Heche kuongoza vijana Africa

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, ameteuliwa na bodi ya Umoja wa Vijana wa Vyama vya Mrengo wa Kati Duniani(IYDU) kuwa mjumbe. Bodi mpya ya IYDU iliyoketi jijini Sydney Australia kuanzia Januari 8 hadi 14 ambapo Bavicha iliwakilishwa na Katibu Mkuu wake Deogratias Siale, imemteua John Heche, kuwa mjumbe mshiriki ambapo atakuwa akisimamia masuala ya Afrika.

International Young Democrat Union (IYDU) is an global alliance of centre-right political youth organisations. Established in 1981, then re-established in1991, the IYDU has 130 full and observer members from over 80 countries and is the youth wing of the International Democrat Union (IDU).
 
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, ameteuliwa na bodi ya Umoja wa Vijana wa Vyama vya Mrengo wa Kati Duniani(IYDU) kuwa mjumbe. Bodi mpya ya IYDU iliyoketi jijini Sydney Australia kuanzia Januari 8 hadi 14 ambapo Bavicha iliwakilishwa na Katibu Mkuu wake Deogratias Siale, imemteua John Heche, kuwa mjumbe mshiriki ambapo atakuwa akisimamia masuala ya Afrika.

International Young Democrat Union (IYDU) is
an global alliance of centre-right political youth organisations. Established in 1981, then re-established in1991, the IYDU has 130 full and observer members from over 80 countries and is the youth wing of the International Democrat Union (IDU).
Ni nafasi nzuri kuongeza uzoefu na kujifunza mengi kutoka pande zingine za dunia. Congratulation Mr. Heche for the post!!
 
hongera heche,kajifunze demokrasi ya kweli na wengine huku.pia kale ka lugha ketu ka pale malimbe(duche) katanyooka sasa
 
hii inatokana na mkakati imara wa cdm kuwapika na kuwafunda vijana tangu wakiwa kwenye vyuo na baada ya kujiunga na chama hii ni hazina kubwa ya viongozi wetu wa badae
 
Congratulations for nomination, this is a chance for political exposure worldwide. Bravo bro!
 
Wakuu hii ndio habari kutoka BAVICHA niliyofanikiwa kuidaka. Jisomeeni mwenyewe bandugu.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BAVICHA KUWA MJUMBE WA BODI YA INTERNATIONAL YOUNG DEMOCRAT UNION (IYDU)
Umoja wa Vijana wa Vyama vya Mrengo wa Kati Duniani (International Young Democrat Union, IYDU) ulifanya mkutano wake mkuu nchini Australia uliokutanisha vijana zaidi 120 kutoka nchi mbalimbali kuanzia tarehe 8- 14 Jan 2012 ambapo BAVICHA kama mwanachama wa umoja huu iliwakilishwa na katibu Mkuu wake Deogratias Siale.

Mkutano huu pamoja na mambo mengine ulikuwa na agenda ya uchaguzi wa viongozi kwa nafasi za mwenyekiti, naibu mwenyekiti, makamu wenyeviti 10 na mweka hazina. Katika uchaguzi huo, Bara la Africa lilikuwa na wagombea wawili katika nafasi ya makamu mwenyekiti ambao ni Charles Owerdu kutoka Ghana na John Heche, Mwenyekiti wa BAVICHA aliyependekezwa kuwania nafasi hiyo na nchi za Ufaransa, Ugiriki na Ujerumani.

Demokrasia ilichukua mkondo wake ambapo wagombea wote wawili kutoka Afrika hawakupata kura za kutosha kushinda nafasi hiyo ambapo makamu wote 10 walitoka nchi za Ulaya, Amerika na Amerika ya Kusini na Bara la Afrika lilikosa mwakilishi katika bodi ya uongozi wa IYDU.

Hivyo basi, bodi mpya ya IYDU iliyoketi jijini Sydney imemteua John Heche, mwenyekiti wa BAVICHA kuwa mjumbe mshiriki wa bodi ya IYDU ambapo atakuwa akisimamia masuala ya Afrika. Pia bodi hiyo imemteua Mercy Gakuya wa chama cha DP cha Kenya kushirikiana na Heche katika kusimamia mambo ya Afrika ambao kwa pamoja watakuwa wakihudhuria vikao vyote vya bodi hiyo kwa mwaka mzima.

Hii ni fursa muhimu kwa BAVICHA na vijana wote wa Tanzania wanaohitaji mabadiliko na uhuru wa kweli kwani pamoja na mambo mengine itasaidia kuendelea kupata uzoefu, ujuzi na maarifa ya kuendesha mapambano ya kudai haki.

Uteuzi huu unaendelea kuthibitisha kuwa Chadema siku zote kimekuwa kikipika na kutoa viongozi, si tu wanaoaminika na umma wa watanzania peke yake bali pia jumuiya za kimataifa na ulimwengu kwa ujumla.

Pia BAVICHA inapenda kutumia fursa hii kurekebisha kauli iliyotolewa na gazeti moja la kila siku hapa nchini kuwa BAVICHA ilikwenda Sydney kuomba misaada.

Taarifa hiyo ilipotosha maudhui ya safari hii kwani kama mwanachama BAVICHA ilihudhuria mkutano huo na ilichofanya ni kuripoti hali halisi ya kisiasa inavyoendela hapa nchini kama walivyofanya wengine kwa nchi zao ili pia kuwapa fursa wajumbe wengine wa mkutano huo kujifunza jinsi ya kuendesha siasa kwa kua moja ya malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu katika mambo haya hususani kwa vijana.

Aidha, ni imani ya BAVICHA kuwa matatizo ya nchi hii kamwe hayawezi kutatuliwa kwa misaada kutoka nje ya nchi. Tunaamini kuwa matatizo ya watanzania yatatatuliwa na watanzania wenyewe kupitia viongozi bora wenye maono na malengo thabiti ya kizalendo pasi kutegemea wageni na kama wageni hawa wataona haja ya kusaidia basi watafanya hivyo kwa kuunga mkono tuu juhudi hizi pasi kupigiwa magoti, utamaduni ambao umekua ukiendekezwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambao unaishushia hadhi nchi yetu.BAVICHA na Chadema kwa ujumla haitakaa hata siku moja kuabudu misaada ya nje ili kutatua matatizo ya watanzania.
Imetolewa leo tarehe 16/02/2012, Dar es salaam na;
Deogratias Siale
Katibu Mkuu BAVICHA Taifa
 
Hongera sana kamanda,jifunze kwa wenzetu ili vijana wa sasa na wabadae wapate ujuzi kutoka kwako kwa lengo la kupata wapigania haki na rasilimali za taifa letu

bravo
 
mi nayashangaa mavijana ya CCM

song3.jpg
song2.jpg
 
Hongera sana Heche umeonyesha uthubutu, kuweza, na sasa songa mbele kwa mapambano dhidi ya waccm.
 
Duh yaani CHADEMA internationally known locally respected, hivi vyama vingine hapa Bongo hasa Umoja wa Vijana mna mikakati gani?
hapa naongelea CCM na CUF....
 
Back
Top Bottom