Heligoland-Zanzibar Treaty:The basis For Malawi Claims | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heligoland-Zanzibar Treaty:The basis For Malawi Claims

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by anney, Aug 4, 2012.

 1. a

  anney Senior Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Read this Heligoland treaty document between German & Great Britain which is the one of the documents used by the Malawi government to argue their case.
   

  Attached Files:

 2. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Serikali ya Tanzania inalijua hili kwa wazi na mapana yake kwamba hatuna haki hata ye tone moja la maji ya Ziwa Malawi.

  Serikali haitakiwi kulifanya jambo hili la kisiasa maana kama ni siasa zako utacheza na wananchi wako lakini unaoweza kuwapiga mabomu ya machozi lakini si kwa watu kama Malawi ambao ni Soveregn state subject to international laws.

  Kama kweli Tanzania inataka hata tone moja la Ziwa Nyasa, iachane na porojo za kisiasa na i-file lawsuit for the boundary ili mpaka uwe katikati ya maji kama wengine duniani.

  Vinginevyo tutapigizana kelele kama wajinga na hakuna litakalotokea. Tutasubiri Rais wa Malawi tunayechekeana naye anayewapiga mabomu wapinzani wake nchini mwake, sisi tunatumia ziwa lile na kudhani kama ni letu.

  Kesho wapinzani wa Malawi waliokuwa wanapigwa mabomu ya mchozi wanakamata nchi, na nyinyi mliokuwa ama mnakaa kimya bila kumkemea anaona mnatumia ziwa lake na si lenu. Kwa nini asilie na nyinyi.

  Mimi huyu mama wa Malawi namkubali. Inawezekana anawapa fundisho wote waliomkera akiwa mpinzani wa serikali. Unadhani kwa nini alisema hamtaki Omar Bashir kuja mle.

  Mwacheni mama yetu awafundishe adabu wote wanaodhani tutafumbia maonevu ya dunia na ndipo mjue muonewaji akikamata power mjue litakalotokea.

  Najua kuna watakaonikejeli kuwa sina uzalendo. Hapa si suala la uzalendo. Baba na mama yangu wakifanya ujambazi wa kumdhulumu jirani yangu siwezi kukaa kimya na kuwatetea kwa kinachoitwa uzalendo. Huo ni wizi.

  Nendeni Mahakama za Kimataifa kuwashinda wamalawi na msidhani wa kupelekwa mahakamani ni migomo ya madktari na walimu tu.
   
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu Anney,

  Kwanza kabisa hii document inasema kwamba mkataba huu ni wa muda "temporarily".

  Halafu kwa uangalifu soma vipengele X1 na X11.

  Kwenye kipengele cha X1 inasemwa kwamba Sultan atarudisha kisiwa cha Mafya kwa wajerumani kwa ridhaa ya Uingereza bila masharti.

  Kipengele cha X11 kinasisitiza kwamba mpaka itakapopitishwa na bunge la Uingereza sehemu hio inabakia kuwa chini ya Uingereza.

  Sasa wamalawi wakichukulia hii document wanakuwa wamekosa kila kitu.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  WEWE NI MJINGA HAUNA AKILI, kama ziwa lote ni la malawi, ile bandari ya mbambabay kule mbinga na ile ya kyela zinafanya nini, mbona muda wote tumekuwa tukisafirisha bidhaa zetu mle bila malawi kuingilia, sasa wameona kuna mafuta ndo wanataka kutuzuia, si wangetuzuia toka zamani tusijenge bandari ya mbambabay pale na kule kyela na kusiwe na usafiri kutoka mbinga hadi kyela kwa maji ya ziwa, zile hotel za matemabeach kule kyela zinafanya nini kwenye maji ya malawi?...are you serious?
   
 5. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Richard,

  Kigezo cha mipaka ni ramani iliyokuwa submitted huko United Nations. Wanaochora ramani hizikwenye GoogleEarth na GPS zote si wajinga. Ni ramani wanayotumia.

  Narudia, haya mambo Tanzania ilitakiwa kuliwasilisha kwenye international community kuliko kudanganya kuwa inachukua hatua zingine ambazo sanasana zitailetea matatizo Tanzania.

  Malawi wako correct.
   
 6. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu, nakuunga mkono kabisa ila nilitaka tu pawepo angalizo kwenye hii document.

  Malawi wanaangalia wao walipata nini baada ya uhuru na hii kitu ya Ziwa Nyasa haipo kwenye akili yao.

  Wakoloni wametuletea matatizo sana.
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nikupateje wewe utakuwa mmalawi uliyejibanza hapa kwetu.
  Kama ni mtanzania basi utakuwa jinga kabisa. Miaka yote wamalawi walikuwa hawajui kwamba ziwa lote ni la kwao?
  Nachojua ni kwamba malawi watake wasitake, wapende wasipende tunagawana pasu kwa pasu ziwa nyasa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Acha porojo za google earth na treaty za wakoloni uchwara.

  UN Convention ya 1982 inasemaje kuhusu mipaka ya majini!??
   
 9. J

  Jonas justin Member

  #9
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nawasiwasi na uraia wako...
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kitu cha 1890 hawa jamaa wana shida kwa brain sasa nasi tukikomaa na mikataba ya karne ya 19 si Rwanda na Burundi zitakuwa mikoa yetu!
   
 11. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wewe ndo twambie sasa hiyo convention ya 1982 inasema nini !
   
 12. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Achana naye huyo. Haelewei kwamba hiyo convention iko valid kama hakuna Treaty.

  Unadhani wa-Malawi nao ni wazembe kutunza international document zao kama wewe ulivyoshindwa kutunza Mkataba wa Muunngano wa miaka 48 tu iliyopita??!!
   
 13. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hapana hawapo right, na muanzisha topic sidhani kama hii ndo hoja ya Wamalawi. Huu ni mtazamo wake Anney yeye binafsi

  Kamuzu Banda alijikita kwenye mipaka ya pre-colonial societies/ kingdoms. Ndo maana akasema hata zile wilaya nne za mpakani kwa upande wa Tanzania ni za Malawi.

  Nionavyo mimi aidha tuwaachie tu Wamalawi mbona hata Kawawa ashawahi sema hilo ziwa ni lao.

  Ila kama tutang'ang'ania basi tufanye hivyo kwa kigezo cha sheria za kimataifa zinazoitwa Littoral law na Riparian law. Hakuna ubishi kati yetu na Wamalawi kwamba hilo ziwa linaunda mpaka. Kwa upande wetu tunasema mpaka upo katikati ya ziwa.

  Hata hizi google maps mnazozipost hapa zinaonesha hilo ziwa ndo linaunda mpaka. Na hapa ndipo littoral na riparian law zinaweza kutumika. Kwa mujibu wa littoral na riparian law sisi pia tuna haki ya kumiliki hilo ziwa kwa kigezo kwamba linaunda mpaka wetu hata kama limelalia upande wa Malawi
   
 14. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Riparian zones ni maeneo yanayopakana na kingo za ziwa au bahari. Ni kwa mujibu huu ndiyo tukaweza kujenga Mbamba Bay port.

  Kuhusu Littoral zone kwa hili ziwa ni ngumu kwa sababu kumbuka hili liko katikati ya rift valley na dimension zake si kama kwenye coastline.

  Hivyo, ama utumie Littoral law au Riparian law bado utaipotosha Tanzania kwa sababu si madai yake. Tanzania inataka mpaka uwe katikati wakatikwa hizi mbili haiwezi ku-achieve hiyo goal.
   
 15. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Need we say more? watu wanataka kufanya serious business. Sio misifa ya kuwa na maliasili kibao wakati tija ni sifuri...go Malawi.
   
 16. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Haijalishi mpaka upo kwa wapi hizo sheria za riparian na littoral zikitupa umiliki wa namna moja au nyingine hao Malawi hawataruhusiwa hata kujenga bwawa. Mimi naona tuanzie hapo
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lakini unajua Treaty hii pia haizitambui nchi za Rwanda na Burundi..Sasa tuwauliza Malawi wao wanazitambua nchi za Rwanda na Burundi?.. kama wanazitambua inakuwaje wanapingana na treaty hii hii wanayoitumia leo kudai Lake Nyasa ni yao..
   
 18. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wewe ndie mjinga, kwani Malawi wanamiliki ziwa (maji)na sio ardhi ambako nyie mumejenga bandari za Mbambabay na Kyela.
   
 19. mkada

  mkada JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Kuna watu wanajiita jf snr expert member,halafu kichwani ni empty headed,yaani tabula rasa
   
 20. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,869
  Likes Received: 2,815
  Trophy Points: 280
  Sasa kama ni wajuzi wa kutunza documents walikuwa wapi wakati tunayatumia hayo maji? Acha uvivu wewe! Yaani hapa wote tunatakiwa kuwa wapole tuelewane kindugu tu. Maana kama tukiamua kufuatilia mipaka ya Deutsch Ostafrika tutaenda kudai Rwanda, Burundi zirudi kwetu na Dar, Tanga, Mtwara, Mombasa, Lamu, Malindi n.k ziende kwa Sultani wa Zanzibar.

  Ziwa tutaligawa kati kwa kati watake wasitake!!
   
Loading...