Hee! Tukitangulizana nani ataonekana mfanyakazi ??

Hee! Tukitangulizana nani ataonekana mfanyakazi ??

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
Ni jirani.Sio mbali sana na nilipokulia.Nawafahamu vema tangu mume wake akiwa ni dobi,mpaka leo ana gari na duka moja ila sasa kwenye kuongeza duka la pili ndipo dada huyu anapoonekana kuwa njia panda na kutaka kuvunja ndoa yake.Utamshauri nini?
::
Ilikuwa hivi,,baada ya mume wake kuwa na duka kubwa na walau kujisahaulisha tabu alizopitia.Mume wake alimwita mkewe na kumshauri kwa wema "Mke wangu,duka limekua,wateja wamezidi,naona tufungue duka la pili,sisi wenyewe hatuwezi,na kama unavyojua muda wote nafuatilia bidhaa hivyo tutafute MFANYAKAZI wa kutusaidia kuuza dukani.."
::
Mwanzoni mke aliona jambo la kawaida,alikubali na duka likafunguliwa.Wakatangaza mtu yeyote anaeweza kuuza dukani,kwa mwezi hakuna aliyejitokeza.
::
Mungu si athumani,akajitokeza dada mmoja toka wilaya jirani,aliyeenda tu kuwatembelea ndugu zake.Na alipoambiwa tenda hiyo,,akakubali na akaenda kuwaona mke na mume hawa (majina yamehifadhiwa)
::
Mke alipomtazama dada yule,,ameumbika ni mrembo,ni mzuri alipowaza sana akaona hafui dafu na muda si muda,angenyanganywa mume! Akasema kabisaa "Hee! Tukitembea pamoja njiani,,nani ataonekana mfanyakazi?''
::
Mke kakataa,mume kakubali dada afanye kazi.Na mke wa jamaa kila siku analia.Amenipigia simu kuniomba ushauri,,nimemwambia anipe muda.JE NIMSHAURI NINI MKE WA JAMAA HUYU? Jamaa yangu huyu sijamweleza chochote,na tangu yule dada aanze kibarua,wateja ni wengi na biashara inaenda kasi.
::
Karibuni kwa ushauri.
=
 
Huyo dada mjinga, inabidi amwamini mumewe na ajiamini, maana kama atakataa huyo, wazuri na waliombika wengi tu. Ikiwa ana lake jambo asipolifanya hapo atafanya kwengine.
 
That is why alwayz you look so unique....U're looking for future/development....hajiamini wakati ameolewa na yupo ndani ya ndoa, je angekuwa kwenye period of shake well before use (a.k.a GF/BF) ingekuaje? mshauri aache utoto huyo demu-mke wa huyo msela!

Huyo dada mjinga, inabidi amwamini mumewe na ajiamini, maana kama atakataa huyo, wazuri na waliombika wengi tu. Ikiwa ana lake jambo asipolifanya hapo atafanya kwengine.
 
kwani kumkatalia ndo dawa?huyo m/ume anakutana na wangapi wazuri zaidi ya mke wake huko barabarani?na kama mume kashampenda huyo msichana hata asipokua mfanyakazi wake atamgegeda tu maana mawasiliano yapo..
 
Atakuwa anaogopa huyo dada kujimilikisha duka nn?
Mwambie ajadiliane tena na mumewe ,mke ana uzito wake atii!
 
huyo shosti wako mwambie atulie yupo so insecured na wivu tele kuzidiwa uzuri. Aache mawazo potofu, yamkini hajaona jambo lolote la kutia mashaka. Wazuri wapo tele zaidi yake hata zaidi yangu!!
 
Hajui tu,mwanaume akiamua ku-cheat ana-cheat tu..hata aletwe mbaya..akiamua kumfunua kama bibie hana msimamo anafunuliwa..
 
period of shake well before use (a.k.a GF/BF)

kwa kweli jitihada zinahitajika ktoka kwenye hili kundi lol
 
Back
Top Bottom