Heche kuongoza vijana Africa

Heche kuongoza vijana Africa

Hongera Bavicha, Hongera John Heche.

Nadhani uteuzi huu uwe ni chachu kwa bavicha, chachu kwa chadema na chachu kwa maendeleo ya kidemokrasia kwa vijana wa kitanzania.
 
Bigup Heche nd bravo CDM! Plz kama kuna m2 anajua anaweza kunipa kidogo data kuhusu elimu ya Heche na katibu wake na wana ishu gan nyingine mbali na sias" Akhsanteni kwa majibu mazuri makamanda.
 
"Bado Dunia inahitaji watu wenye uthubutu wa kufanya kitu sio wanaoweza kuthubutu kukosoa kitu"
hongera kamanda
 
Hongera sana Heche wakati wengine wakigombania u kampeni manager wewe endelea kuimarisha chama.
 
Wakuu hii ndio habari kutoka BAVICHA niliyofanikiwa kuidaka. Jisomeeni mwenyewe bandugu.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BAVICHA KUWA MJUMBE WA BODI YA INTERNATIONAL YOUNG DEMOCRAT UNION (IYDU)
Umoja wa Vijana wa Vyama vya Mrengo wa Kati Duniani (International Young Democrat Union, IYDU) ulifanya mkutano wake mkuu nchini Australia uliokutanisha vijana zaidi 120 kutoka nchi mbalimbali kuanzia tarehe 8- 14 Jan 2012 ambapo BAVICHA kama mwanachama wa umoja huu iliwakilishwa na katibu Mkuu wake Deogratias Siale.

Mkutano huu pamoja na mambo mengine ulikuwa na agenda ya uchaguzi wa viongozi kwa nafasi za mwenyekiti, naibu mwenyekiti, makamu wenyeviti 10 na mweka hazina. Katika uchaguzi huo, Bara la Africa lilikuwa na wagombea wawili katika nafasi ya makamu mwenyekiti ambao ni Charles Owerdu kutoka Ghana na John Heche, Mwenyekiti wa BAVICHA aliyependekezwa kuwania nafasi hiyo na nchi za Ufaransa, Ugiriki na Ujerumani.

Demokrasia ilichukua mkondo wake ambapo wagombea wote wawili kutoka Afrika hawakupata kura za kutosha kushinda nafasi hiyo ambapo makamu wote 10 walitoka nchi za Ulaya, Amerika na Amerika ya Kusini na Bara la Afrika lilikosa mwakilishi katika bodi ya uongozi wa IYDU.

Hivyo basi, bodi mpya ya IYDU iliyoketi jijini Sydney imemteua John Heche, mwenyekiti wa BAVICHA kuwa mjumbe mshiriki wa bodi ya IYDU ambapo atakuwa akisimamia masuala ya Afrika. Pia bodi hiyo imemteua Mercy Gakuya wa chama cha DP cha Kenya kushirikiana na Heche katika kusimamia mambo ya Afrika ambao kwa pamoja watakuwa wakihudhuria vikao vyote vya bodi hiyo kwa mwaka mzima.

Hii ni fursa muhimu kwa BAVICHA na vijana wote wa Tanzania wanaohitaji mabadiliko na uhuru wa kweli kwani pamoja na mambo mengine itasaidia kuendelea kupata uzoefu, ujuzi na maarifa ya kuendesha mapambano ya kudai haki.

Uteuzi huu unaendelea kuthibitisha kuwa Chadema siku zote kimekuwa kikipika na kutoa viongozi, si tu wanaoaminika na umma wa watanzania peke yake bali pia jumuiya za kimataifa na ulimwengu kwa ujumla.

Pia BAVICHA inapenda kutumia fursa hii kurekebisha kauli iliyotolewa na gazeti moja la kila siku hapa nchini kuwa BAVICHA ilikwenda Sydney kuomba misaada.

Taarifa hiyo ilipotosha maudhui ya safari hii kwani kama mwanachama BAVICHA ilihudhuria mkutano huo na ilichofanya ni kuripoti hali halisi ya kisiasa inavyoendela hapa nchini kama walivyofanya wengine kwa nchi zao ili pia kuwapa fursa wajumbe wengine wa mkutano huo kujifunza jinsi ya kuendesha siasa kwa kua moja ya malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu katika mambo haya hususani kwa vijana.

Aidha, ni imani ya BAVICHA kuwa matatizo ya nchi hii kamwe hayawezi kutatuliwa kwa misaada kutoka nje ya nchi. Tunaamini kuwa matatizo ya watanzania yatatatuliwa na watanzania wenyewe kupitia viongozi bora wenye maono na malengo thabiti ya kizalendo pasi kutegemea wageni na kama wageni hawa wataona haja ya kusaidia basi watafanya hivyo kwa kuunga mkono tuu juhudi hizi pasi kupigiwa magoti, utamaduni ambao umekua ukiendekezwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambao unaishushia hadhi nchi yetu.BAVICHA na Chadema kwa ujumla haitakaa hata siku moja kuabudu misaada ya nje ili kutatua matatizo ya watanzania.
Imetolewa leo tarehe 16/02/2012, Dar es salaam na;
Deogratias Siale
Katibu Mkuu BAVICHA Taifa

Bravoo CDM, Bravoo BAVICHA, Bravoo Heche na Bravoo katibu mkuu kwa kuiwakilisha vema taasisi ako uko australia mpaka wakaona ni vema wamteue mwenyekiti wenu kuwa mjumbe wa bodi. UV - masaburi endeleeni kupigani matumbo yenu na makundi yenu.
 
hawa wengine walikuwa wanachinja Ng'ombe CCM Kirumba
 
chadema endelezeni moto wa kuiimarisha BAVICHA hii ndiyo taasis yenye jeshi la muda mrefu ndani ya chama chenu hii ndiyo tanuri la kupika viongozi wenu wa badae HECHE anapokwenda vikao huko nje AVITUMIE kuwaokoa vijana kifkra na namna ya kuliokoa taifa dhidi ya mambo mengi yanayoliangamiza taifa tumpe moyo yeye na katibu wake na wajumbe wote wa baraza wapate uzoefu wa kutosha tusiwakatishe tamaa dhidi ya majungu tusiwavizie eti ni wapi watakosea ikizingatiwa ndiyo BARAZA la kwanza la vijana kusimama tuwape muda sasa wafye ke vichaka VIVA BAVICHA HONGERA KAMANDA HECHE INAALLAH MASWAABHRINA
 
safi sana ndugu yangu mura tunakutakia mafanikio mema kiongozi makini na mtarajiwa
 
Hivi Yule Grayson Nyakunguru au manyori nyakuguru...yuko wapi...
 
Back
Top Bottom