Hekaheka za Xmas na kunusurika kifo

Mjusi Sharobalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2025
Posts
8,306
Reaction score
14,631
Salamu wakuu.

Ndani ya siku hizi mbili tatu nimekuwa na ukimya usio wa kawaida ndani ya jukwaa hili na si kawaida yangu kupotea kwa muda mrefu kiasi hicho.

Ukweli ni kwamba nilikumbwa na tukio la uvamizi usiku wa XMAS tarehe 25 December baada ya kuvamiwa na vibaka, majambalika, wakulungwa wa jiji na wazee wa ngwasuma mishale ya saa 7 usiku.

Hakuna mazara makubwa niliyapa kiafya zaidi ya kuchukuliwa kiasi cha pesa kadhaa pamoja na simu inayonipatia kiburi na jeuri ya kuzurura humu jukwaani masaa 20 na ma4.

Nawasilisha.
 
Karibu tena bro nakubali ujchetuaji waki hapa jf
 
Unajisikiaje kibaka au jambazi akipigwa risasi akafa?
 
Saa 7 usiku unazurura hovyo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…