilo la ECSROW kwa sababu pesa hizo zilikuwa ni deni ambalo TANESCO ilikuwa inadaiwa na IPTL.

> pia Kikwete alisema kwamba, Rugemalira alilipa kodi aliyokuwa anadaiwa kiasi cha shilingi Bilioni 38, kwa muktadha huo, RUGEMALIRA hana makosa kwenye hili, alilipa kodi zote.

> Kikwete pia alisema fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta ESCROW hazikuwa zinafikia Sh306 bilioni, bali ni Sh202 bilioni na zilikuwa mali ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.

Hizo ni baadhi ya kauli za aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika awamu ya 4 ya 2005-2015, mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.. (tumetunza kumbukumbu hizi kwenye maktaba zetu ipasavyo)..

Kwa mujibu wa mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mwenyewe pale Diamond Jubilee alisema kwamba.., tarehe 15.9.2013 mahakama kuu ya Tanzania ulifanya uamuzi wa maombi ya kampuni ya VIP kuomba kusimamisha mchakato wa kuuza hiza za IPTL wakilumbana juu ya hisa, uamuzi wa mahakama ulikuwa PAP wapewe hisa 30% na wakanunua 70% na waliandikisha hisa 70% BRELA,

.., Kikwete pia alinukuliwa akisemw kwamba, mahakama iliamua hisa zikabidhiwe PAP ambao ndiyo mmiliki halali wa IPTL., Uamuzi huo wa mahakama ulimaanisha kuwa PAP wanatakiwa kumiliki mpaka pesa za ESCROW kwa PAP, uamauzi ambao ulizua malumbano serikalini juu ya akaunti ifungwe au isifungwe, pesa zitoke au zisitoke...

Katika moja ya mapendekezo ya kamati ya PAC kuhusu sakata la ESCROW.., iliitaka serikali iandae na kuwasilisha marekebisho ya sheria ya uundwaji na namna ya kushughulikia na rushwa kubwa, kimsingi hilo lilikuwa ni moja pa pendekezo bora sana.., hadi leo wizara ya katiba na sheria sijafahamu kama imekwisha kufanya hivyo....., kuna taarifa ziliwahi kuzuka kwamba, serikali imekuwa inaifanyia marekebisho taasisi ya kuzuia rushwa tangu mwaka 2008.., (sijaona mabadiliko hayo ya kimantiki)...

Mapendekezo karibu yote hayajafanyiwa kazi... (binafsi nayakumbuka kwa uzuri sana).., baadhi ni kama...

(i) kuundwa kwa tume ya kijaji kuwachunguza majaji waliohusika na sakata la ESCROW..

(ii) PCCB yaani TAKUKURU, na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vichukue hatua kwa watu waliotajwa.

(iii) Mamlaka husika za kifedha na kiuchunguzi ziitaje STANBIC-TANZANIA na benki zilizohusika katika sakata hilo, zitangazwe kuwa taasisi zinazotakatisha fedha..

(iv) kuwavua nafasi za kiutumishi, watumishi wa umma wakiwemo mawaziri waliotajwa na pia kuivunja bodi ya TANESCO...

(v) kutaifisha mitambo ya IPTL, ambayo inatajwa kununuliwa kwa njia zisizo rasmi na kwa ujanja mwingi...

(vi) uwazi mkubwa wa mikataba haswa ile mikataba inayogusa maslahi ya wananchi moja kwa moja.., pia kupitia mikataba yote.., bila kuathiri kanuni za usiri wa mikataba (usiri wa mikataba (company secret)

HITIMISHO: TANESCO IMESHINDWA kesi yake dhidi ya IPTL (Independent Power Tanzania Limited). Pia TANESCO imeamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320..., TANESCO sasa wanatakiwa kuilipa benki ya Standard Chartered Bank-Hong Kong (SCB-HK) US$148.4M (zaidi ya Sh. bilioni 320 za kitanzania).

Hivyo tunajikita kujiuliza maswali yenye mantiki sasa...., nani atalipa deni hilo la IPTL la zaidi ya shilingi bilioni 320!? UMMA au WATU BINAFSI!? sitegemei fedha za makusanyo ya ndani zitumike kulipa deni hilo wakati awali mlitushirikisha kusujudu na kusema kwa sauti kwamba PESA ZILE HAZIKUWA NA CHEMBE CHEMBE ZA KUWA ZA UMMA...

niseme sasa, imetosha.., nisije kufika sehemu isiyo salama sana kwa sababu ya kuandika hata yale msiyopenda kuruhusu macho yenu yatazame na kusoma pia kuelewa...

Martin Maranja Masese
Mwananchi wa kawaida
martinchizzle@gmail.com
 

KING DUBU

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
893
1,000
Mhh! Amesema Waliostaafu wasiguswe wala kujadiliwa wakati dili zinaonekana zimechipuka huko.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,745
2,000
Fedha za Escrow hazikuwa Fedha za Umma!

CAG katika Report yake aliwakosoa Tanesco kwa kuonesha Account ya Escrow Kama ni Asset ya Tanesco

Account ya Tegeta Escrow ilikuwa na kazi ya kuhifadhi Fedha ambazo Tanesco wanailipa IPTL, iweje Fedha unayolipa kwa Mtoa Huduma igeuke kuwa yako kwa kuwa tu watoe Huduma wana ugomvi uliopelekea Fedha Yao ihifadhiwe mpaka Kesi Yao itakapokwisha!

Watu wajifunze kwanza maana ya Escrow Account na ni wakat gani hulazimika kufungua Account ya namna hiyo

Kwanini Tanesco waliamua kuweka 'hela' zao kwny Escrow Account?
 

ikipendaroho

JF-Expert Member
Jul 26, 2015
3,632
2,000
Zile Noah sasa naona zitakabidhiwa kwetu zimetiwa sport rims kwa speed hii ya kukamata wahujumu uchumi.
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,942
2,000
Fedha za Escrow hazikuwa Fedha za Umma!

CAG katika Report yake aliwakosoa Tanesco kwa kuonesha Account ya Escrow Kama ni Asset ya Tanesco

Account ya Tegeta Escrow ilikuwa na kazi ya kuhifadhi Fedha ambazo Tanesco wanailipa IPTL, iweje Fedha unayolipa kwa Mtoa Huduma igeuke kuwa yako kwa kuwa tu watoe Huduma wana ugomvi uliopelekea Fedha Yao ihifadhiwe mpaka Kesi Yao itakapokwisha!

Watu wajifunze kwanza maana ya Escrow Account na ni wakat gani hulazimika kufungua Account ya namna hiyo

Kwanini Tanesco waliamua kuweka 'hela' zao kwny Escrow Account?
Sasa mkuu ulishaambiwa Tanesco walilalamika kuwa walikuwa wanakuwa overcharged kimakosa kwenye capacity charges sasa kma mahakama ikakubali kuwa Tanesco ilikuwa overcharged kimakosa sasa ile balance ya TANESCO kivp yote ichukuliwe na hao PAP/IPTL ??? Hakuna aliesema pesa zote zilizokuwemo ni za UMMA ila tunachosema ni kuwa kwenye ile account kulikuwa na pesa za umma ambazo ilibidi Tanesco walipwe !!!!

Haya wakasema pesa sio za umma?? Je ile kodi ya bilion 21 nayo ni ya mtu binafsi?? Hyo tu ilitosha kuwanyoosha hawa jamaaa

Nashangaa mkuu watetea... ssa hta kwa reasoning ya kawaida tu kma pesa ni zako binafsi kivp ugawe kma njugu kwa vigogo wa serikali?? Katibu wa rais alipewa mgao kma nani?? walikuwa na urafiki gani hasa na chenge au ngeleja??? Kwanni asitoe kwa watoto yatima ila ametoa kwa vigogo wenye ushawishi???

Mkuu fikiri mara mbili
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,745
2,000
Sasa mkuu ulishaambiwa Tanesco walilalamika kuwa walikuwa wanakuwa overcharged kimakosa kwenye capacity charges sasa kma mahakama ikakubali kuwa Tanesco ilikuwa overcharged kimakosa sasa ile balance ya TANESCO kivp yote ichukuliwe na hao PAP/IPTL ??? Hakuna aliesema pesa zote zilizokuwemo ni za UMMA ila tunachosema ni kuwa kwenye ile account kulikuwa na pesa za umma ambazo ilibidi Tanesco walipwe !!!!

Haya wakasema pesa sio za umma?? Je ile kodi ya bilion 21 nayo ni ya mtu binafsi?? Hyo tu ilitosha kuwanyoosha hawa jamaaa

Nashangaa mkuu watetea... ssa hta kwa reasoning ya kawaida tu kma pesa ni zako binafsi kivp ugawe kma njugu kwa vigogo wa serikali?? Katibu wa rais alipewa mgao kma nani?? walikuwa na urafiki gani hasa na chenge au ngeleja??? Kwanni asitoe kwa watoto yatima ila ametoa kwa vigogo wenye ushawishi???

Mkuu fikiri mara mbili


Hayo unayoongea yana Mantiki kwny Mijadala ya Kisiasa sio kwny Chember za Mahakama!

Mwenye Fedha Ana Uhuru wa kuchagua AMPE Nani Fedha na kwa Malengo yapi, Miongoni Mwa 'Waliohongwa' Wapo Maaskofu jee nao Walihongwa ili kuruhusu Fedha zitoke kwani wana nafasi gani kwny Mchwakato wa kuzitoa hizo Fedha ?

Msingi wa kufungukuliwa kwa Account ya Escrow wengi mmepotoshwa, Msingi wa Account ya Escrow ni Mgogoro baina ya Wanahisa wa IPTL waliokuwa wana Mgogoro sio IPTL na Tanesco japo kilikuwa na Shauri Mahakamani baina ya Tanesco na IPTL, wana Hisa wa IPTL baada ya kumaliza tofauti zao Hapakuwa na haja ya kuendelea kuwepo kwa Account ya Escrow ilibidi kila Mtu kuchukua chake

Kuhusu Habari ya Kodi, With holding Tax unakatwa direct na Mpokea Huduma( Tanesco) kabla ya ku effect Malipo
Kwny Kodi ya Mapato James Rugemalila alikuwa Smart kulipa hizo Fedha TRA kwa kujulisha source ya Mapato yale
Kwa Upande wa Singa Singa hakulipa hiyo Coperate tax na hapo ni kosa la kukwepa kodi sio kuchota Fedha za Escrow na Kama inavyosemwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom