Hekima ya masikini haisikilizwi

LUCKYHUSTLER

Member
Jul 9, 2012
14
11
HEKIMA YA MASKINI HAISIKILIZWI.
Jioni ya leo nikiwa natazama video kuhusu biashara na mafanikio, baada ya kutazama video kadhaa hatimaye nilikutana na video ambayo mfanyabiashara Mo Dewji alikuwa anahojiwa. Kilichotokea ni kuwa nilikuwa makini zaidi kumsikiliza huyu bwana kiasi ambacho kilipelekea kujihoji mwenyewe kuhusu ulipopatikana umakini huu, maana ni jioni nilishachoka pia nimetizama video nyingine kwa umakini usiotulia sehemu moja (divided attention).

Kipengele kilichonivutia zaidi ni pale aliposema ‘Afrika watu wenye utajiri wa kuanzia dollar bilioni moja ni 31 tu na yeye yumo’ Sitaki kuujadili utajiri wake bali nitajadili umakini(Attention)– moja ya bidhaa muhimu duniani hasa baada ya kuongezeka kwa mambo ila muda ni ule ule.Umakini tulivu niliokuwa nao katika kumsilikiliza bilionea huyu bwana Mo (selective attention).

Imeandikwa kuwa ‘ hekima ya maskini hudharauliwa wala maneno yake hayasikilizwi’ wakati namsikiliza nilikuwa nafahamu hekima ya maskini haisikilizwi. Moja ya tafsiri niliyokuwa nimeilewa ni hii maneno hayatoshi matendo yanahitajika.

Ili uweze kufanya mambo hapa duniani lazima uwe tajiri.
Maana nyepesi ya utajiri imebebwa na wingi wa kile ulichonancho, moja ya msamiati unaopendwa na wanadamu ni huu wingi/vingi yaani ‘more’ kila mtu anataka more money, more knowledge, more power, more….. na msamiati huu unahusihwa na vitu vizuri tu hakuna anayetaka more stress au more problems haya mambo mabaya msamiati wake ni less.

Ni nini kinachotuvutia kutamani vile vitu vizuri kwa wingi, jibu lake ni asili ya mwanadamu Mungu hakumuumba mtu awe na vichache bali vingi. Mungu hachukizwi na utajiri uliopatikana kwa njia nzuri na unaotumika vizuri. Fikiria hili jambo tajiri wa kwanza duniani ni nani?

Wengi watasema mfalme Sulemani ila ukiufikiria uumbaji vizuri utagundua tajiri wa kwanza duniani ni Adam na mkewe. Kwanini ? Adam alipewa vyote yaani bahari zilikuwa zake, mito yake , samaki wake, ardhi yote yake, milima yake, mbuzi, ng’ombe, kondoo, swala, simba……………

Hivyo vyote Mungu alimpa yeye avimiliki na kuvitawala, so huyo ndo tajiri anayeongoza katika historia ya wanadamu. Yaani ni tajiri mpaka wa watu, kwasababu watu bilioni 7+ waliopo ni watoto wake, wajukuu……………
Nieleze sababu mbili kubwa nilizozipata baada ya kujihoji, na kuukumbuka huo mstari wa Biblia.

Sababu ya kwanza ni hii hekima ya maskini haisikilizwi maana haina nguvu. Huwezi kuwa unaongea maneno matupu lazima ili uheshimiwe na wale wanaokusilikiliza ni lazima uweke kwenye utekelezaji vitu vionekane. Sababu ya pili ni hii wanadamu tumeumbwa katika namna ya kupenda utajiri au wingi wa vitu au neno more katika mambo yote mazuri.Kwahiyo tajiri atasikilizwa kwasababu ameweza kuwa na vingi hivyo anao ushahidi wa namna ya kupata vingi.

Mtu maskini aweke tangazo juu ya semina ya wajasiriamali topic iwe ni jinsi ya kuwa tajiri, ni ngumu kupata hata mtu mmoja hata kama hakuna kiingilio. Kwasababu hekima yako unayotaka kutufundisha tuwe matajiri haijakusaidia wewe mwenyewe itamsaidia nani?

Ila akiweka tangazo hilo hilo mtu tajiri watu wataenda kumsikiliza na watalipa pesa awafundishe, wakijua anayosema ameyafanyia kazi na amepata matokeo bora ( sio maneno matupu). Kutaka kupata utajiri ni asili ya mwanadamu, sio jambo baya kwasababu ya nini uutake umaskini kwa faida gani?

Nimetafakari na kuamua kukufikirisha juu ya asili yetu.
Best wishes in your endeavors.

Goodluck Edington Moshi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom