Hekima ya Lowassa imeua upinzani Tanzania

Hekima ya Lowassa imeua upinzani Tanzania

Yeye aliyejaliwa hekima hawezi kuanguka au kuangushwa kirahisi.
 
Wapo wengi watakaojitahidi kupinga mtazamo wangu, ila naomba kila anayepinga apinge kwa vigezo vinavyoeleweka.

Siasa za Tanzania hazihitaji upole na kukubali kunyenyekea kwa watawala. Siasa za Tanzania hazihitaji hofu na kuogopa watawala na vyombo vya dola.

Ili kufanya siasa za Tanzania inahitaji kujitoa muhanga kama ambavyo CUF na CHADEMA imekuwa ikifanya muda wote.

Ni Lowassa aliyewashauri watu watulie, baada ya kuona tume imependelea, kama watu wangehamaki na kupambana kwa vyovyote vile kungekuwepo na heshima kubwa kati ya chama tawala na wapinzani.

Ni Lowassa alimwambia Seif atulie atafute haki kwa mazungumzo, niwakumbushe, kilichosababisha serikali ya mapinduzi ya Z,bar kufanyia marekebisho katiba yao ni ung'ang'ari wa CUF waliokuwa nao baada ya chaguzi mbalimbali.

Kama wapinzani wangekuwa na ile tabia yao ya kungangamara kama zamani leo uonevu unaoendelea usingekuwepo hata Rais Magufuli asingewanyanyasa kama anavyofanya leo, maana amegundua ni waoga sana.

Nchi za Afrika zote ambazo zimepata adabu na kuheshimiana ni pale wapinzani walipokubali kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya wengine.

Lowassa hekima yako imewaponza wapinzani
Acha kupotosha sio hekima za Lowassa ndio zimewaponza wapinzani,bali ni matendo yake Lowassa ndio yana wagarimu wapinzani hivi sasa,unatarajia Lowassa atakeme rushwa au ufisadi ambayo ndio ajenda kuu ya Chadema wakati msafi Dr Slaa alipokuwa ndio jemedari wa mapambano,Kwa kifupi kwa sasa Lowassa ni sawa na samaki aliyeopolewa baharini na kuwekwa kwenye beseni la maji,tunasubiri maigizo ya mafuriko kwa wanachadema wenzake .
 
...Siasa za Tanzania hazihitaji upole na kukubali kunyenyekea kwa watawala. Siasa za Tanzania hazihitaji hofu na kuogopa watawala na vyombo vya dola...
Mbona wewe muoga na unajificha nyuma ya keyboard sasa?
 
Ni kweli nilimpigia Lowasa kura lkn nimekosa IMANI naye, nahisi amekuja kuua upinzani..aangaliwe kwa jicho la 3
 
Lowasa kiukweli simpendi kabisa.huyu mzee kasababisha matatizo mengi sana huku upinzani..kasababisha tumempoteza Dr.slaa,,kasababisha CUF leo hii ina mgogoro maana bila yeye Lipumba asingejiuzuru,,kasababisha tumepigwa ban mikutano ya siasa,kasababisha leo Chadema tunashindwa kuuongelea ufisadi maana fisadi papa tupo nae meza kuu,yaaani huyu mzee kasababisha matatizo chungu nzima huku upinzani..
Ninamlaumu Mbowe sana. Afunguke aachane na Lowasa
 
EL na Sumaye wapo upinzani ili kudhoofisha na mwisho kuua kabisa nguvu waliyonayo, kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa.

Siyo KWELI ndugu yangu. Ingekuwa hiyo ndo kazi waliyotumwa kufanya, leo hii JPM asingehangaika kutumia mamilioni kuhangaika na upinzani. Pili, asingezuia mikutano ya siasa. Maana ndo ingekuwa njia rahisi ya kupumbaza wananchi.

Kinyume chake ni kwamba, nakubaliana na huyu mleta uzi kwamba, matumizi ya Hekima iliyopitiliza ndo huzalisha uonevu ulipitiliza. Hapo Kenya wanaheshimiana sasa hivi maana wapinzani hawachekeani na watawala. Lakini, tusisahau pia kuwa, JPM naye anafahamu hilo na ndo maana kuna tofauti kati yake na JK.

Mmoja aliamini sana kwenye matumizi ya hekima na upole na mwingine amegundua Hekima ikizidi Taifa litaangamia. Mimi nadhani Upinzani kuanzia day 1, walipotangaza UKUTA, walitakiwa watoke barabarani, jeshi lipige, liue lifanye nini lakini ambacho kingefuata ni kuanza kuheshimiana.

Haiwezekani kila siku wewe uwe wa kuua raia wako tu, kuna siku utashindwa au kulazimishwa kuacha. Heshima ingekuwepo. Kwasasa, JPM ndiye mpinzani, Lowassa utafikiri ndiye Rais.
 
raisi wa mioyo.......swala ni kukosa hoja ndicho kinachoitafuna upinzani swala la kukubali ama kukataa matokeo halijaanza leo limeanza kitambo kama nikuingia barabarani basi watu wangekuwa wameshaingia barabarani hata before lowassa kugombea 2015.
Mwaka sijui wa ngapi sasa wapinzani wanakataa kila matokeo ya uchaguzi lkn hathubutu hata mtu mmoja kuingia barabarani kuandamana.
 
Siyo KWELI ndugu yangu. Ingekuwa hiyo ndo kazi waliyotumwa kufanya, leo hii JPM asingehangaika kutumia mamilioni kuhangaika na upinzani. Pili, asingezuia mikutano ya siasa. Maana ndo ingekuwa njia rahisi ya kupumbaza wananchi. Kinyume chake ni kwamba, nakubaliana na huyu mleta uzi kwamba, matumizi ya Hekima iliyopitiliza ndo huzalisha uonevu ulipitiliza. Hapo Kenya wanaheshimiana sasa hivi maana wapinzani hawachekeani na watawala. Lakini, tusisahau pia kuwa, JPM naye anafahamu hilo na ndo maana kuna tofauti kati yake na JK. Mmoja aliamini sana kwenye matumizi ya hekima na upole na mwingine amegundua Hekima ikizidi Taifa litaangamia. Mimi nadhani Upinzani kuanzia day 1, walipotangaza UKUTA, walitakiwa watoke barabarani, jeshi lipige, liue lifanye nini lakini ambacho kingefuata ni kuanza kuheshimiana. Haiwezekani kila siku wewe uwe wa kuua raia wako tu, kuna siku utashindwa au kulazimishwa kuacha. Heshima ingekuwepo. Kwasasa, JPM ndiye mpinzani, Lowassa utafikiri ndiye Rais.
Cheki facts hizi:

* Arusha kipindi kile cha maandamano ya CHADEMA watu ya waliuwawa afu hakuna chochote kilichotokea

*Maandamano mengine Mwangosi kauwawa kimyaaa

*Kamanda Mawazo kauwawa kinyama sana sana wala hakuna mtu aliyejali.
 
Tatizo mnajadili Tanganyika tu, ila maandamano yalileta big result Z,bar. kama si kuwa ngangari kusingekuwepo serikali ya umoja wa kitaifa. Safari hii kama Cuf wangechachamaa nakuhakikishia Shein asingeweza kutawala Seif angepewa haki yake
 
Kama yangeleta manufaa kwao kwanini hawakuthubutu kuandamana?Mziki wa kukimbilia mombasa kipindi kile unadhani ilikua mchezo.
 
Lowasa kiukweli simpendi kabisa.huyu mzee kasababisha matatizo mengi sana huku upinzani..kasababisha tumempoteza Dr.slaa,,kasababisha CUF leo hii ina mgogoro maana bila yeye Lipumba asingejiuzuru,,kasababisha tumepigwa ban mikutano ya siasa,kasababisha leo Chadema tunashindwa kuuongelea ufisadi maana fisadi papa tupo nae meza kuu,yaaani huyu mzee kasababisha matatizo chungu nzima huku upinzani..
pambana na hali yako mkuu wewe siyo mpinzani
 
Lowassa hekima yako imewaponza wapinzani

Kuna hadithi ya ya Hisopo ya chura aliyekubali kumbeba nyoka mgongoni ili kumvusha ng'ambo. Walikubaliana kuwa nyoka asimgonge chura na nyoka alikubali. Walipofika ng'ambo alipomtua tu nyoka akamgonga! Chura akaruka na kuuliza "kwanini umenigonga tena baada ya kukuvusha?"...
 
Cheki facts hizi:

* Arusha kipindi kile cha maandamano ya CHADEMA watu ya waliuwawa afu hakuna chochote kilichotokea

*Maandamano mengine Mwangosi kauwawa kimyaaa

*Kamanda Mawazo kauwawa kinyama sana sana wala hakuna mtu aliyejali.
Na watu wanaouawa kwenye maandamano ya siasa huwa ni mazwazwa, huwezi kukuta hata siku moja Mbowe au familia yake imepata hata mchubuko wakati wakiandamana
 
Naamini upinzani hautokufa,ila cha moto watakiona!
 
Back
Top Bottom