Joshua Mbezi
JF-Expert Member
- Oct 18, 2024
- 1,935
- 4,181
NGUVU na AKILI: TUBOMOE au TUJENGE?
Kuna mwimbaji aliimba, “Bomoa eh, Bomoa Baba Tutajenga kesho”
Na wana mikesha wakaimba,
“Chocheaa, Chocheaa karama ya Bwana chochea”.
Lakini Bwana Yesu anasema katika Mathayo 5:9, “HERI WAPATANISHI MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU”.
Nchi ina joto kali. Tunahitaji kiyoyozi cha kupoza siyo heater ya kuongeza joto.
Anayesikia joto kali na anayesikia baridi kali, nani anahitaji kutumia akili kujilinda?
Mwenye joto kali aweza kuvua nguo zote na kubaki uchi ili asisumbuke na joto.
Mwenye baridi anahitaji akili kupata nguo za joto ili kujilinda na baridi.
Kama taifa, kwa sasa tunahitaji akili si nguvu. Nguvu ni kwa ajili ya kubomoa, lakini akili ni kwa ajili ya kujenga. Kwa nini?
1. Hao wana harakati wa Kenya hawakutumwa na serikali yao. Mnaharibu mahusiano ya nchi kwa ujinga wa watu wachache.
2. Wanaojibu kwa kukashifu wakenya, hawajatumwa na rais wala serikali. Uchawa usivuruge mahusiano na nchi jirani.
3. Huyo “mjinga” Gwajima kajituma au katumwa, anajua yeye. Jadilini hoja achana na ukichaa wake. Mlipoiba kura ili ashinde hamkujadili bungeni, leo bunge linafika mwisho ndo mnatuambia mliiba kura? Basi futeni sheria zooote alizoshiriki kutunga. Hatutaki sheria zilizotungwa na mwizi?
4. Sawa, Gwajima kakosa adabu. Nyie mmekosa zaidi kwa kujitambulisha mlivyo wezi.
5. Rais wetu siyo “Katope” kwamba mnamkinga na mvua asiyeyuke. Mbona mnamsengenya kila siku mitaani? Ana uwezo mkubwa tunamjua na hilo mnalijua. Ana roho ya utu na tunaijua. Msimtumie kubariki mambo mabaya yanayotokea.
6. Kutekwa na kupotea kwa watu ni tatizo. Kama kuna aliyeteka kwa kuagizwa na mamlaka ajitokeze tumuone. Kimya hakiondoi tatizo. Shetani Gwajima kahoji jambo jema. Tulikatae kwa sababu limeletwa na shetani? Mamlaka ya kutoa roho tumwachie Mungu aliyeiweka (Mwanzo 2:7).
7. Kwa nini Msajili anaipigia kampeini CHADEMA? Kila hatua anayochukua inachochea moto na kuongeza huruma kwa CHADEMA. Ugaidi na uhaini wa CHADEMA hauongezi uzalendo kwa vyama vingine. CHADEMA ina uwezo wa kujiharibia na tunauona bila darubini. Iache ijifie.