PreGE2025 Helbeth Mlelwa anadaiwa kukamatwa na polisi kwa kurekodi ujumbe wa kulaani kukamatwa Tundu Lissu TikTok

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Kada wa chama cha demokrasia na maendeleo Hilda Newton kupitia ukurasa wake wa X ameandika kuwa Helbeth mlelwa akamatwa kwa kosa kurekodi video kukamatwa kwa Mwenyekiti Lissu.

"Taarifa za hivi punde serikali ya kupitia jeshi la polisi kanda maalumu Dar es Salaam imemkamata Helbeth Mlelwa mkazi wa Kigamboni kwa kosa la kurekodi ujumbe wa kulaani kukamatwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu. Polisi hao wanadai ujumbe huo uliopo YouTube umevunja sheria za nchi bila kutaja ni sheria ipi imevunjwa.

Mlelwa amefikishwa kituo cha polisi Kigamboni na baadaye ametolewa kituo cha polisi Kigamboni na kupelekwa kituo kingine ambacho hakijawekwa wazi. Ndugu zake ambao waliongonzana naye kama mashahidi huru katika kituo hicho cha polisi wamefukuzwa na polisi Kigamboni. Nawasiliana na mawakili wapiganaji wa Dar ili waende Central posta au Oysterbay. Wakimkosa tutamfuata Murilo nyumbani kwake Mbezi na kumalizana naye hukohuko uzuri kwake panafahamika.

Naweka hapa link ya video hiyo ya kulaani kukamatwa kwa Lissu ambayo polisi wanadai inavunja sheria" - Hilda Newton


Mlelwa anafanya shughuli za kidini kama mchungaji na hii ndio video aliyerekodi akilaani kamatwa kwa Lissu

Your browser is not able to display this video.
 
Kazi ya Mungu inaendelea kufanyika.

Njia iliyonjema.
 
Vyama hivi vya siasa visitufanye tuwe maadui tutangulize utu Mbele.

pastor Helbeth
 
ChoiceVariable kuna sheria ya nchi imevunjwa hapo? Au ndiyo mnaanza kushughulika na mnaowaona wanachanganya dini na siasa? Sasa hii ndiyo jambo jema. Washughulikieni halafu muone maana wapo waliosema, wanaosema na wengi watasema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…