Heko Usalama wa Taifa

Pamoja na yote,to this end ninawasiwasi na waliopewa dhamana ya kuiongoza idara hii muhimu kwa usalama wa nchi yetu,hainiingii akilini hata kidogo kuwa na idara yenye ufanisi wakati kiongozi wake mkuu serikalini kwa maana ya waziri wake akishabikia mambo ambayo matokeo yake yanaweza kuharibu usalama na utulivu wa taifa..am sorry to say this ,to me she is a public relation officer wa mafisadi.
 
Hapiness Katabazi kauona ukweli lazima aseme kuwa penye kutoa hongera basi itolewe.nyie mliozoea kulaumu kila kitu kazi kwenu.
Hongera Katabazi kwa kuamka.
 
Mh!!! nimeshtuka huyu dada inawezekana anautaka ubunge wa kuteuliwa.Na bado tutayaona mengi mwaka huu.
 
Ni kweli mkuu, baada ya kutuletea makala hiyo aliyo andika awali, kila mwenye akili atamwelewa. Aje hapa atufafanulie tofauti hizo mbili za makala zake zimetokana na nini? Maana zina rangi tofauti, nyeusi na nyeupe.
awezekana na yeye ni mmoja wao, anatikisa kiberiti kujua njiti zimo au la. Ndio namna nyingine ya utendaji wa wasalama wa Taifa. Wataupataje umbeya kujua watu wanafikiri nini wajue pa kuanzia? Ile ya kwanza haikumpa feedback ya kutosha, sasa amegeuza sura angalau apate kwa wale wanaoamini mbadala wa ile ya kwanza.

Ofcourse hakuna mtu anayekuwambaya tuuuu pasipo uzuri hata kaduchu, au mzuriiiiiii na hakuna hata ubaya hata kaduchu. Hata Nyota ya Asubuhi Malaika alieaminiwa sana na Mungu si alikujaonyesha picha yake halisi ya upande wa pili ndipo katupwa duniani? Ikiwa mti mbichi unaunguzwa, mti mkavu itakuwaje?

Leka
 
Mpunguzieni Rais nguvu nyingi za KUTEUA zisizohojiwa wala kuthibitishwa na yeyote ili tupate WATENDAJI wazuri kwenye idara nyeti kama hii ya TISS. Vinginevyo wote wanaoteuliwa wataendelelea kuwatumikia kwanza waliowateua. Naamini TISS kama zilivyo idara na taasisi nyingine za UMMA zina watu ambao wanaweza kufanya kazi vizuri tu kwa maslahi ya Taifa kwanza.
 
Hapiness Katabazi kauona ukweli lazima aseme kuwa penye kutoa hongera basi itolewe.nyie mliozoea kulaumu kila kitu kazi kwenu.
Hongera Katabazi kwa kuamka.
Hakuna anayeweza kushangaa kwa uliyosema.
 
Nimesoma hoja yako mama,l abda kama nimesoma haraka haraka,lakini sioni jambo lolote la kukufanyanya wewe uwapongeze usalama wa Taifa. To me hawa ndio watu ambao in the first place wametufanya tufike Tanzania hapa tulipo leo. Wangekuwa makini yote tunayo yaona leo yangeonekana mapema na yakarekebishwa.

Jamaa hawa wametekwa kabisa na uovu ulioko katika jamii leo,kwa hiyo hawana uwezo kabisa wa kutusaidia kama ilivyotegemewa unless a complete overhaul of the system is made.
 
Nimesoma hoja yako mama, labda kama nimesoma haraka haraka,lakini sioni jambo lolote la kukufanyanya wewe uwapongeze usalama wa Taifa. To me hawa ndio watu ambao in the first place wametufanya tufike Tanzania hapa tulipo leo. Wangekuwa makini yote tunayo yaona leo yangeonekana mapema na yakarekebishwa.

Jamaa hawa wametekwa kabisa na uovu ulioko katika jamii leo,kwa hiyo hawana uwezo kabisa wa kutusaidia kama ilivyotegemewa unless a complete overhaul of the system is made.
Nimebaki naduwaa...nahisi ntabaki salama!
 
Propaganda hizi ni kama ujumbe wa leo.Nashukuru tumekuwa werevu sasa kujua what is going on.angalia Tangold,meremeta,BoT, and son hawa TISS wako wapi kila siku dhahabu inapotea kwenda majuu
 
Tanzania haijawahi kuwa na usalama wa taifa hata mwaka mmoja kama wapo basi watakuwa hawajui kazi na maana ya usalama wa taifa ninaweza kusema Tanzania tuna watu wa usalama wa viongozi wa taifa kazi inayoweza kufanywa na jeshi la polisi.

FBI au CIA kwa mfano vina vitengo vya kulinda maslahi ya mataifa yao CIA anaweza kuja kuishi Tanzania kwa muda mrefu tu anaweza kuja kama Mwalimu na ukiangalia wanaokuja wachache sana hufudisha masomo ya maana sana sana watafundisha PE au kwaya ya shule

Wengine huja kujifunza tamaduni zetu lakini hao wote lengo si tamaduni wanapiga mahesabu ni vipi nchi yao itafaidika na kitu gani toka Tanzania madini maliasili nk na kila siku wanapeleka ripoti makao makuu.

Angalia walivyo wepesi kukimbilia sehemu za majanga kama Haiti ni kweli watatoa misaada ya nguvu lakini ujue kuna kitu kinatafutwa kwa manufaa ya nchi zao hao ndio usalama wa taifa.

Tofauti na watu wetu kama nilivyosema tuna watu wa usalama wa viongozi wa taifa mtashinda nao bar mitaani hakuna wanachofanya cha maana hawana plan yeyote zaidi ya kuvizia vimagendo vidogo vidogo na dili za ujambazi ambazo nazo nyingi huwa wanahusishwa nazo utasema huo ni usalama wa taifa sasa polisi afanye nini.

Mkuu niliwahi kulisemea hili, CIA ndo waliua kiwanda chetu cha Nyumbu wakati wa Mzee Mwinyi na waliirubuni serikali ya TZ kwamba iachane na tekinolojia za urusi bali wao marekani watatoa pesa na kuiboresha ili itoe magari ya kiraia. Hapo walimnunua manager wa nyumbu na kumpa pesa kibao yeye bila kujua kuwa wale watu ni CIA. Serikali ilipoamua kuachana na kutengeneza magari ya kijeshi (nyumbu) na wamarekani walipo hakikisha kuwa mpango huo umekufa basi nao wakatoa masharti ya kutoa huo mtaji, serikali ikakataa masharti na wao wakajitoa kwenye mradi na ndo mwisho wa nyumbu.

Uoga wa USA ulikuwa kwamba tukiweza kuimarisha gari za nyumbu basi tutajukwamua haraka ktk umaskini na hivyo kutowategemea kwa misaada. Wakati yale yanafanyika hao vijana wetu wanao jiita usalama wa taifa/CCM walikuwa wanakunywa tu komoni.

Tujiulize tukio la ugaidi la 1998 pale kwenye ubalozi wa USA, je mpaka waarabu wakaja wakaishi pale kinondoni, wakapanga nyumba, wakatengeneza mabomu pale kimara bucha, na wakafanikiwa kuulipua ubalozi, wao walikuwa wapii???

Kwa ufupi ni kwamba idara zetu za usalama hakuna professionals na wale wachache wanao jaribu kafanya kazi kitaalam huwa wanazushiwa majungu na hatimaye kunyimwa madaraka.

Mfano mzuri ni kifo cha Gen. Imrani Kombe, mkapa alimuua yule jamaa kwa sababu alikataa mawazo ya kifisadi ya serikali ya mkapa.
 
Usalama wa taifa ni idara nyeti sana katika kuamua muskabali wa taifa kutimiza malengo yake Muhimu.Kwa nikijaribu kusoma comparative Defensive sysytem analysis ya Israel,Uk,USA vs Ya India na kisha nijaribu kufutailia kwa karibu hii ya kwetu hapo nyumbani...kwa kweli tunastahili kufanya kazi ya Ziada

Tatizo la mfumo wetu wa usalama wa Taifa linashabihiana sana na la India enzi za Jawahlal nehru ,na pia baadae tena hadi alipokuja kunadilisha hii system kwenye serikali ya mh.Narshran Rao...pia Chama cha BJP cha Atal behar Vajpayee akiwa Pm.so tatizo letu liko katik structure zaidi.Hata india wamekuja kufanya Reform kubwa miaka michache iliyopita na Mh.Manmohan singh wa congress

Zamani National security council ilikua ikitegemea zaidi retired army generals,foreign services officers ambao wengi walikua hawana ujuzi na internal issues.Leo hii ukiangalia Defency policy ya India ni nzuri sana...structure ya NSC na National Security Advisory Board(NSAB),Intelligence Bureau na coordination yake utaona ni kwa nini wameweza kuidhibiti pakistan,ni kwa nini wameweza kuwa alert na movement za China nk.

Nikipata muda nitachangia zaidi,kwakweli yetu inahitaji kazi ya ziada!
 
hii ndiyo elimu tuitakayo ili tujue kwamba tupo salama na nchi inalindwa ndani na nje.
 
Nilishikwa na butwaa nikitaka kujua kulikoni sasa nimeelewa pongezi hizi zna lengo gani katika zama tulizomo!
 
Back
Top Bottom