Kama utojali weka somo kidogo kuhusu BITCOIN.
Siyo mjuvi sana wa hii kitu ila ni crypto currency, yani ni digital money siyo tangible.
Aliyeanzisha hajulikani maana alijipa jina la uongo.
Inatumika kununua vitu na kulipana kama ilivyo mpesa au tigo pesa.
Sema sasa hii thamani yake imepanda sana kwahiyo wakati inaanza mwaka 2009 haikuwa na thamani, thamani yake ilianza kurekodiwa na kuuzwa mwaka 2010 haikuwa kufika hata 1$, thamani yake kubwa kuwahi rekodiwa mwaka 2010 ilikuwa bitcon moja sawa na 0.39$.
Kwa hiyo mfano ungenunua bitcoin 1000 ungetumia dollar 390.
Leo ungeamua kuziuza ungepata 6,600,000$ ambayo kwa tshs ni bilion zaidi ya 13 za kitanzania
Kwanini inapanda thamani sana?
Jibu ni kwamba jumla ya bitcoins zitakazokuwa kwenye mfumo ni milion 21, ambazo zinajiongeza kwenye mzunguki kila baada ya muda flani.
Mpaka sasa nusu ya bitcoins kati ya hizo milion 21 tayari ziko kwenye mzunguko ikiwa na maana zaidi ya bitcoins milion 10, na nusu bado haijaingia kwenye mzunguko itaingia mwaka 2020.
Bitcoin inapatikana kwa kuichimba kama dhahabu tofauti yake unaichimba kqa kutumia computer, ambapo kila block 1 ni sawa na bitcoin 12.5, na kila siku zinachimbwa kama bitcoin 3,600.
Kama kuchimba huwez unanunua,
Inasemekana kwamba mtengenezaji mkubwa wa software ya bitcoin ajulikanaye kwa jina fake la Satoshi Nakomoto anamiliki bitcoin milion 1.
Hivyo utaona ya kwamba kuna bitcoin chache kwenye mzunguko wakati kila siku wahitaji wanaongezeka.