Helkopta, magari ya Zimamoto mangapi tuliyonayo karne hii ya uchumi wa Viwanda?

Vyura99tu

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
1,641
1,747
Nimekuwa nawaza katika kuendelea kufanya mambo makubwa na ya kuinua uchumi wa chini walau basi kufikia wa kati!

Tumekuwa na matukio mengi ya hapa na pale ambayo kwa ujumla wake ili kufikiwa haraka na kuendana na barabara zetu, Je ni Helicopter ngapi ziko nchini mwetu kwa huduma za haraka na hata uokoaji?

Pia kwa kuwa tumeendelea kujenga majengo makubwa na marefu hata kule tunakopeleka mji mkuu Dodoma. Je, Magari makubwa ya kudhibiti moto kwenye majengo tunayo mangapi?

Miundo mbinu ya mabomba ya maji ili magari kuendelea kujaza maji eneo la tukio yameimarishwaje?

Ni vyema basi kama hatujafikia mahali hapo basi washauri wa mwenyekiti semeni paazeni sauti tupunguze baadhi ili tuweke vitendeakazi hivi ndani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili bunge la mwenyekiti hawana wasiwasi na majanga, yakitokea watakwapua ramirambi na kuneemeka.
 
Shauri yako, watakuja kukutukana kuwa hawataki maendeleo ya vitu, wanataka ya watu. Mimi mpaka leo hawajaniambia tofauti yake.
 
Hayo majengo yanayojengwa kisasa yanawekewa system ya kukabiliana na moto yenyewe kabla hao zimamoto hawajafika.

Tununue helicopter kwa ajili ya moto wakati hata magari ya kubebea wagonjwa ni shida tutakuwa hatuna akili kbs


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo majengo yanayojengwa kisasa yanawekewa system ya kukabiliana na moto yenyewe kabla hao zimamoto hawajafika.

Tununue helicopter kwa ajili ya moto wakati hata magari ya kubebea wagonjwa ni shida tutakuwa hatuna akili kbs


Sent using Jamii Forums mobile app
Janga la moto likitokea waungueee weee na wengine waangamie badala ya kuzuia halafu hayo magari na helicopters ndio zibebe majeruhi na maiti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi letu la zimamoto linahitaji maboresho makubwa sana maana vitendea kazi bado ni tatizo ila ufinyu wa bajeti unawakwamisha.
 
KAmbulan Es SalaamAmbulance j (DAR) - London (Any)
1 adultEconomy


Ambulance je,
 
Back
Top Bottom